Dkt. Janabi na Wanaharakati wa Afya tuache upotoshaji. Nchi ina tatizo kubwa la Utapiamlo na sio uzito wala unene

Leo ninaandika nikiwa na hasira zilizochanganyikana na huzuni kwa upotoshaji mkubwa unaofanywa na huyu daktari pamoja na madaktari wengine uchwara wanaolazimisha ionekane kuwa nchi ipo kwenye tatizo kubwa la unene uliopitiliza wakati ni kinyume chake.

Tumekuwa tukiwasikia msile wanga mara usikun kuleni tu matunda na maji mengi wakati wananchi wengi wanakula tu ili kuzuia msiba na sio kuzingatia mlo kamili kwasababu ya umaskini.

Hizo nguvu mnazotumia kwa ajili ya kikundi cha watu wachache mngetumia kuonyesha ukubwa wa tatizo la lishe kwa wananchi mngepata thawabu. Dr Janabi huna tofauti na mke wa mfalme wa Ufaransa aliyesema watu kama hawana mikate wale keki.

Kwa mujibu wa mtandao wa STATISTA hadi kufikia November 2021 kulikuwa na 31.8% ya watoto wa chini ya miaka miatno wenye utapiamlo uliokithiri (Chronic Malnutrition). Ni 4% tu ya watoto huzaliwa wakiwa overweight.

Kimsingi hivyo vyakula anavyosema Janabi watu wasile ni ndoto za watanzania wengi kuvipata angalau mara moja kwa siku. Mikoa mingi ya Tanzania inakabiliwa na tatizo la lishe. Ninachoona ni ndugu Janabi kudhani maisha anayoishi yeye ndo wanayoishi watanzania wote. ASIJISAHAU

Ninatoa wito kwa serikali za mitaa kupambana ili mashuleni watoto wawe wanapata chakula. Wale wazazi/ walezi wapumbavu wanaokataa kuchangia vyakula kwa kisingizio cha ELIMU BURE wakamatwe watupwe tu ndani maana wanaturudisha nyuma. Haihitaji utafiti kujua kama kuna tatizo kubwa la lishe karibu maeneo yote nchini.
Acha wivu we chawa

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Shida siyo kula milo miwili


Hata ukila mara 5 Kwa siku, Kwa ulaji wetu wa vyakula vya sukari, wanga na mafuta/fat nyingi ni sio lishe

Halafu mwili wako unahitaji chakula kidogo sana tofauti na unavyojua.

Mwili hauhitaji tule kama tunavyokula ni mazoea tu ya hovyo


Halafu pia unaweza kula vizuri Kwa pesa ndogo tu
Ni kweli ukisemacho mimi point yangu ni kwamba tusiweke siasa kwenye maisha ya watu.

Swala la sukari badala ya kuja na suluhisho mtu anaweka siasa mara oh kuna tatizo la uzito uliopita kiasi, watu wanadhalilisha taaluma kwa nini wasikae kimya kama hawana la maana kuzungumza.
 
Kwahio watu wanaokula vizuri mfano Ulaya na Japan, hawafi kwa sukari Wala presha? Wao vifo vyao vinatokana na nini? Mwili wa binadamu ni Kama mazao ya musimu mfano mahindi, hata ukiendelea kupalilia na kuweka mbolea baada ya miezi sita yatakauka na kufa, uhai umefika mwisho
Sijasema hawafi ila sio kwa kiwango kikubwa kama nchi za kusini mwa jangwa la Sahara. Vifo vinavyo tokana na Magonjwa yasiyo ambukiza duniani ni 31% na katika idadi hiyo 76% wanatokea kusini mwa jangwa la Sahara (WHO, 2023).
 
Watanzania kawaida hawapendi kuambiwa mambo yanayokaraisha nafsi zao.....wao wanapenda kusikia mambo mazuri......na ndio maana wamekuwa fursa kwa wachungaji na mitume matapeli wanaowalisha maneno matamu huku wakivuna mamilioni.......

Prof Janabi kwa nafasi yake lazima awahusie watu juu ya madhara ya mitindo mibaya ya maisha kitu ambacho waTanzania hawapendi kukisikia....

Takwimu ziko wazi kuwa kumekuwa na ongezeko la wagonjwa wa maradhi hayo pamoja na mengine yanayohusiana na mitindo mibovu ya maisha.........na bahati mbaya kutokana na vipato vyetu kushindwa kumudu gharama za matibabu............

Sasa kwanini tusichukue tahadhari kabla ya hatari.........

Mkiambiwa na watalaamu mnaanza matusi na kejeli.......

Matumizi makubwa ya sukari, pombe Kali na pombe zingine na vyakula vya viwandani hatari kwa afya zetu.......

Inawezekana takwimu za obesity zisiwe kubwa kulinganisha na mataifa lakini kama taifa tunatakiwa kuchukua tahadhari ili tusifikie huko....kwa kuwa hata hao wenye takwimu kubwa hawapendi hali na wanachukua hatua kupambana na hali hiyo...........

Prof Janabi endelea kuwakumbusha hata kama hawapendi lakini iko siku watakumbuka maneno yako wakiwa vitandani.......
upo sahihi mkuu
 
Inasemekana huyu propesa anaukichaa.akiwa mdogo alitibiwa milembe.yawezekana ukichaa haukaisha
 
Back
Top Bottom