TANZIA Dkt. Masumbuko Lamwai afariki dunia

Makumbele

Member
May 9, 2009
65
390
9D28AB6F-68D5-4885-955D-8194D9A0055D.png


Aliwayewahi kuwa Mbunge wa Ubungo na Mbunge wa kuteuliwa na Rais, Dkt. Masumbuko Lamwai amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Mei 05, 2020.

Dkt. Lamwai atakumbukwa kama Mwanasiasa machachari, Mwanasheria nguli na Mkufunzi Mwandamizi (senior lecturer) wa Tumaini University.

Akiwa NCCR-Mageuzi, alikuwa na wanasiasa wengine wakongwe kama Mabere Marando, Marehemu Dk Sengondo Mvungi (RIP), Augustine Mrema, Makongoro Nyerere, Prince Bagenda, Ndimara Tegambwage, Stephen Wassira na wengine wengi.

Katika Uchaguzi Mkuu wa Vyama Vingi wa 1995, NCCR-Mageuzi walitetemesha na kutingisha nchi mpaka Mwl Nyerere akaingilia kati baada kusimama majukwaani CCM.

Baadae alijivua uanachama wa NCCR na kuhamia CCM.

Mwenyezi Mungu amjalie pumziko la amani.


MDOGO WA MAREHEMU DKT. LAMWAI, MH. JOSEPH SELASINI AZUNGUMZIA KIFO CHA KAKA YAKE

Kupitia mahojiano yake na kituo cha East Africa Radio asubuhi ya leo, Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini ameeleza hivi:

Dk Lamwai ni kaka yangu. Ni mtoto wa kwanza kuzaliwa katika familia ya Mzee Roman Selasini na Mama Katarina Roman.

Na kama kiongozi wa familia ametuongoza kwa hekima na busara mpaka mwisho wa uhai wake. Kama mtoto wa kwanza, ametutengenezea misingi mizuri katika familia.

Alikuwa ni mwanasheria aliyebobea katika mwenendo wa mashitaka pamoja na ushahidi (evidence and civil procedures)


MBUNGE PEKEE WA UPINZANI
Katika maisha yake ya kisiasa alipata kuwa diwani wa Manzese mwaka 1995 na baadaye alikuwa ni mbunge wa Ubungo na alikuwa mbunge pekee wa upinzani. Nakumbuka mwaka 1995 Tume ya Uchaguzi ilipofuta uchaguzi wa Mkoa wa Dar es Salaam yeye hakuafiki akaendelea na kumshinda marehemu Venance Ngula wakati huo. Alidumu kwa miaka miwili na baadaye mahakama ikatengua ubunge wake.

Kipindi kilichofuata Mh. Benjamin Mkapa alimteua kuwa Mbunge wa kuteuliwa na Rais. Hiyo ilikuwa baada ya kurejea CCM kutokea NCCR-Mageuzi. Amefariki akiwa ni mwanachama wa Chama cha Mapinduzi.

ALIKUWA HODARI, MWENYE MSIMAMO NA USHIRIKIANO
Namfahamu kama mtu hodari, mtu aliyekuwa na misimamo. Mtu ambaye alikuwa akikusudia jambo lake anapambana nalo mpaka ahakikishe limefika mwisho. Ni mtu alikuwa determined kwaakweli.

Alikuwa anashirikiana na watu kufanya jambo. Hata sisi wadogo zake alikuwa akituagiza hasubirii mrejesho, bali munakwenda wote.

Tumepata pengo kubwa katika familia. Tulipotelewa na wazazi na yeye alibaki kuwa kiongozi wetu na sasa ameondoka. Ni pengo ambalo halizibiki.


ALIPENDA KAZI YA UALIMU
Alipokuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alianzisha kampuni yake ya Uwakili inayoitwa Lamwai Advocates. Amefanikiwa kuwasomesha watoto wake wote wanne (4) ambao ni mawakili na wanashughulika na hiyo ofisi yake.

Baada ya kutoka Chuo Kikuu alikuwa ni mhadhiri wa Sheria wa Chuo Kikuu cha Tumaini - Dar es Salaam. Aliendelea na kazi hizo mbili: Kuendesha kampuni yake pamoja na hiyo ya Uhadhiri.

Kazi ya ualimu aliipenda sana. Ni kazi ya familia. Familia yetu ina wanasiasa wengi sana na walimu wengi. Kwahiyo alipenda sana kusomesha mpaka mwisho wa uhai wake.

AFYA KUDHOOFU NA UMAUTI
Afya yake ilidhoofu katika kipindi cha wiki mbili tatu zilizopita. Lakini pamoja na kudhoofu huko, alipigwa na malaria kali ambayo alikuwa anaendelea kupata dawa.

Hata Jumapili alikaa na watoto wake wakaongea sana ni vile tu hauwezi kujua Mungu amepanga nini. Jana usiku akazidiwa na katika safari ya kumpeleka hospitali, akafia njiani.

Kwa sasa mwili umehifadhiwa Hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es salaam.

=====

SOMA: BAADHI YA KESI ALIZOWAHI KUSIMAMIA
Jinsi mbunge Ramadhan Kihiyo alivyojiuzulu baada ya kashfa ya kufoji vyeti - JamiiForums

Mbunge wa Longido Onesmo Nangole (CHADEMA) huenda akavuliwa ubunge kwa kufoji elimu - JamiiForums

Sarah Simbaulanga: Mwanamke wa kwanza kuiba pesa ndefu katika historia ya benki zote nchini - JamiiForums

---
MACHACHE KUMHUSU

1. Ndiye mtanzania wa kwanza kutunukiwa Shahada ya udaktari wa Falsafa katika sheria (Criminal and Procedural Law - LLD) Chuo Kikuu Oxford, moja ya vyuo vinavyoheshimika sana duniani.

2. Ndiye mwanafunzi wa kwanza kutoka Afrika kusoma kozi ya miaka minne kwa miaka miwili chuoni hapo. PhD in Criminal &Procedural Law (Oxford) ni miaka minne (full time) na miaka 6 hadi 8 (part time). Lakini Lamwai aliomba kusoma miaka miwili na akahitimu.

3. Mwanzoni mwa miaka ya 1990 akiwa Mhadhiri UDSM alishirikiana na wanaharakati wenzie kuanzisha vuguvugu la kudai mfumo wa vyama vingi.

4. Mwaka 1994 aligombea udiwani Kata ya Manzese kupitia NCCR. Alishinda lakini CCM wakachakachua. Akaenda Mahakamani matokeo yakabatilishwa. Uchaguzi ukarudiwa, akagombea na kushinda.

5. Akiwa diwani pekee wa upinzani Manispaa ya Kinondoni aligombea Umeya na kupata kura moja (ya kwake). Alipoulizwa kwanini aligombea wakati alijua hatashinda, alijibu "nisingegombea ningelazimika kumpigia mgombea wa CCM au kuharibu kura. Yote mawili ni makosa. Hivyo niliamua kugombea ili nimpe kura mgombea sahihi"
_
6. Ndiye Mbunge wa kwanza wa upinzani jimbo la Ubungo baada ya kushinda uchaguzi mkuu 1995.

7. Yeye na Mabere Marando wakiwa bungeni waligomea kiapo cha Utii kwa Rais, kwahoja kuwa wabunge hawapaswi kumtii Rais kwa sababu bunge ni mhimili unaojitegemea. Baada ya mabishano makali ya kisheria, Spika Msekwa alikubaliana na hoja yao. Kiapo cha wabunge kikafanyiwa marekebisho na kuondoa sehemu ya "utii kwa Rais" kisha wabunge wote wakaapa upya.

8. Mwaka 1996 aliongoza kesi maarufu ya uchaguzi iliyomvua ubunge aliyekua Mbunge wa Temeke, Ramadhani Kihiyo kutokana na kughushi taarifa za elimu yake. Mbali na kesi hiyo ameshiriki pia kusimamia kesi mbalimbali nje na ndani ya nchi. Mwaka 2006 alishiriki kuandaa muongozo wa Haki za binadamu kwa nchi za jumuiya ya madola.

9. Mwaka 1999 baada ya kupitia misukosuko mingi ya kisiasa ikiwemo mali zake kupigwa mnada, kufilisiwa na kufutiwa leseni ya uwakili aliamua kurudi CCM.

10. Dr.Masumbuko Lamwai ni kaka yake Mhe.Joseph Selasini (Mbunge wa Rombo). Majina yake kamili ni Dr.Emmanuel Masumbuko Roman Selasini Lamwai.!
 
Makumbele,
Nini kinawakumba CCM, RIP msomi mwanasheria Dr. Masumbuko Lamwai.
spacer.gif


Photo and profile
Lawyer: Dr. MASUMBUKO LAMWAI
Country: TANZANIA

LEGAL EDUCATION: University of Dar es Salaam (Faculty of Law)
FAME: Successful litigation; Civil Procedure & Practice; Criminal Law; M.P (Ubungo); Mageuzi Architect; Lecturer (UDSM's Faculty of Law
Title :Senior Lecturer
Office :Faculty of Law in the Department of Legal Theory
Email :
Tel :
EDUCATION

LL.D (London)
LL.M (1978) UDSM,
LL.B (1976) UDSM

Kesi tajwa alizosimamia Dr. Masumbuko Lamwai
Juni 10, 2016
MLALAMIKIWA wa kwanza katika kesi ya uchaguzi Jimbo la Longido mkoa wa Arusha, Mbunge wa Longido, Onesmo Ole Nangole (CHADEMA), ameieleza Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kuwa anajua kusoma na kuandika Kiswahili, lakini hajui kusoma na kuandika Kiingereza.

Shahidi huyo wa kwanza kwa upande wa wajibu maombi, alisema hayo jana mbele ya Jaji Mfawidhi Kanda ya Bukoba, Silvangirwa Mwangesi aliyesikiliza kesi hiyo wakati akihojiwa na Wakili Dk Masumbuko Lamwai.

Wakili Lamwai alitoa Mahakamani hapo fomu iliyojazwa na Nangole, ambayo ameiprint kutoka katika tovuti ya Bunge la Jamhuri ya Muungano ikiwa na picha na kuiwasilisha Mahakamani hapo, na aliomba kuisoma mbele ya Jaji Mwangesi na inaonesha alisoma wapi mbunge huyo elimu ya sekondari.

Nangole aliisoma na kuonesha kuwa alisoma katika Shule ya Arusha Sekondari mwaka 2008 hadi 2011, wakati katika Mahakama hiyo amesema hakusoma sekondari na wala hajui kusoma na kuandika Kiingereza.

Wakili Lamwai alimuuliza Nangole kama katika mikutano ya kampeni yeye na wafuasi wake, walitumia lugha za kashfa dhidi ya mgombea wa CCM, Dk Stephen Kiruswa, ambapo alikana kutoa lugha hizo.

Lakini, alipopewa hati ya kiapo chake na kutakiwa kusoma, ilionesha kutamka maneno hayo katika mikutano ya hadhara na katika kiapo chake. Nangole alipotakiwa kusema mahakama iamini nini ili itoe maamuzi kwa kiapo alichoandika au alichosema mahakamani hapo, Nangole alikaa kimya na Jaji Mwangesi alimwamuru kujibu swali, ndipo aliposema hajui.

Aidha, Dk Lamwai alimuuliza katika timu yake iliyokuwa na watu 14, kama alihudhuria mikutano yote ya kampeni 68, Nangole alisema siyo yote alihudhuria na mingine ilikuwa ikihutubiwa na Karisti Lazaro wakati huo akiwa Katibu wa Chadema Wilaya ya Arusha, sasa ni Meya wa Jiji la Arusha na Isack Joseph maarufu kwa jina la Kadogoo, sasa ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli.

