Dk Mwakyembe arejea nchini

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,082
NAIBU Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe, amerejea nchini akitokea Hospitali ya Apollo nchini India alikolazwa kwa ajili ya matibabu ya ugonjwa wa ngozi. Dk Mwakymbe aliondoka nchini Oktoba 9 mwaka huu kwenda nchini India baada ya hali yake ya afya kuzorota huku ngozi yake ikionekana kudhoofika.

Baada ya kukaa India kwa takriban miezi miwili, jana saa 7:00 mchana, Dk Mwakyembe aliwasili nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere kwa ndege ya Shirika la Qatar Airways.

Habari zilizolifikia gazeti hili jana mchana zilieleza kuwa baada ya kutua jijini Dar es Salaam, Dk Mwakyembe aliondoka moja kwa moja kuelekea mkoani Mbeya. Akizungumza na gazeti hili jijini Dar es Salaam jana, Msemaji wa Familia na Mbunge wa Lupa, Victor Mwambalaswa alisema, afya ya mbunge huyo wa Kyela, ni nzuri ndio maana ameruhusiwa kutoka hospitali.

“Ni kweli Dk Mwakyembe amerejea nchini salama .Tunamshukuru Mungu, hii inatokana na madaktari waliokuwa wakimpatia matibabu kumpa ruhusa baada ya kuona hali yake ni nzuri na kwamba anaweza kuendelea na majukumu yake kama kawaida,” alifafanua Mwambalaswa na kuongeza:

“Kutokana na hali hiyo, tunaamini kuwa, kurudi kwake nchini, kutaleta matumaini mapya ya afya yake.” Msemaji huyo wa familia alisema, baada ya kurudi, Dk Mwakyembe atapumzika kijijini kwao Kyela ili aweze kujumuika na wanafamilia katika kipindi hiki cha Sikukuu ya Chrismasi na mwaka mpya, kabla ya kuanza kazi rasmi ya ujenzi wa taifa mwakani.

::Mwananchi::
 
lihimidiwe jina la yesu....god is good all the time. welcome home comrade....
 
Dk Mwakyembe arejea nchini Send to a friend
Monday, 12 December 2011 20:42
0digg

dk-mwakyembe-hoi.jpg
Naibu Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe

Patricia Kimelemeta
NAIBU Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe, amerejea nchini akitokea Hospitali ya Apollo nchini India alikolazwa kwa ajili ya matibabu ya ugonjwa wa ngozi. Dk Mwakymbe aliondoka nchini Oktoba 9 mwaka huu kwenda nchini India baada ya hali yake ya afya kuzorota huku ngozi yake ikionekana kudhoofika.

Baada ya kukaa India kwa takriban miezi miwili, jana saa 7:00 mchana, Dk Mwakyembe aliwasili nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere kwa ndege ya Shirika la Qatar Airways.

Habari zilizolifikia gazeti hili jana mchana zilieleza kuwa baada ya kutua jijini Dar es Salaam, Dk Mwakyembe aliondoka moja kwa moja kuelekea mkoani Mbeya. Akizungumza na gazeti hili jijini Dar es Salaam jana, Msemaji wa Familia na Mbunge wa Lupa, Victor Mwambalaswa alisema, afya ya mbunge huyo wa Kyela, ni nzuri ndio maana ameruhusiwa kutoka hospitali.

“Ni kweli Dk Mwakyembe amerejea nchini salama .Tunamshukuru Mungu, hii inatokana na madaktari waliokuwa wakimpatia matibabu kumpa ruhusa baada ya kuona hali yake ni nzuri na kwamba anaweza kuendelea na majukumu yake kama kawaida,” alifafanua Mwambalaswa na kuongeza:

“Kutokana na hali hiyo, tunaamini kuwa, kurudi kwake nchini, kutaleta matumaini mapya ya afya yake.” Msemaji huyo wa familia alisema, baada ya kurudi, Dk Mwakyembe atapumzika kijijini kwao Kyela ili aweze kujumuika na wanafamilia katika kipindi hiki cha Sikukuu ya Chrismasi na mwaka mpya, kabla ya kuanza kazi rasmi ya ujenzi wa taifa mwakani.

Alisema, kutokana na hali hiyo anaamini, sala za wananchi ni miongoni mwa mambo yaliyofanya apone haraka na kurudi nyumbani Kuugua
Taarifa za kuugua kwa Dk Mwakyembe zilianza kuvuma mwanzoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu baada ya kuanza kupata matibabu nchini.

Hata hivyo, kutokana na afya yake kuendelea kuzorota, Serikali ililazimika kumkimbiza nchini India kwa ajili ya matibabu zaidi.

Taarifa za awali, zilisema Dk Mwakyembe alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari ambapo alikuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Lakini, taarifa hizo za ugonjwa wa kisukari zilipingwa na baadhi ya washirika wake wa karibu kisiasa, ambao waliamini Naibu waziri huyo, alilishwa sumu iliyosababisha nywele zake kunyonyoka, ngozi ya mwili wake kupepetuka na kutoa unga, huku akiwa amevimba. Hata hivyio ilielezwa kuwa, madaktari nchini India ndio pekee ambao wangeweza kuangalia namna ya kumsaidia katika ugonjwa huo.
 
Pole baba. Hongera kwa kuwa vita hii nadhani imechochea shauku yako ya kupigana na mafisadi. Tuko nyuma yako kamanda.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Pole baba. Hongera kwa kuwa vita hii nadhani imechochea shauku yako ya kupigana na mafisadi. Tuko nyuma yako kamanda.

....Ngoja tusubiri kama ataamua kuyaongelea yaliyomsibu hadi ikabidi kwenda kutibiwa India.
 
Pole sana na karibu nyumbani ,ila watanzania wanasubiri sana kujua nini kilikusibu na itasaidia sana kujua ukweli na uzushi.
 
Karibu nyumbani Mpiganaji na ukapate japo mapunziko kidogo nyumbani kabla hatujasikia moja kwa moja toka kwako juu ya Pollonium na mwenendo wake mzima mwilini mwako.

Maombi yetu kwako na Prof Mwandosya kila uchao.
 
kwa magazeti ya udaku title ya habari hii ingekuwa "kambi ya sitta yaimarishwa,lowassa aanza kuufyata"
 
Karibu nyumbani mheshimiwa. Ni muda muafaka wa kueleza watanzania mambo yooote bila kuficha ficha na kuweka viporo.
 
wabongo our line of thinking is becoming questionable ila tunashukuru mwakiembe karudi salama
Swali je kabla ya ccm kudaka agenda ya cdm ya kupinga ufisadi ina maana viongozi hakuwa wanaugua kama ilivyo kawaida kwa binadamu kuugua?
 
Na orodha hii ya Mbeya inaendeleaje?, Hilda Ngoye (Mb) na mkiti wa CCM wa mkoa wa mbeya?, lakini Mbeya mjiangalie!
 
Hivi ile ripoti ya chanzo cha matatizo yake naweza ipata wapi mana nimeitafuta humu jf sikufanikiwa,mwenye nayo anipatie wadau! Karibu kamanda Mwak
 
Back
Top Bottom