Diamond LIVE @ Dar Live Mbagala - Hii ni sahihi kweli?

Exkot sawa na ving'ora je? Haya ya nini kuwachomesha mahindi watu kwenye foleni? Kama ana hela aweke plate number private kama kina nwanko kanu,ushawah ona superstar mwenye hela anatembelea opa? Hata bob jr anamshinda kwa gari zuri kutwa kujisifia oh nimeingiza m 100 pale mcity,diamond unajiaibisha uza opa nunua hata jaguar xtype.
 
Wadau nilikuwa nikitokea kwenye harakati zangu binafsi nikirejea kwangu,muda niliokuwa napita Mbagala maeneo ya Dar Live ni muda ambao Helicopter iliyokuwa imemchukua Super Star wenu Diamond ilikuwa ikirandaranda hewani,nikiwa bado nasota kwenye foleni Super Star wenu akashushwa dizaini akaingizwa kwenye Benz nyeusi ikisindikizwa na Deffender 2 za Polisi,1 mbele ikimsafishia njia kwa king'ora,katikati BENZ iliyombeba yeye na nyuma Deffender nyingine ile inayobebaga Polisi wale wa kusimama huku Polisi wengine kibao wakiwa njiani mpk nikashawishika kuamini pengine "Baba Mwanaasha" labda alikuwa akijiandaa kupita,kumbe Diamond....sasa hebu mnisaidie kunielewesha hivi ni sahihi kwa Jeshi letu kutumia resources zake kwaajili ya issue za "Nimpende nani" kweli?

Nawasilisha.

Mweshimiwa naona kuna haja ya kujua ana kadi gani ya chama
 
Mbona hata kamanda 'KOVU' aliupigia saluti mwili wa marehemu 'KAYUMBA'? au mmeshasahau? sasa kama bosi wako anafanya hivyo kwanini nao wasimuenzi?

Kwa hiyo ile saluti ya Kova nayo ililipiwa!
 
Polisi wanaingilia kati issue kama hizi kwa maslahi ya Raia jamani, Tusielewe vibaya! Wamepima, wameona hapo issue ingeachwa iende kivyake, basi taharuki ingetokea, na hata maafa yangetokea, kwani huyo jamaa kama ulivyosema ni super star wetu, Hivyo huo msongamano uliokkuwa hapo ukimsubiri maana yake purukushani na mkanyagano usingekuwa wa kawaida. Refer Mazishi ya kanumba! Tatizo letu wa Bongo tumezoea kulaumu.... Kwa mfano polisi wasingekuwepo, na madhara yangetokea, basi tungejitokeza tena kulaumu kwamba polisi walikuwa wapi??

Thats true tusiwe wepesi wa kulaumu kila kitu bila kutathmini mazingira yaliyopelekea hilo kufanyika hivyo. ni swala la usalama wa raia tu ,hata wewe kama unashughuli yako ya kijamii inawatu wengi waeza omba ulinzi tu.
 
Mbona wacheza mpira wanapoenda mechi uwanja wa taifa wanapewa escort na hamsemi? Hata wewe ukitaka escort kwenda ofisini kama kuna umuhimu wa escort nenda kaombe wakupe defender iku-rush fasta.
 
watanzania hawakosi neno hata siku moja yani.. we hiyo opa unayo au ndo daladala daily acha ujinga wewe mwenzako kapenda hilo gari kama unaona halimfai mnunulie H4 au range kwanza anavyozisaka hela huwa unamsaidia au ndo unataka kumsaidia kwenye matumizi jasho lake acha atumie apendavyo... kwanza inavoonekana ulienda kumshangaa huko mbagala ili uje utuletee upuuzi wako hapa
 
kwa swala kama hilo hakuna shida-maana ni moja ya kazi za polisi-
ni swala la kulipa hela wanayotaka na kukamilisha utaratibu mwingine then hakuna tatizo tena-mbona mamtoni mambo kama haya kwa mastaa wao ni mambo ya kawaida sana
 
Na wewe umesema kweli kabisa, na upinzani ndio upo njiani kuuon'goa udini wakisaidiwa na wanasiasa waliotokea makanisani? na wafadhili wakuu CDU ya ujerumani au sio?

Duh! Dini Mpaka Dar Live? Kweli waTz kuna mambo!!
 
Thats true tusiwe wepesi wa kulaumu kila kitu bila kutathmini mazingira yaliyopelekea hilo kufanyika hivyo. ni swala la usalama wa raia tu ,hata wewe kama unashughuli yako ya kijamii inawatu wengi waeza omba ulinzi tu.

sawa sawa!!
 
kwa kipindi hiki diamond tumuache kama alivyo!nathubutu kusema kwa bongo hamnaga kama diamond!
 
hawana haya arumeru watu wanahitaji ulinzi wait wanajazana kwenye bongo flava pambafu kabisa haya
Ila simu ya nyani muda miti yote .... ili wote waamini kuwa serikal ya baba mwanasha imechoka kuwaza lazima hayo yatokee
 
Wadau nilikuwa nikitokea kwenye harakati zangu binafsi nikirejea kwangu,muda niliokuwa napita Mbagala maeneo ya Dar Live ni muda ambao Helicopter iliyokuwa imemchukua Super Star wenu Diamond ilikuwa ikirandaranda hewani,nikiwa bado nasota kwenye foleni Super Star wenu akashushwa dizaini akaingizwa kwenye Benz nyeusi ikisindikizwa na Deffender 2 za Polisi,1 mbele ikimsafishia njia kwa king'ora,katikati BENZ iliyombeba yeye na nyuma Deffender nyingine ile inayobebaga Polisi wale wa kusimama huku Polisi wengine kibao wakiwa njiani mpk nikashawishika kuamini pengine "Baba Mwanaasha" labda alikuwa akijiandaa kupita,kumbe Diamond....sasa hebu mnisaidie kunielewesha hivi ni sahihi kwa Jeshi letu kutumia resources zake kwaajili ya issue za "Nimpende nani" kweli?

Nawasilisha.

Ndugu ukitaka ulinzi wa polisi kama unakitu muhimu unalipia,hakuna bure hapo,isitoshe wanarinda usalama si unajua nyomi la dar live! na wote waendao hapo hawafanani! ndio maana wanalipa polisi kufanya ulinzi.
 
Back
Top Bottom