Shahidi huyo alioneshwa picha na wakili Lamwai, ambayo ni ushahidi uliotolewa kama kielelezo P5c cha matukio ndani ya chumba cha kuhesabu kura, akiwemo mbunge na wafuasi wake wakiwa mbele ya kompyuta iliyovurugwa ;na kumuuliza ni kwa nini walikuwa wengi ndani ya chumba hicho kinyume cha sheria, shahidi alijibu hajui.

Aliulizwa na Wakili Lamwai, kama kulikuwa na wafuasi wengi wa CCM ndani ya chumba hicho, mbunge huyo alikiri kutokuwepo katika chumba hicho wafuasi wa chama hicho tawala.

Baadhi ya mahojiano kati ya Wakili Lamwai na shahidi huyo wa kwanza wa upande wa mjibu maombi yalikuwa: Wakili: Kwa nini hukusoma kiapo chako? Shahidi: Naumwa macho.

Wakili: Sio kuwa hujui kusoma Kiingereza?

Shahidi: Hapana.

Wakili: Sekondari ulisoma wapi?

Shahidi: Sikusoma.

Wakili: Elimu ya sekondari ulisoma shule gani?

Shahidi: Sikusoma sekondari.

Wakili: Katika fomu yako uliyoandika siku unajiandikisha bungeni ambayo nimeiprint katika tovuti ya Bunge la Jamhuri ya Muungano, hii hapa, inaonesha umeandika umesoma wapi sekondari? Katika shule ya Arusha sekondari.

Shahidi: Sijui mimi, sikuandika mimi hiyo.

Wakili: Unajua kusoma na kuandika Kiingereza?

Shahidi: Sijui.

Wakili: Kwanini umesomewa kiapo chako kilichoandikwa Kiingereza na wakili wako, ni kwa sababu hujui Kiingereza?

Shahidi: Najua kusoma na kuandika Kiswahili.

Wakili: Unajua Kiingereza?

Shahidi: Kimya.

Jaji: Jibu swali. Mbona maswali ni rahisi tu pamoja na kwamba yanauma…jibu tu.

Shahidi: Sijui kusoma Kiingereza wala kuandika.

Wakili: Katika maisha yako yote ya miaka 23 uliyokuwa CCM ulikuwa na vyeo mbalimbali.

Shahidi: Ndio. Wakili: Ulihama CCM kumfuata Edward Lowassa CHADEMA sio?

Shahidi: Ndio, unauliza jibu.

Wakili: Ulifanya hivyo ili ubebwe na Lowassa katika ubunge Longido sio?

Shahidi: Ndio jibu unalo.
Source: HABARILEO Mbunge wa Longido Onesmo Nangole (CHADEMA) huenda akavuliwa ubunge kwa kufoji elimu - JamiiForums
 
Ni miongoni mwa wanasiasa walioisisimua sana Tanzania miaka ya tisini. Mungu ampumzishe kwa amani, amina.
Naam, nakumbuka uchaguzi wa mdogo wa Temeke mwaka 1996..pale Mwembe Yanga Kuna uzushi ulitokea kuwa CCM wameficha kura ofisi ya mtaa,jamaa ilibidi waingie yeye na Makongoro Hadi darini kuzisaka kura feki!

Vijana wa CCM tulikuwa na wakati mgumu Sana Uchaguzi! Kabla ya Happ alikuwa amemtesa Mahakamani Ramadhan Kihiyo ,mwanafunzi hewa wa DIT mwaka1973!
 
View attachment 1440056

Aliwayewahi kuwa mbunge wa Ubungo na mbunge wa kuteuliwa na Rais, Dkt. Masumbuko Lamwai amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Mei 05, 2020...
Daah R.I.P jembe nakumbuka kipindi Cha mzee wa kiraracha, Augustino lyatonga mrema ulichachafya vya kutosha CCM mpaka CCM wakakufungia kutokufanya kazi ya uwakili tanganyika
 
Back
Top Bottom