Dkt. Kigwangalla: Ripoti ya CAG ni ya uongo, nimechafuliwa sana. Prof. Adolf Mkenda ndiye aliyeratibu mimi kuchafuliwa

John Haramba

JF-Expert Member
Feb 4, 2022
365
1,373
Nukuu za Hamis Kigwangalla, Mbunge wa Nzega Vijijini kuhusu ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

"Kwa kawaida katika taarifa za CAG huwa kuna hoja nyingi, hoja hizo zinapelekea kamati ya PAC kuzijadili na kuwasilisha taarifa zake bungeni. Katika taarifa zake CAG si kwamba alinigusa tu mimi kama Kigwangalla bali alinigusa kama Waziri wa Maliasili na Utalii.

"Taarifa ya CAG iligusia vitu vingi vidogo vidogo ambavyo CAG hakuvithibitisha na kupelekea kunichafua mimi binafsi kama Kigwangalla na kunisababishia maumivu binafsi mimi na wapendwa wangu pamoja na maumivu ya kisiasa jimboni kwangu.

"Kwa kuwa mimi ni mbunge mzoefu sikutaka kujibu maelezo aliyoyatoa CAG kwenye taarifa iliyoishia Juni 2020, hakuishia hapo hata mwaka jana pia alirudia maelezo yaleyale licha ya mimi kumpa CAG taarifa sahihi. Mimi nilinyamaza kwa kuwa naheshimu Taasisi ya CAG.

"Nimechafuliwa sana, nimeonewa sana na kwa muda mrefu nimeamua kunyamaza kwa ajili ya kuheshimu sheria, kanuni na taratibu zilizopo. Umefika wakati wa mimi kusema, nitasema kwa sababu uongo ukirudiwa rudiwa sana bila kurekebishwa huaminiwa.

"Nimeamua kusema ili kusafisha taswira yangu katika jamii na miongoni mwa Wabunge na mashabiki wangu katika harakati za kisiasa. Kwanza, ninakanusha tuhuma zote zilizoandikwa kwenye ripoti ya CAG kuhusu mimi ni za uongo na hakuna hata moja ni ya kweli.

"Sijawahi kula rushwa wala fedha katika wizara ambayo nilikuwa naisimamia (Wizara ya Maliasili na Utalii), na kimsingi niliisimamia Wizara hiyo kwa uzalendo na kwa kutumia vipawa vyangu vyote.

"Nilikuta Wizara ya Maliasili na Utalii inapokea watalii takribani 940,000 na mimi nikafanikisha kuongeza idadi hadi kufikia watalii 1,600,000 kwa mwaka, na wizara ilikuwa inachangia pato la Taifa takribani trilioni 3 mimi nikaongeze hadi kufikia trilioni 6.5.

“Katika taarifa ya CAG inayoishia Juni 2020 CAG amesema katika Tamasha la Urithi shilingi bilioni 2.085 zilitumika nje ya bajeti, haya siyo maelezo sahihi, na bajeti ya Tamasha la Urithi ilitungwa tangu mwaka uliopita na kuwekwa katika kila Idara ya Wizara.

"Agosti 4, 2018 nilipata ajali na Tamasha lilikuwa linafanyika Septemba, 2018. Wakati wanaamua wawape Clouds Media matangazo, TBC kurusha live, sikuwepo ofisini, lakini bado CAG alikuwa anarudia kusema kuwa mimi ndiyo niliyeidhinisha taasisi hizo zipewe fedha.

“Kwa mazingira yalivyokuwa ninaamini aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili, Profesa Adolf Mkenda ndiye aliyeratibu mambo yote ya mimi kuchafuliwa, alikuwa akipeleka documents kwa Rais kila mara mpaka Rais Magufuli akaniita na kuniuliza mgogoro wetu.

“Nilimwambia Profesa Mkenda ni mvivu hakai ofisini, yuko bize na kampeni kwao Moshi, anataka kwenda kugombea. Ilifika hatua nikamuomba Rais anipumzishe kwa kuandika barua yenye kurasa tano ili Wizara iwe salama.

“Haikujibiwa, baadaye nikaandika barua nyingine ndipo tukaitwa na Katibu Mkuu Kiongozi kwenda kupatanishwa, tuhuma alizozitoa kwenye kikao hicho ndizo hizohizo zilizomo kwenye ripoti ya CAG."
 
Prof Mkenda atakuwa mjinga kweli kweli iwapo atakubali kuingia katika huu mkenge wa kujibizana na Dr Kigwangallah.

Dr Kigwangallah bila uWaziri au uSpika haoni faida ya ubunge.Kwake yeye ubunge ni daraja tu la kupata madaraka.

Report ya CAG inaandaliwa na wataalam wabobezi katika fani ya uhasibu/wakaguzi.Kabla report haijatoka hoja zote urejeshwa kwa watuhumiwa,sasa leo mwaka wa pili unakurupika na kuwatwisha mzigo wengine.

Dr Kigwangallah alikuwa ni Waziri wa TANAPA kila siku anazurura na ndege za TANAPA,hadi Dr Magufuli aliwahi kulisema hili.

Dr Kigwangallah alimteua ndugu yake alikuwa mhasibu wa Kanda TANAPA na kumpeleka Ngorongoro kuwa Mkurugenzi wa fedha halafu leo hii anajifanya hakutoa amri ya kuchota fedha za taasisi zilikuwa chini ya Wizara ya maliasili na Utalii.

Ni huyu huyu Kigwangallah aliyemchukua mtumishi wa TANAPA na kumfanya Katibu myeka wake badala ya kuwatumia watumishi wa Wizara.

Dr Kigwangallah alikuwa haonekani Wizarani kila siku yuko Arusha ungefikiri Wizara ya maliasili ipo Arusha.

Kibaya zaidi alikuwa akipitisha Mambo yake mabaya kwa Naibu Katibu Mkuu kwakuwa Katibu Mkuu alikuwa akimkatalia.
 
Back
Top Bottom