benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,504
- 3,034
Baada ya kukwama mara ya kwanza hatimaye Mfanyabisahara maarufu nchini Tanzania, Rostam Aziz anatarajia kuanza rasmi utekelezaji wa mradi wake wa gesi nchini Kenya huku akisifia mazingira bora ya uwekezaji katika nchi hiyo.
Rostam kupitia kampuni yake ya Taifa Gas ameruhusiwa kutekeleza mradi wake ambao unatajwa kuwa na thamani ya Dola za kimarekani 130 milioni (Sh304 bilioni) hali itakayomfanya kuwa kampuni kubwa zaidi ya gesi katika nchi hiyo namba moja kiuchumi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Katika mradi huo Taifa Gas itajenga mtambo wa tani 30,000 katika eneo maalumu la uwekezaji Dongo Kundu jirani na Bandari ya Mombasa, hivyo kuongeza ushindani kwa kampuni za Vivo, Rubis na Total pamoja na Africa Gas and Oil Limited (AGOL) zinazosambaza nishati hiyo nchini humo.
Taarifa ya iliyotolewa na taifa gesi leo Alhamisi Februari 23, 2022 imeeleza uzinduzi rasmi wa mradi huo wa mabilioni ya Shilingi utafanyika Jumapili, Februari 26 mwaka huu na utaongozwa na Rais William Ruto.
Ikumbukwe Rostam Aziz ni miongoni mwa Wafanyabiashara walioongozana na Mhe Rais Samia Suluhu katika ziara yake nchini Kenya ambapo Mei 5, 2021 katika kongamano la wafanyabiashara wa Tanzania na Kenya alizungumzia changamoto anazokutana nazo katika jitihada za kuwekeza nchini Kenya ambapo mamlaka husika ziliahidi kufanyia kazi changamoto hizo
Chanzo: Mwananchi