Dk Slaa aitonesha CCM Igunga

sir.JAPHET

JF-Expert Member
May 18, 2012
699
133
Jumapili, Agosti 26, 2012 06:46

Na Abdalah Amir, Igunga



dk.%20slaa.jpg

Dk. Wilbrod Slaa

*Asema uchaguzi ukirudiwa haitashinda
*Kasulumbai amtupia kombora Magufuli

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willbrod Slaa amesema uchaguzi mdogo wa Igunga mkoani Tabora ukifanyika sasa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kisitarajie kushinda.
Dk. Slaa alitoa kauli hiyo jana mjini Igunga alipohutubia mamia ya wananchi kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine.

"Nawaambia wana Igunga, nimekuja kuwashukuru kwa kazi nzuri mlioifanya wakati wa uchaguzi mdogo wa mwaka jana, mlituonyesha imani…nawaambia CCM hata uchaguzi huu ukirudiwa sasa hivi hawashindi," alisema.

Alisema kwa sababu hiyo, Chadema kiko tayari kuingia kwenye uchaguzi wa marudio wakati wowote kwa sababu kina uhakika wa kushinda.

"Hatuna wasiwasi na hili, nawaambia Chadema wako tayari kwa uchaguzi, uamuzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora kutengeua matokeo haya tumeupokea kwa mikono miwili kabisa,"alisema Dk. Slaa.

Dk Slaa, ambaye aliogozana na Mbunge wa Maswa Mashariki, Silvester Kasulumbai, alisema CCM wanapaswa kujilaumu wenyewe kwa kuwatumia mawaziri kutoa ahadi kwa wananchi wakati wakitambua kufanya hivyo ni kosa.

Alisema makosa hayo yanazidi kuwagharimu wananchi wa Igunga kutokana na gharama kubwa zinazotumika kurudia uchaguzi.

Alisema katika uchaguzi mdogo uliompatia ubunge mgombea wa CCM, Dk. Peter Kafumu zaidi ya Sh bilioni tatu zilitumika kiasi ambacho kingefanya kazi za kuinua maendeleo ya wananchi.

"Uchaguzi ukiitishwa leo hatuna wasiwasi, tuna uhakika wa kushinda mapema saa 4 asubuhi. CCM hawana ubavu wa kupambana na Chadema, wanachofanya ni kushinda kwa ghiliba na vitisho,

"…mathalani, kauli ya Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama (eti Chadema kilikodisha makomandoo kutoka Libya na Pakstan) haiwezi kuvumilika, anapaswa kuwaomba radhi wana Igunga kwa uongo huo" alisema Dk. Slaa.

Naye Kasulumbai alizungumzia kauli ya Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli kujenga daraja la Mbutu endapo mgombea wao atachaguliwa haivumiliki.

Alisema Magufuli kama waziri, anapaswa kuwaomba radhi wananchi wa Igunga kwa sababu ujenzi wa miundombinu ni kazi ya serikali iliyoko madarakani.

"Daraja hili lilicheleweshwa kujengwa na Serikali iliyo madarakani… kwa nini waje kuwaomba muwachague eti ndiyo wajenge…namtaka Magufuli awaombe msamaha.

"…miaka yote walilifumbia macho, leo hii baada ya kuona Chadema tumejizatiti na kuwaeleza ukweli wananchi…eti ndiyo wanazinduka ujenzi wa daraja, sisi wapinzani kazi yetu ni kupiga kelele".


Toa Maoni yako kwa habari hii


 
hivi magufuli akiwa anaenda jimboni kwake chato huwa hapiti njia ya igunga? maana ni aibu mbele ya wananchi wa igunga kwa jinsi alivyo dhalilika
 
Slaa+na+Kashindye.JPG

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, akisalimiana na aliyekuwa mgombea wa ubunge jimbo la Igunga katika uchaguzi mdogo mwaka jana, kupitia Chadema, Mwalimu Joseph Kashindye, walipokutana katika mkutano wa kuwashukuru wananchi wa jimbo hilo kwa ushiriki wao katika kesi ya uchaguzi wa jimbo hilo, ambayo Chadema kiliibuka mshindi, uliofanytika kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Igunga


Dk+Slaa+na+Kasulumbai.JPG

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa akikumbatinana na Mbunge wa Maswa Mashariki, Slyvester Kasulumbai, walipokutana katika mkutano wa hadhara wa kuwashukuru wananchi wa jimbo la Igunga kwa ushiriki wao katika kesi ya uchaguzi wa jimbo hilo, kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Igunga juzi.

Picha+ya+mbele.jpg

Aliyekuwa mgombea wa jimbo la Igunga katika uchaguzi mdogo mwaka jana, kupitia Chadema, mwalimu Joseph Kashindye na aliyekuwa meneja wa kampeni, Slyvester Kasulumbai, wakiwasili kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini Igunga, ambako kulifanyika mkutano wa hadhara.Picha zote na Joseph Senga)


Picha zote source: www.hakingowi.com
 
Nampa hesima sn mzee Slaa.
Ni m'baba mwenye uvumilivu sana na ana upendo wa kweli. Kitendo cha kutumia muda wake wote kuzunguka kujenga chama si maamuzi madogo.

Mbegu anayoipanda huko thamani yake ni kubwa sn kwa ustawi wa Taifa letu, hata km si leo basi ni baadaye. Wa kusema watasema kuwa ni ishu ya posho, lakini wenye akili zetu tunaona ng'ambo ya uzio wa posho.

Tunaziona akili za watu zikifunguka na kubadilikaMungu mbariki Baba huyu.
 
Nampa hesima sn mzee Slaa.
Ni m'baba mwenye uvumilivu sana na ana upendo wa kweli. Kitendo cha kutumia muda wake wote kuzunguka kujenga chama si maamuzi madogo.

Mbegu anayoipanda huko thamani yake ni kubwa sn kwa ustawi wa Taifa letu, hata km si leo basi ni baadaye. Wa kusema watasema kuwa ni ishu ya posho, lakini wenye akili zetu tunaona ng'ambo ya uzio wa posho.

Tunaziona akili za watu zikifunguka na kubadilikaMungu mbariki Baba huyu.

usisahau kuwa anatengeneza mshiko vilevile (posho za safari)
 
Back
Top Bottom