Dereva Wa Nape kugombea Uenyekiti Wa CCM Mwanza

Kibanga Ampiga Mkoloni

JF-Expert Member
Aug 9, 2007
18,697
8,843
1.jpg
 
ADAM%2BSOUD.jpg


Nape dereva wake anaelekea kumkimbia na kutaka nafasi ya uongozi baada ya kuamua kugombea uenyekiti Mwanza.

 
1.jpg


Ujumbe wake ndio huu hapa kuhakikisha uamuzi wake wa kugombea nafasi ya uongozi wa chama badala ya kuwa msindikizaji wa wakubwa tu. Msindikizaji ni mshahara wake wa mwezi tu wakati anaowasindikiza licha ya mshahara wana malupulupu yasokifani.
 
Kwa hiyo unamshitaki hapa Jf ili tumzuie? Mwaka huu mtajibeba! By the way ni haki yake kuchagua na kuchaguliwa! Au huko kwenu madereva hawaruhusiwi?
 
nampa heko na kumtia shime. umaskini si deni bali ni mtaji. chochote utakachodhamiria kitatimia. songa mbele utashinda
 
Aisee babaangu hapo cha ajabu nini??? Mwache agombee ili chama kizidi kuporomoka

ngoja nijiliwaze na mbege
 
Amechoka kusindikiza vilaza kila kukicha na akijipima anaona kabisa ana uwezo hata zaidi ya anaowasafirisha kila siku kwenye uwezo na fikra za kujadili na kuamua mambo!pia ana haki kikatiba!mpeni nafasi akagombee na kusikilizwa wanachana wao ndio wataamua kumpa ama la!
 
Kabla ya kuwa dereva wa NAPE alikuwa anamwendesha nani? Atakuwa amejifunza kuwa;
1. wanachoongea viongozi wake sicho wanachokitenda.
2. amegundua ulaji na yeye anataka akazitafune.

Hii ya pili ndio naiona ina uzito zaidi. Kila la kheri atimize ndoto zake, malengo ni muhimu kuyafikia.
 
kesho pia house girl wake nae atamkimbia ataenda kugombea viti maalum na atapewa,watu makini wameisha wote,unategemea watamsimamisha nani sasa
 
Katika CV Ongeza pia leseni yako class C, cheti cha veta na cheti cha NIT mabibo. kwa viwango vya ccm ya leo inatosha sana.
 
Nepi hivi yule house girl na kimanda wako wao lina wanachukua form? magamba bhana!
 
nampa heko na kumtia shime. umaskini si deni bali ni mtaji. chochote utakachodhamiria kitatimia. songa mbele utashinda

Kaza buti baba udereva ni kazi kama kazi nyingine hauzuiwi kuwa kiongozi ; hata wakina Mustapha Songambele walikuwa madereva wa taxi hapa Dar wakaishia kuwa wakuu wa Mkoa , hiyo ndio ccm na Tanu kabla yake!!
 
nampa heko na kumtia shime. umaskini si deni bali ni mtaji. chochote utakachodhamiria kitatimia. songa mbele utashinda

hivi nani kakuambia mtu anayefanya kazi ndani CCM ni masikini? hasa ukiweka maanani kuwa ni dereva wa kigogo? cheki sura yake ni masikini huyo? hapo ni mchezo ule ule wa kupokezana vijiti kama walivyozoea baba anamwachia mwanae na wajukuu wake. Nape hana mtoto kachagua kumpigia dereva wake rafiki yake huwezi jua yanayofanyika vichochoroni baada ya kazi
 
Binafsi ninarudisha kadi ya CHADEMA jioni ya leo na kesho kutwa nachukua kadi ya ccm na kugombea nafasi ya mwenyekiti mwanza hapo hapo. tutakutana kwenye kujinadi.
 
Back
Top Bottom