Dkt. Bashiru Ally ''amkaanga'' Lazaro Nyalandu

Nyalandu ana kasha nyingi sana, ila kwa bahati mbaya zaidi Dr. amejibu kama kada na sio kama mwanataaluma
Ndio mkuu sasa hapa watu hawataki kujua kama dr ni mtaalamu na aliyakiwa kujibu kitaalamu,

Kibaya zaidi naziona kashfa za Nyalandu zikiishia mtandaoni tu
 
Na hao ndio "Think-tank" ya Tanzania.

"...kuwa mkweli dhidi ya tuhuma kwa watawala sio jambo rahisi...."
Oliver Tambo
Ukweli ni dhana tu kulingana na fikra zako!

Upungufu wa fikra unaweza kusababisha ukadhani suala/jambo fulani ni kweli wakati kwa wenye fikra pana wanajua sio kweli.
 
Kuna hoja ya Nyalandu anayodai kuhusu CCM kwa sasa kukosa dira.

Kwanza unaposema kwa sasa CCM imekosa dira wakati umekuwa ndani yake kwa kipindi kirefu inabidi utueleze, kipindi cha nyuma ilikuwa na dira gani?

Je, hiyo dira iliyokuwepo kipindi cha nyuma ilikuwa inaonekana kwenye chama alichojiunga nacho?

Hiyo dira iliyokuwepo kipindi cha nyuma ilimsaidiaje mwananchi hasa mwenye uwezo mdogo kielimu na kiuchumi?
Kamuulize Nyalandu hayo maswali tuone kama atashindwa kukujibu!
 
Mkuu;
Weka swali/hoja yenye mantiki ili upate jibu lenye mantiki.

Ninajibu hoja kulingana na aina ya swali/hoja.
Kuna ugumu gani ya kumwambia mtu swali lako siwezi kulijibu badala yake unamuelekeza sehemu uliyotolea hoja yako.

Ukija na hoja kuwa mkweli na jipange kwa swali lolote hata kama ni rubbish.

Hekima, ukweli ni vitu muhimu sana
 
Kuna hoja ya Nyalandu anayodai kuhusu CCM kwa sasa kukosa dira.

Kwanza unaposema kwa sasa CCM imekosa dira wakati umekuwa ndani yake kwa kipindi kirefu inabidi utueleze, kipindi cha nyuma ilikuwa na dira gani?

Je, hiyo dira iliyokuwepo kipindi cha nyuma ilikuwa inaonekana kwenye chama alichojiunga nacho?

Hiyo dira iliyokuwepo kipindi cha nyuma ilimsaidiaje mwananchi hasa mwenye uwezo mdogo kielimu na kiuchumi?
Imekosa dira baada ya kufuta vibali vya kuwinda ambavyo vilitolewa kwa magumashi na huyo Nyalandu.
 
Nyarandu hata hivyo alikuwa amecherewa cku zte mda ndo hutoa majibu, tilitegemea kuachwa na Ccm amewahi Ku lisign. Ondoka uligawa vitaru vya loliondo kwa wamarekani wako. Achape raba
Jamaa eti anasema CCM imekosa dira/mwelekeo!

Inawezekana CCM imekosa mweleko/dira kwa mujibu wa fikra zake kwa sababu kuukosa Uwaziri ni kukosa mwelekeo na dira!
 
Bushiru Ally anaona jinsi mwenzao alivyowaacha. Sasa hana jinsi ni kujikomba tu. Wala hawezi akajibu kuwakilisha wananchi, au kuisimamia katiba hataki aonekana hana mkia. Namkumbuka Dr Juani Mwaikusa, Dr Songondo Mvungi. Mungu angekuwa ametuomba mbadala wa hawa watu, walahi mimi ningemchagu huyu!! Wewe je? Acheni uoga tililikeni tu.
 
Ukitaka kuwa critical soma na mawazo ya wengine. Hakuna lolote jipya alilofanya kwa kuhama na sio mtu wa kwanza. Alishanusa kuwa anaandaliwa vikao vya kumhoji kuhusu mwenendo na msomamo wake. Huko anakikwenda akifika aulize kilichomtoa zito kabwe ni nini. Kila chama kina misingi na taratibu zake. Ukiona hazikufai unaondoka kama alivyofanya.
Kama suala ni kuhojiwa, Nyalandu angekuwa salama zaidi kuhojiwa akiwa CCM kuliko akiwa Chadema. Kama ulimwangalia usoni Chakubanga wakati akihojiwa na ITV kuhusu kuondoka kwa Nyalandu CCM ni rahisi kuona kwamba kama ni kuhojiwa hilo litafanyika kama njia ya kumkomoa na kumfanyia visasi Nyalandu, wala hilo halikuwepo kabla hajaondoka CCM!
 
