Diamond Platinum....Hata kama imevuja..ila taaamu

mkweli wa mambo

JF-Expert Member
Oct 28, 2013
329
178
yeeees..ni yuleyule tena mkali wa wakali, sukari ya warembo hasa masuperstar wetu wa kike,yule anayejiita raisi wa wasafi, yuleyule ambae ana make headline kila koona ya Tz na Africa kwa ujumla..Platinuuuuuum...ebhana jamaa anajua,sio kwamba tu namsifia la hasha..nimepata kusikiliza nyimbo yake mpya hii iliyovuja sijui inaitwa nini vileee sijui kitorondo..mwanzoni nilipoona title ya kitorondo nikadharau ndo madudu gani ayo tena jamaa anaimba,ila daah namsifu mchizi anajua kusoma nyakati,anajua ni aina gani ya muziki autoe utakaoendana na nyakati zilizopo, kama mtakumbuka kuna kipindi kwaito zilitamba sana,mchizi akatupia nyimbo zake za style iyo akakomba mashabiki kibaaao..saivi kwaito inaishia ivo mchizi kasoma nyakati tena akaibuka na mtindo huu sijui ni mnanda sijui mchiriku mi sielewi, ila all in all nyimbo taamu balaa, nyimbo inachezeka..tena kalenga haswaaaa kuleeee kwa watoto wa uswazi kule kwenye vigodoro ambavyo kila mtu anafahamu siku izi vigodoro ndo mpango mzima. Daaah,kwa style hii Diamond atakaa sana kwenye peak ya game hili..wasanii wengine mjifunze kutoka kwake,someni nyakati.
 
  • Thanks
Reactions: ehm
Kheeee!!ama kweli na nyie mtakuwa vitorondo..hv wimbo ukifanana title maana yake amekopy eeeh...!!
 
KWELI KIJANA HUYU NAMUAMINIA. Wakosaji ndio maneno yao hao.Nimezisikiliza nyimbo HIZI zenye jina la kufanana Kitorondo ya Nurdin ft Alsay na Diamond Platinum.Kweli zina mahadhi ya kufanana NA ZIMEPIGWA katika mtindo wa Kigodoro.

Sijui aliyepiga muziki wake kwa mtindo wa Kwasakwasa, Hip Hop,Rn B,Rumba. Zuku,Chacha,Mchiriku na kadhalika nanai hapo atakuwa kamwiga mwingine.Hii ni mitindo tu.Yeyote aweza kupiga mziki wake kwa mtindo autakao.Upekee wa ubunifu uko zaidi katka ujumba na maudhui.

Sasa sikiliza kazi hizi na wewe uamue.:smiling:
1.Nurdin feat Alsay-https://www.youtube.com/watch?v=qJtiA6IGnxc
2.Diamond Platinum-diamond platnumz KITORONDO - YouTube
 
Kiukweli jamaa anajua sn! Pia anajituma sn kwa kutambua soko linahitaji nn na katika wakati upi! Big up bro!

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom