Diouf wa Twanga kortini kwa unyang'anyi

Ibrah

JF-Expert Member
Mar 22, 2007
2,729
528
Diouf wa Twanga kortini kwa unyang'anyi


Rehema Maigala

MWANAMUZIKI wa bendi ya Afican Stars (Twanga Pepeta), Msafiri Saidi Diouf (30), mkazi wa Gongo la Mboto amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kujibu mashitaka ya kuiba kwa kutumia nguvu.

Mshitakiwa huyo aliongezwa jana katika Mahakama ya Kinondoni baada ya mpelelezi wa polisi kugundua kuwa Diouf pia ni mshitakiwa katika kesi ya unyang'anyi wa kutumia nguvu.

Awali kesi hiyo ilisomwa Oktoba 16, mwaka huu, ambapo washitakiwa wawili Mbaraka Muba (30) na Yahaya Mkabati walisimamishwa kizimbani na kusomewa mashitaka yao.

Kesi hiyo ipo mbele ya Hakimu Stahimili Ngwaisya na kusomwa na Mwendesha Mashitaka Inspekta wa Polisi, Nassoro Sisiwaya ambaye alidai Oktoba mwaka huu, washitakiwa wote kwa pamoja walimnyang'anya mlalamikaji Abdul Selemani fedha taslimu Sh. 300,000 .

Washitakiwa wote kwa pamoja walikana mashitaka hayo na wamerudishwa rumande hadi kesi hiyo itakapotajwa tena Novemba 11 mwaka huu.

SOURCE: Majira 28 Okt. 2008
 
Vijana wenzangu dawa za kulevya zinaharibu maisha.....ni ushauri tu.
 
Tena kama huyo Diof yaelekea mwisho wake utakuwa mbaya sana amezidi anaendekeza sana hayo maunga!!! Kama ikithibitika wamekwiba kweli let them go behind bars!!!
 
Back
Top Bottom