Muuza Kangala
JF-Expert Member
- Jul 21, 2021
- 1,138
- 4,213
Mwanamke mmoja mkazi wa Mtaa wa Nduka, Kata ya Chamwino jijini Dodoma, Rehema Shabani (41), amefariki duniani kwa kujimwagia mafuta ya taa na kujiwasha moto akiwa amejifungia chumbani kwake.
Tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa nne asubuhi huku chanzo kikiwa bado hakijafahamika.
Alisema mtoto wake kabla ya umauti kumfika alikuwa akiumwa kwa muda mrefu hali ambayo wakati mwingine ilikuwa ikimfanya kuchanganyikiwa.
“Alikuwa anaumwa kabla ya tukio hili hali ambayo ilikuwa inamfanya wakati mwingine kuwa kama mtu aliyechanganyikiwa na wakati mwingine kuwa sawa.
“Leo niliamka asubuhi yeye akiwa amelala, lakini badaye aliamka na kuniuliza mama unapika uji nikasema ndiyo akasema sawa akaondoka akaenda dukani baadaye akarudi baada ya kukuta duka limefungwa na kisha kurejea tena dukani,” alisema.
Nipashe