buthabutha
JF-Expert Member
- Jan 26, 2017
- 659
- 395
Dr Slaa Ajitathimni Kurud Nchini.......Adai Upinzani Usipojipanga Unaweza Kufutika 2020 source MPEKUZI HURU
Mzee wewe ulikimbia nchini,ukaenda kula raha kwa wazungu maneno-maneno kuhusu nchi yetu? We baki na raha zako huko canada na sisi tubaki nchini kwetu tutajuana wenyewe humu humu.Kaa kimya.Hayo ni maoni ya Dr.Slaa kama yalivyoripotiwa katika gazeti la Mtanzania.
Pia kwa mujibu wa gazeti hilo,Dr.slaa sasa anafikiria kurejea nyumbani. Akizungumza na Mtanzania akiwa nchini Canada jana, Dk. Slaa alisema amemaliza masomo yake na baada ya kufanya tafakari atarejea nchini wakati wowote ''Ni kweli nimemaliza masomo yangu. Bado napima mazingira yaliyonifanya niondoke na familia yangu. Baada ya hapo tutaangalia uwezekano wa kurejea.
Alisema pamoja na kuachana na siasa za vyama atakuwa tayari kupiga kelele pale anapoona masilahi ya taifa yanaumia ''Hadi sasa sijapiga kelele kwa kuwa sijaona masilahi ya taifa yakiangamizwa , hatua mbalimbali zinazochukuliwa ni kweli zinawaumiza wasiohusika.
Ndio maana nilitumia katika makala mojawapo mtego wa panya huwakamata wanaohusika na wasiohusika. Hivyo makosa madogo mimi hayanisumbui kwa kuwa hakuna binadamu kamilifu.'' Alisema
Rais Magufuli
Akizungumzia utendaji wa Rais M agufuli alisema watu waelewe hakuna nchi hata moja ambapo kiongozi atakubalika kwa watu wote kwa asilimia 100.
Alisema wapo watu ambao masilahi yao yataguswa kwa namna moja au nyingine hivyo lazima watapiga kelele.
Kutokana na hilo amaesma Magufuli katika kundi ambalo halihitaji fedha ameyatekeleza yote kwa asilimia 99.9, ikiwa ninpamoja na uwajibikaji serikalini, kuchukua hatua dhidi ya rushwa, wizi wa mali za umma, uwindaji haramu na kudhibiti dawa za kulevya.
''Hatua zimechukuliwa zinapaswa kuwa endelevu . Kwa bahati mbaya mchwa wengine waliopenya mpaka ndani ya Ikulu na serikali na huwezi kufagia serikali nzima kwa siku moja.
Kwa jinsi ambavyo Rais hayumbiwala hayumbishwi , nina hakika atafika malengo ya kurudisha taifa kwenye misingi ya tunu za taifa ya uwazi, ukweli,uadilifu kuheshimiana na na kuthaminiana na hasa kujali utu''
Hii ndio ambayo JPM anaiita kipindi cha mpito. Tutafika tu, tunatakiwa kuwa wavumilivu na wenye uzalendo wa kweli, ana nia njema ya kufikisha taifa mahali pazuri.
Hii inahitaji kuweka pembeni masilahi yetu binafsi kama mtu mmoja mmoja, viongozi wa serikali hata wa kisiasa''
Kuhusu Upinzani
Kuhusu mwenendo huo endapo utasaidia upinzani kuingia Ikulu 2020, Dk. Slaa alisema wakija na ajenda mbadala na makini yenye kuwalenga wananchi moja kwa moja itawasaidia.
Dk. Slaa ambaye pia alipata kugombea urais kupitia Chadema mwaka 2010, alisema endapo wataendelea kurukia kauli za Rais, basi upinzani utafutika kabla ya 2020.
“Kama nilivyorejea mara kadhaa, upinzani makini utaingia Ikulu kwa ajenda mbadala. Ajenda makini yenye kuwalenga wananchi moja kwa moja katika kuwatoa kwenye kero zao mbalimbali.
“Hadi sasa ninachoona ni ‘kurukia’ kauli za JPM, lakini kauli si ajenda na hatupeani maksi kwa kuzungumzia usahihi wa lugha. Wako wanaotazama usahihi wa lugha na mahali pa kutazama usahihi huo. Kimsingi hayo ni masuala ya darasani au kwenye uandishi wa vitabu.
“Aidha kumtuhumu JPM kukiuka Katiba na sheria nayo haina tija. Wote wanaomtuhumu wanajua kuwa wakiambiwa waonyeshe kifungu mahususi alichokiuka yeye mwenyewe katika utendaji wake hawana majibu ya kuridhisha.
“Hivyo mimi sijaona mwenendo wa JPM unaosaidia kuingiza upinzani Ikulu. Isitoshe kama hawatakuja na ajenda makini na mkakati ulioandaliwa unaowatoa wananchi hapa walipo kwenda kwenye raha, upinzani unaweza kufutika kabla ya 2020,”alisema Dk. Slaa.
