bucca
JF-Expert Member
- Oct 24, 2013
- 540
- 84
Kwani bungeni hakuna sero?
Hakuna mkuu.
Kwani bungeni hakuna sero?
Mh. Lema wakati wa kampeni zako 2010 mimi ni miongoni mwa waliokuunga mkono sana haswa kutokana na slogan zako mf. " wao wana pesa sisi tuna Mungu tutashinda", pia ahadi yako ya kujenga stand mbili kubwa nje ya mji (moja njia ya kutokea usa kabla ya kufika mjini na nyingine njia ya kutokea kisongo-ahadi uliitoa kwenye mkutano pale sanawari kwenye kale ka eneo wanako park tax. Ni katika siku hiyo pia ulisema serikali ya ccm inashindwa akili na mmiliki wa naura springs hotel kwa kuweka mt. meru hospital mahali ambapo palipaswa kuwekwa kitega uchumi na kuahidi kuindoa pale na kujenga hospital ya kisasa mahali pengine ili pale pajengwe kitega uchumi) kupitia ahadi zako hizi wadau wa mji wa arusha tuliona fikra mpya zenye kuleta mabadiliko ya kiuchumi na kijamii kwa kuboresha na ku locate kwa usahii miundo mbinu muhimu. Nilikupigia kampeni kwa watu wa karibu kwangu na kuhakikisha wanakuwa mabalozi wa kueneza kampeni yako kwa kila mpiga kura. Bahati mbaya sana hakuna hata moja kati ya ahadi hizi uliyotekeleza au hata kuisemea kimkakati wa utekelezaji baada ya kupata nafasi ya ubunge. kwa hili una deni kwa waliokuchagua au kukuunga mkono kwa moja kati ya ahadi hizi au zote kwa pamoja.
Kwenye bunge la katiba pia hujaonyesha umahiri wa kusababisha niamini kwamba ccm imekuwa kikwazo kwa hoja yako yoyote. pili umekuwa na mahudhurio hafifu kwenye vikao vya bunge hili muhimu (haswa siku za mwanzoni na kama sikosei wewe ni miongoni mwa wajumbe ambao hawakuapishwa/ kuapa kwa wakati sahii hivyo kulazimisha kutumika kwa muda mwingine kuapa badala ya utekelezwaji wa shughuli za bunge. Kutokana na haya yote siungi mkono hatua yako na ninakushauri tulia bungeni toa hoja za msingi na kama zikikwamishwa kwa mizengwe wananchi tutaona na tutaunga mkono hatua yako ila kwa sasa ustahili kuchukua hatua hiyo.
bora uondoke tu . hakuna kitu chochote ulichochangia cha maana.. bunge limekuzidi akili... lakini siamini....hivi kweli utaachia posho ya laki tatu hivi hivi tu.? labda sio lema ninaemjua mimi....!
Ondoka tu lema wala hakuna shida.Wewe ondoka tu! usafiri si unao!?Watakaobaki wataendeleza shughuli hiyo muhimu kwa mustakabali wa taifa letu.
Kama ulienda dodoma ukitegemea kwamba CCM Itakuwa inakubeba kama mtoto badala ya kutumia hoja kushawishi, basi wewe ondoka tu kaka!? Nchi hii ni ya kidemokrasia ndugu yangu.
bora uondoke tu . hakuna kitu chochote ulichochangia cha maana.. bunge limekuzidi akili... lakini siamini....hivi kweli utaachia posho ya laki tatu hivi hivi tu.? labda sio lema ninaemjua mimi....!
Katika wajumbe wote waliokuwapo pale mjengoni ni Lema pekee alielewa kioja cha upigaji kura wa jana.
Kimsingi kamati iliwasilisha mapendekezo ya namna ya upigaji kura...na kabla wajumbe hawajaridhia namna hiyo ya upigaji kura tukajionea inaanza kutumika!sielewi kilichokuwa kinapigiwa kura ni kipi ilihali kimantiki wajumbe walikubali probably through maridhiano.Ni heri ingetumika kura ya kuhoji kwa ujumla au kura ya siri au kura ya wazi....yaani ni ujuha kalulu wa aina yake...ONLY LEMA NDIYE ALIYELIONA HILO!
I support you,rudi nyumbani kwani kuna mengi ya kufanya kuliko unafiki,vioja na uharibifu wa fedha unaoendelea hapo dodoma
Hakuna mwananchi mwenye akili timamu anayemuhitaji Lema kwenye Bunge la Katiba.
munene umeamua kuziacha laki 300 per day?.
Huyu kama ni mume wangu nnampa talaka hukohuko aliko. Aibu kubwa sana mwanamme anaejiita mpambanaji kukata tamaa. Khaa! Mwanamme mzima hata haoni haya kuongea namna hiyo? chadema poleni sana na watu wa Arusha, huyo ndiye "mpambanaji" mliyemchaguwa!
Bora angejiita mpambaji.
Sasa naamini zile picha zilikuwa ni za kweli.