Dkt. Samizi ashiriki harambee ujenzi wa Kanisa Jimboni

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
328
414
Dkt. Florence George Samizi ameendelea kuwa mstari wa mbele kushiriki shughuli mbalimbali za maendeleo na kijamii katika Jimbo lake la Muhambwe mkoani Kigoma na wikendi hii Jumapili alishiriki misa takatifu iliyoendeshwa.

Mhashamu Baba Askofu wa Jimbo Kuu la Kigoma, Joseph Mlola kisha kushiriki harambee ya ujenzi wa kanisa iliyoongozwa na mgeni rasmi Jenerali Mstaafu Venance Mabeyo.

Kwenye harambee hiyo kiasi taslimu Tshs 81,865,500 zilipatikana huku ahadi zikiwa Tshs 37,450,000 na
Jumla kuu kuwa 119,315,500.

Mgeni rasmi aliunga mkono fedha taslimu Tshs 7,200,000 na ahadi ya Tshs 3,800,000.

Mbunge Samizi anaendelea kuwahimiza wadau wengine kuchangia harambee hiyo na kusisitiza kwamba michango inaendelea kupokelewa.

Dkt. Samizi ametoa pongezi nyingi kwa waumini wote kujitoa kwa moyo, kamati ya maandalizi, pongezi za pekee kwa Paroko Fr Deus kwa mipango mizuri ya kuiendeleza Parokia.

IMG-20231030-WA0023.jpg
IMG-20231030-WA0024.jpg
IMG-20231030-WA0025.jpg
IMG-20231030-WA0026.jpg
IMG-20231030-WA0012.jpg
IMG-20231030-WA0014.jpg
IMG-20231030-WA0015.jpg
IMG-20231030-WA0016.jpg
IMG-20231030-WA0019.jpg
IMG-20231030-WA0018.jpg
IMG-20231030-WA0020.jpg
IMG-20231030-WA0021.jpg
IMG-20231030-WA0022.jpg
IMG-20231030-WA0011.jpg
 
Back
Top Bottom