Chanzo:Mtanzania
Akirudi ahamie hiko chama.
Ana mawazo mgando sana Dr Slaa. Hii ni dunia mpya, wewe unadhani Sera za kwenye makaratasi hata ziwe nzuri namna gani bila kuondoa njaa na matatizo kwa wananchi watakukubali?
Dr Slaa
Kuhusu Upinzani
Kuhusu mwenendo huo endapo utasaidia upinzani kuingia Ikulu 2020, Dk. Slaa alisema wakija na ajenda mbadala na makini yenye kuwalenga wananchi moja kwa moja itawasaidia.
Dk. Slaa ambaye pia alipata kugombea urais kupitia Chadema mwaka 2010, alisema endapo wataendelea kurukia kauli za Rais, basi upinzani utafutika kabla ya 2020.
“Kama nilivyorejea mara kadhaa, upinzani makini utaingia Ikulu kwa ajenda mbadala. Ajenda makini yenye kuwalenga wananchi moja kwa moja katika kuwatoa kwenye kero zao mbalimbali.
“Hadi sasa ninachoona ni ‘kurukia’ kauli za JPM, lakini kauli si ajenda na hatupeani maksi kwa kuzungumzia usahihi wa lugha. Wako wanaotazama usahihi wa lugha na mahali pa kutazama usahihi huo. Kimsingi hayo ni masuala ya darasani au kwenye uandishi wa vitabu.
“Aidha kumtuhumu JPM kukiuka Katiba na sheria nayo haina tija. Wote wanaomtuhumu wanajua kuwa wakiambiwa waonyeshe kifungu mahususi alichokiuka yeye mwenyewe katika utendaji wake hawana majibu ya kuridhisha.
“Hivyo mimi sijaona mwenendo wa JPM unaosaidia kuingiza upinzani Ikulu. Isitoshe kama hawatakuja na ajenda makini na mkakati ulioandaliwa unaowatoa wananchi hapa walipo kwenda kwenye raha, upinzani unaweza kufutika kabla ya 2020,”alisema Dk. Slaa.
Chanzo: Mtanzania
Hizo hoteli nyingi zilijengwa kwaa kifisadi, na zilikuwa zikitegemea pesa za wananchi walalahoi, seminars za uongo na ambazo zimepangwa kifisadi fisadi, kila siku utaona Dar peke yake semira 40 hadi 60 , kitu ambacho kingefanyika katika kumbi za mikutano za wizarani. Seminar ya siku moja inafanywa kwa siku 5.
Seminar ya wafanyikazi wa mbeya inafanyika Dar ama Arusha.
Hii ndio ilikuwa inawalipa wenye hoteli, bei za vyumba vilipanda kwa sababu hiyo, chumba Dar 150000 kwa siku tena hotel ya kawaida tuu. Arusha 80, 000 hali myu wa kawaida analipa 30,000 KWA CHUMBA . Hao watu walikuwa wakupuwaji wa pesa za umma.
Atanusuru vipi?
Point of correction you miss him not weDr. We missing him badly.
Hiyo ni historia, siasa zile za Slaa sasa hivi hakuna wa kumsikiliza na haziwezj kuleta badiliko loloteHilo ni buludoza, Slaa anajua aset na liability. Mkimtaka arudi ondoeni liabiliti muone mziki wake.
Akiingia Ccm, toba!
..wala hakuna cha raha huko aliko wala nini...aliyekudanganya anakula raha nani?.....huko ng'ambo aliko wala hapati mapato kama alivyokuwa anapata TZ chini ya chedema....huko waliko na mchumba wake sana sana wanafanya kazi nje ya taaluma zao....kama kuna ufadhili na utakua unaishia sasa...na kama ni kazi wanafanya basi ujue ni za kitwana tu....mfano kuosha vyooo ama vyombo kwenye mahoteli ya wazungu....usidhani wanapokaa nje ya nchi wana raha sana....usisahau pia kuwa hata hali ya hewa sio friendly huko waliko.....sasa inaonekana ufadhili wao huko umeisha...na sasa wanatafta kiki za kurudia bongo...ni rahisi sana kuwasoma watu wanafiki na waongo....kama huyu babu...Mzee wewe ulikimbia nchini,ukaenda kula raha kwa wazungu maneno-maneno kuhusu nchi yetu? We baki na raha zako huko canada na sisi tubaki nchini kwetu tutajuana wenyewe humu humu.Kaa kimya.
binadamu wa ajabu sana! Dr siku hizi ni spika tu redio iko 'jikoni'.Kama kweli hayo ni maoni ya Dr Slaa ni dhahiri huyu mzee amezeeka vibaya hususani baada ya kumaliza pesa zote huko Canada.
Mkuu kubali Dr Slaa amekuchakaza. Gusia hoja zake na siyo personality.Akirudi na akitaka kurudisha heshima yake aache kumtumia yule "mchumba" kama mshauri wake.
Hakika nawaambia, aliyemharibia Slaa maisha yake ya kisiasa ni "mchumba"