Diwani anaruhusiwa kuendelea na ajira ya serikali?

Mzee wa Juu kwa Juu,

Unabwaga bonge la point halafu unakimbia. Kaa humu humu usaidie kujibu. Ndiyo maana mimi nimeng'ang'ana na kuwauliza kuhusu Shyrose Bhanji ambaye ni muwakilishi kwenye Bunge la Afrika Mashariki.

Kama ulivyosema uwakilishi si ajira. Uwakilishi ni kutuwakilisha kwenye vikao amvayo hatuwezi kwenda nchi nzima au kata nzima au kijiji kizima. Vikao vikiisha wewe muwakilishi kama ni mbunge njoo utuambie majibu uliyopewa tulipokutuma utuwakilishe. Basi.

Uwakilishi si ajira, iwe ni udiwani, ubunge, au hata uwakilishi wa mkutano wa kijiji, mkutano wa mtaa, mkutano wa chama cha siasa.

Ninakubaliana na dhana ya kuwa wote wawili yaani diwani na mbunge ni wawakilishi wa umma lakini si watumishi wa umma kwa maana ya sheria ya utumishi wa umma ya mwaka 2002 na kanuni zake za 2003 na pia ninakubaliana kuwa Udiwani si ajira kwa kuzingatia ibara YA 24 Inayotamka juu ya haki ya mtu kulipwa kutokana na kazi anayofanya, kwa maana ya kulipwa stahili inayofanana na kazi kinyume chake diwani pia sheria ama kanuni na maadili ya diwani yanabainisha kuwa diwani ni mtu anayechaguliwa na wananchi ktk eneo lake kwa namna tu ya umaarufu wake na kwa imani kuwa ana uwezo fulani.
 
Kwa mujibu wa katiba mtu anapopata majukumu ya kisiasa anatakiwa aache utumishi wa uma mara moja.leta majina

Mchangiaji mmoja amewataja madiwani wa Morogoro mjini ambao bado wanalipwa mshahara na SUA.
Ni kweli tena nimeambiwa wapo watatu, wote ni waajiliwa wa SUA (taasisi ya serikali)
 
Mzee wa Juu kwa Juu,

Unabwaga bonge la point halafu unakimbia. Kaa humu humu usaidie kujibu. Ndiyo maana mimi nimeng'ang'ana na kuwauliza kuhusu Shyrose Bhanji ambaye ni muwakilishi kwenye Bunge la Afrika Mashariki.

Kama ulivyosema uwakilishi si ajira. Uwakilishi ni kutuwakilisha kwenye vikao amvayo hatuwezi kwenda nchi nzima au kata nzima au kijiji kizima. Vikao vikiisha wewe muwakilishi kama ni mbunge njoo utuambie majibu uliyopewa tulipokutuma utuwakilishe. Basi.

Uwakilishi si ajira, iwe ni udiwani, ubunge, au hata uwakilishi wa mkutano wa kijiji, mkutano wa mtaa, mkutano wa chama cha siasa.

Mdau Nikupateje kwamba uwakilishi si ajira hivyo unahitaji uwe na shughuli zingine za kukuingizia kipato na kama ni mtumishi wa umma unaacha au unachukua likizo ya bila malipo ya miaka kadhaa (sina uhakika na hili), tatizo hawa wawakilishi wetu wanatuchakachua na kufanya tuamini kwamba wao ndio kila kitu na ndio maana utawasikia katika kipindi chake ameleta barabara, maji, umeme wakati mpaka huo umeme umekuja kulikuwa na process kibao ambayo ili-involve watu mbambali ikiwemo (wawakilishwa) ambao katika vipaumbele vyao waliainisha hayo matatizo na mbunge kufikisha huko lakini badala ya kuja ku-acknoledge contribution za watu wengine na kurudisha feedback wanakuja tambo kibao.
 
Last edited by a moderator:
Hairuhusiwi hata chembe! Tunaomba mifano ku-support madai haya mazito.

Ni kama nilivyoandika hapo juu kwamba mwana JF katoa mfano wa madiwani watatu wa Morogoro Mjini mabao pia ni waajiliwa wa SUA na bado wako ofisini SUA.

Hii inaweza kuwa ni kinyume sawa na watendaji wakuu wa serikali na hata askari wasioruhusiwa kuwa ktk siasa lakini ghafla mtu anaibuka na kugombea ubunge kumbe alikuwa na kadi ya CCM siku nyingi akiwa ktk nafasi inayomtaka asiwe mwanasiasa.

Ndo akina kafumu hao!
 
Back
Top Bottom