Ngandema Bwila
JF-Expert Member
- Sep 8, 2010
- 1,017
- 256
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)kimesema Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepoteza mwelekeo na sasalinaonekana kama kituko kutokana na viongozi wake "kuwabeba" wabungewa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuwabana wapinzani katika mijadala mbalimbalibungeni.
Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC,Dk. Hellen Kijo-Bisimba, katika tamko lililosomwa kwa niaba yake na WakiliImelda Urio kutoka kituo hicho.
Dk. Bisimba alisema kwa sasa hakuna uwiano katika mijadala ya bajetiinayoendelea ndani ya Bunge mjini Dodoma kwa kuwa viongozi wanaowaogoza wabungewameonekana wazi kufanya upendeleo kwa wabunge wa CCM.
Aliwataja viongozi hao kuwa Spika wa Bunge na Naibu wake pamoja na wenyevitiambao wamepewa dhamana ya kuongoza vikao.
Aliwataka viongozi hao kubadili mitizamo yao ili kutoa fursa kwa wabungekujadali kwa uwazi hoja kwa faida ya wananchi badala ya maslahi ya vyama vyao.
Tunawataka wabunge watekeleze majukumu yao ipasavyo na kulirudishia heshimaBunge la 10 kama lilivyokuwa Bunge la Tisa, Bunge la sasa limepoteza mwelekeona kuonekana kama kituko mbele ya jamii inayowaangalia, alisema katika tamkohilo.
Aidha, LHRC kimewataka wabunge kuachana na utaratibu wa kutumia muda mwingikutoa salaam pamoja na pole kwa kuwa jambo hilo ni kinyume cha kanuni namba151(1)-(4).
Dk. Bisimba alisema kama kuna jambo la kutakiwa kutoa pole ama pongezi, Spikaanaweza kufanya hivyo kwa niaba ya wabunge badala ya mbunge mmoja mmoja kufanyahivyo kiasi cha kutumia muda mwingi ambao angeutumia kutoa mchango wake katikamijadala.
Kasoro zingine zilizoainishwa katika tamko hilo la LHRC ni pamoja na wabungekuendelea kutumia lugha za kuudhi, kuzomeana na kutaka miongozo bila sababu zamsingi kinyume cha kanuni namba 64 (1) (g).
Bado tunaona lugha za matusi na za kuudhi zikiendelea kutolewa na wabungekatika vikao vya Bunge vinavyoendelea mjini Dodoma na hili jambo linatakiwakukomeshwa, alisema.
Aidha, Dk. Bisimba alisema mahudhurio ya wabunge katika vikao vinavyoendeleabungeni ni hafifu na kwamba jambo hilo ni kinyume cha kanuni namba 143(1), nakwamba mara nyingi viti vimeonekana kuwa vitupu bila watu.
Jumatatu na Jumanne wiki hii hali ya hewa bungeni ilichafuka baada yaMwenyekiti Sylvester Mabumba, kuonekana dhahiri akiyumba kwenye kiti wakati wakikao cha Jumatatu jioni hali iliyozua msuguano mkali na baadhi ya wabunge.
Hali kama hiyo nusura itokee tena Jumanne katika kipindi cha baada ya maswalihadi mchana wakati wa mjadala wa makadirio ya Ofisi ya Makamu wa Rais.
May take: Mama Makinda ni zaidi ya Kichuguu dhidi ya Kilimanjaro katika kuongoza Bunge. CCM ijifunze kuwapa nafasi watu wenye UWEZO badala ya vilaza wenye mtizamo wa kichama dhidi ya maslahi mapana ya Taifa.