Chama Cha Mapinduzi ni genge la wezi, wala rushwa na wabadhirifu wakubwa nchi hii! Ni genge ndani msitu mnene uliojaa muumiani na monsters!!

Ndani ya genge hili hatari duniani, wanahakikisha kuna vikaragosi wao wa kutosha nje ya msitu huo wa mafedhuli! Vikaragosi hivyo vitakuwa vitapewa kwa vipipi na vibiskuti na wakati mwingine kuishia kudanganywa kwa kauli na baada ya hapo, wataingia duniani kuwatetea mafedhuli na manduli wanaoiangamiza nchi!!

Ni kweli, kwavile ni msitu mnene uliojaa majahiri wa kila aina, haishangazi wengine kujikuta wamezaliwa kwenye hilo limsitu la waovu na kujikuta wakitenda kama manduli mengine yaliyomo humo yanavyotenda!! Hata hivyo, wapo miongoni mwao ambao hatimae wanakuja kupata maono kwamba udhalimu na uovu unaofanywa na jamii yao haukubaliki, sio dunia tu bali hata akhera!

Hawa ni wale wanaoamua kuukumbia msitu huku wakirushiwa kila aina ya silaha kutoka kwa mafedhuli wao ambao hawataki kuona watu wakiungama... wanachotaka ni kuona kizazi chao cha majahiri kikiendelea kushikamana!!!
Asante kwa shairi.
 
Ni ujinga kufikiria kuwa kila kosa ni lazima litamkwe na mahakama. Kuna watu ni wajinga kiasi kwamba hata mtu akipigwa na mwenzake au hata na kiongozi wake wa kazi watasema siyo kosa mpaka mahakama itamke kuwa aliyempiga mwenzake ametenda kosa.

Mahakama zinatoa hukumu lakini kinachoeleza nini ni kosa ni katiba na sheria zetu. Mathalani mtu akifukuzwa kazi bila ya kupewa nafasi ya kujitetea/kujieleza, tunajua kuwa hilo ni kosa, hata kama aliyefanyiwa hilo kosa ataamua kutokwenda mahakamani.
Andiko lako limejikita kwenye dhana wakati sheria ni ukweli uliokubaliwa na jamii fulani.

Ukweli huo unatapata tafsiri mahakamani au kwenye chombo kilichopewa mamlaka ya kutafsiri ukweli uliokubaliwa na jamii hiyo.

Wewe ukidai nimevunja sheria kumbuka kuna mwingine atadai sijavunja hiyo sheria. Kwa mantiki hii, lazima kiwepo chombo kilichokubaliwa katika kutafsiri dhana.
 
Dr bhana eti haoni ujasiri wa Dr slaa,

Kile kitendo cha mtu kusimamia anachokiamini ninujasiri tosha,

Hatuwezi kuogopa kusimamia tunavyoviamin kwa kuogopa kupotea hizi PhD sijui wanazipataga wap

Halafu habari ya mihimili kuingilia hatuwezi kuendelea kuruhusu kisa kuna nchi nyingi tu zipo hivyo au zamani ilikuwa hivyo,

Hapa simtetei Nyalandu kwa sababu najua naye ana majanga yake ya kutosha tu ila tukitaka kujenga hoja lazima tulete maoni yenye mashiko
Nadhani hujaelewa mantiki ya Dkt. Bushiru kuhusiana na mfano wa Dkt. Slaa.

Msome vizuri ili uelewe vizuri.
 
Nyarandu hata hivyo alikuwa amecherewa cku zte mda ndo hutoa majibu, tilitegemea kuachwa na Ccm amewahi Ku lisign. Ondoka uligawa vitaru vya loliondo kwa wamarekani wako. Achape raba
Kwani aligawa kwa matakwa yake?! Si kwamba alikuwa anatekeleza ilani ya CCM na maagizo ya baraza la mawaziri chini ya JK?! Mbona sioni mkimuandama Kikwete?! Aliyeidhinisha biashara hiyo?!
 
Bashiru kama Banna, walishapoteza maana kama wachambuzi wa siasa, hoja za Nyalandu kutokuwa mpya hakuondoi umuhimu wake bali kunasisitiza umuhimu wa kuwa na mjadala wa kitaifa kuirejesha nchi yetu njia kuu. Hoja kwamba hata Marekani kuna tatizo kama hilo haina mashiko, "if you are sick and your friend is sick, does it make you feel better?!"
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom