Dkt. Doto Biteko: Mradi wa JNHPP unatarajiwa kuingiza Megawati 235 katika Gridi ya Taifa mwezi huu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko, leo Februari 19, 2024 amewasili mkoani Mbeya kwa ziara ya kikazi mkoani humo.

Ziara hiyo pia itahusisha ukaguzi wa miradi mbalimbali ya umeme mkoani humo.
Screenshot 2024-02-19 175959.png

Screenshot 2024-02-19 175916.png
Akiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe, Dkt. Biteko amepokelewa na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera.

Katika kikao chake na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Dkt. Biteko ameeleza jitihada zinazofanywa na Serikali katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu, Siasa na Nishati.

Katika Sekta ya Nishati, Dkt. Biteko ameeleza kuwa, upungufu wa umeme nchini ni kati ya megawati 300 hadi 190 lakini kwa sasa kuna matumaini makubwa kwani mradi wa Julius Nyerere (JNHPP) unatarajiwa kuingiza megawati 235 katika gridi ya Taifa mwezi huu na matumaini mengine ni kutoka Mradi wa umeme wa Rusumo ambao utaingiza katika gridi megawati 27.

Amesema kuwa, kiasi hicho cha umeme kitakapoingia kwenye gridi ya Taifa kitaondoa hali ya sasa ya mahitaji ya umeme kuwa makubwa kuliko uzalishaji na pia kuiwezesha Serikali kuendelea kufanya maboresho kwenye miundombinu ya umeme.

Amesema kuwa, kwa Mkoa wa Mbeya ambao mahitaji yake ni kati ya megawati 70 na 74 ambapo kwa sasa wanapata umeme wa megawati 51 na kueleza kuwa, jitihada zinazoendelea sasa zitapelekea Mkoa huo pia kupata umeme kulingana na mahitaji.

Katika hatua nyingine, Dkt. Biteko amepongeza Mkoa wa Mbeya kwa kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato, utekelezaji wa miradi ya maendeleo pamoja na usimamizi mzuri wa sekta Elimu ambao watoto wanaostahili kwenda shule wameripoti kwa zaidi ya asilimia 70.

Vilevile, Dkt. Biteko amesisitiza viongozi kufuata agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan la kuwa, tofauti ya itikadi ya vyama vya siasa isifanye wananchi kuwa maadui bali watu wabishane kwa hoja huku kipaumbele kikiwa ni maendeleo ya nchi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera, amemueleza Dkt. Doto Biteko kuwa, shughuli za kiuchumi katika Mkoa huo zinaendelea vizuri na katika mwaka 2023/2024 walifanikiwa kukusanya mapato ya shilingi Bilioni 49 ikiwa ni zaidi ya asilimia 105.

Ameongeza kuwa, utekelezaji wa miradi ya umeme inaendelea vizuri ikiwemo ya upelekaji umeme vijijini, vitongojini na migodini.

Katika elimu amesema kuwa, Mkoa huo umekuwa na ufaulu mzuri huku watoto wanaopaswa kwenda shule, wakiripoti kwa zaidi ya asilimia 70.
===========For English Audience Only=============
Deputy Prime Minister and Minister of Energy, Dr. Doto Biteko, Visits Mbeya to Inspect Energy Projects

Deputy Prime Minister and Minister of Energy, Dr. Doto Biteko, arrived in Mbeya , February 19, 2024, for an official visit, including inspections of various energy projects in the region. During his meeting with Mbeya Regional Commissioner Juma Homera, they discussed about various government efforts in various sectors such as Education, Politics, and Energy.

In the energy sector, he emphasized the issues of power shortage due to current electricity deficit of 300 to 190 megawatts and this problem is expected to improve significantly. The Julius Nyerere Hydropower Project (JNHPP) is set to inject 235 megawatts into the national grid this month, with additional expectations from the Rusumo Power Project contributing 27 megawatts.

Dr. Biteko has explained the contribution of increasing electricity will address the current challenge of demand surpassing supply. He anticipates it will enable the government to continue infrastructure improvements in the energy sector. For Mbeya Region, where the current demand ranges between 70 and 74 megawatts, the ongoing efforts are expected to match the region's needs.

Furthermore, Dr. Biteko has congratulated Mbeya Region for its excellent performance in revenue collection, successful implementation of development projects, and effective management of the education sector. He praised the region for achieving a collection of over 105% of the target, amounting to 49 billion Tanzanian Shillings for the year 2023/2024.

Deputy prime minister insisted on President Samia Suluhu Hassan's call for political leaders to prioritize national development over ideological differences. He emphasized the importance of constructive debates while ensuring citizens are not divided along party lines.

However, Regional Commissioner Juma Homera, informed Dr. Biteko about the positive economic activities in the region. He highlighted the successful implementation of electrification projects in rural areas, urban centers, and mining areas. In the education sector, he reported a commendable academic performance, with over 70% of eligible children attending school.
 
Back
Top Bottom