Dkt. Magufuli akagua ujenzi nyumba za Serikali

Kaza kamba Ndugu Mungu na watanzania wapo wanakuona kwa kazi za mikono yako!
 
Nadhani tatizo ni jinsi ya kujieleza ndio ilikuwa tatizo ila ki ukweli zile nyumba zilikuwa zimepitwa na wakati sana.
Madhalani, nyingi zilikuwa hazina master bedroom mlikuwa mnashare bafu watoto, mama na baba, kwa wakati huu mtanzania wa kipato cha kati hawezi kukubali kushare bafu na watoto.

Pili, kama kuna mtu alibahatika kwenda kwenye zile nyumba atakubaliana na mimi zilikuwa zimefikia life span yake zilitakiwa kubomolewa na zijengwe mpya.

Shida kwangu kwa nini hawakubomoa baadhi ya nyumba maeneo yale na wakadesign nyumba mpya kwa kupunguza ukubwa wa maeneo na kupata nyumba nyingi zaidi?
Nadhani suala la kuuziwa wafanyakazi ilikuwa ni mojawapo ya mapendekezo ya ripoti na hapo ukumbuke serikali ilikuwa na akina Chenge, Lowassa, Mramba, Yona nk. Hapo ndio Magufuli asingeweza kufurukuta hata maka anaipenda nchi kiasi gani bali ni kusimamia ujenzi wa nyumba mpya kwa kasi ili aweze kupambana na propaganda zilizokuwa zinajitokeza.

Kulikuwa kuna mambo mawili ambayo magufuli alikuwa anatakiwa either achaguwe kufanya kujiuzuru au kupambana ndani ya system na kuwaonyesha watanzania kuwa ni mpambanaji.

Yeye aliamua kubaki na kupambana ndani ya system, na cha kwanza ni kuanza ujenzi wa nyumba mpya mara moja hata kama serikali ina hali mbaya ya kifedha. Na hii ndio uongozi si kukimbia tatizo bali kupambana na kurekebisha tatizo kwa kutafuta njia mbadala.

Hili la ujenzi wa nyumba lazima tumpe sifa zake kwa sababu ameweza kupambana zikajengwa, pili nadhani amepanua mawazo kwamba serikali inabidi iwe inawekeza kwenye nyumba mpya ndio inasaidia ukuaji wa maeneo na pili inaongeza ukuaji wa uchumi hasa kwa kutoa ajira kwa vijana.

Wazo langu binafsi nadhani kuna haja ya serikali kwa siku za baadae hata kwenda kwenye mapori kujenga majengo ya ofisi na wizara mapya na huku mjini ambako kumejaa waachane nako itasaidia kupunguza foleni

Umenena Mkuu, Magufuli ni mmoja wa viongozi wanaofanya vizuri sana lkn hilo haliondoi mabaya aliyofanya pia. Binadamu tunajifunza siku zote pengine hakujua madhara ya maamuzi ya pamoja waliofanya hivyo hatuna budi kusamehe lkn hapo hapo kumueleza ukweli ili ajitambue. Kama kipindi kile wangefikia maamuzi ya kuzibomoa na kujenga nyumba za ghorofa kwy maeneo yale makubwa leo wafanyakazi wasingekuwa wanakaa mbali na shm zao za kazi, hivyo kupunguza ukali wa maisha hasa ukizingatia mabadiliko ya nauli za kila kukicha
 
Mpaka sasa hizi nyumba hazina finishing ya ceiling board, zina badi hafifu, kama hazitapigwa rangi zitaoza hivi karibuni, mkandarasi si mbunifu kila nyumba hazidi mil 18. watangaza 50m hapo.
 
Umenena Mkuu, Magufuli ni mmoja wa viongozi wanaofanya vizuri sana lkn hilo haliondoi mabaya aliyofanya pia. Binadamu tunajifunza siku zote pengine hakujua madhara ya maamuzi ya pamoja waliofanya hivyo hatuna budi kusamehe lkn hapo hapo kumueleza ukweli ili ajitambue. Kama kipindi kile wangefikia maamuzi ya kuzibomoa na kujenga nyumba za ghorofa kwy maeneo yale makubwa leo wafanyakazi wasingekuwa wanakaa mbali na shm zao za kazi, hivyo kupunguza ukali wa maisha hasa ukizingatia mabadiliko ya nauli za kila kukicha

Mkuu ukiangali majibu ya Sumaye kwa nini nyumba ziluzwa na hasa hizo za Oysterbay unazozisema utagundua ililazimu kuziuza, angalia hapa:

Last edited by a moderator:
Mkuu ukiangali majibu ya Sumaye kwa nini nyumba ziluzwa na hasa hizo za Oysterbay unazozisema utagundua ililazimu kuziuza, angalia hapa:

Maelezo ya Sumaye yanajichanganya, kwamba nyumba zilibinafsishwa kwa makosa ya ubinafishaji wakakuta zinakaliwa na wageni hata wakiangalia mitaa muhimu ni ya wageni. Ukiangalia hapo hiyo sio sbb ya kuuza kwani wangeziacha chini ya himaya ya serikali kungekuwa na tatizo gani? Kilichotakiwa hapo ni innovation ya hizo nyumba au kuzibomoa na kujenga upya nyumba zingine ambazo zingekaliwa na watu wengi hasa kwa ukubwa wa maeneo zilizonazo lkn kimechofanyika ni kujimilikisha ili nao wawe wamiliki km walivyo wageni
 
Kama Sumaye hujamuelewa, basi huyo unayebishana naye asimalize muda wake utamchosha bure tu.
 
Kama Sumaye hujamuelewa, basi huyo unayebishana naye asimalize muda wake utamchosha bure tu.

Hapa hakuna kubishana tunatofautiana kwa hoja ndio maana ya jukwaa hili. Anayebisha ni yule anayesimama kwy misimamo yake hata km yupo wrong. Tunaweza kuona au kusikiliza wote lkn tukatofautiana kukichambua kile kilichosemwa. Tusijaribu kuwa na mahaba kwa tunaowapenda tukashindwa kutanua wigo wetu wa kufikiri
 
Wakala wa Nyumba Tanzania - TBA, wanafanya kazi kubwa sana kwenye ujenzi wa nyumba za viongozi na wafanyakazi wa serikali. Hizi ni baadhi nimezipata katika ziara yangu kusini.

IMG-20150703-WA0077.jpg
20150704_220805.jpg
Nyumba ya Jaji Mbeya

IMG-20150703-WA0023.jpg
IMG-20150703-WA0000.jpg
Nyumba ya Jaji Songea, Ruvuma.​
 
Back
Top Bottom