Dereva jihadhari na kulipita gari la mbele yako (overtaking) katika maeneo haya

Wakuu habari:
Baada ya kuona ajali nyingi katika bara la Afrika hasa Tanzania zinatokana na upungufu wa uelewa wa Madereva, miundombinu ya barabara na uzembe, zipopia zinazo sababishwa na chombo chenyewe.

Nimeona leo angalau nifungue uzi kuhusu kukumbashana juu ya hatari ya (overtaking)kulipita gari la mbele yako barabarani.
Kumbuka ukiwa kama Dereva mpya au mkongwe basi unapaswa kuzingatia usalama wako, abiria, watumiaji wengine wa barabara na chombo chako ukiwa barabarani.

Karibu.

Kitendo cha kulipita gari la mbele yako katika maeneo yasiyo sahihi na kwa mazoea kimesababisha vilema na hata vifo kwa baadhi ya watu katika jamii zetu.
Maeneo yafuatayo usithubutu kufanya manuva ya overtaking (kulipita gari la mbele yako) {bila ya uangalifu} yatakugharimu siku moja.

1) KWENYE DARAJA: Epuka kulipita gari la mbele yako kwenye madaraja hasa yasiyo na upana toshelevu, madaraja ni sehemu hatari kuvuka kwani huwezi kulikwepa gari litakalo kuja mbele yako wakati una overtake zaidi utalipeleka gari lako kuingia kwenye maji au kugongana uso kwa uso na gari la mbele yako litakalo jitokeza wakati una overtake.

2) KWENYE KONA: Wakati unapokutana na kona inayo kuzuia uwezo wako wa kuona mbali zaid tafadhali usijaribu kulipita gari la mbele yako kwani huwezi kua na uhakika wa aslimia kubwa kama mbele yako kuna gari linalo kuja au hakuna hivyo itakufanya
Kupungaza ufanisi wako wa kuchukua hatua kama litatokea lolote kwa ghafla.

3) JUU YA MLIMA: kama vile kwenye kona, milima, vilima ni mahali pabaya pa kupita huwezi kuona mbele vizuri na unaweza kukosa mwendo wa kutosha wa kulipita gari la mbele yako na kusababisha kugongana na gari ulililo taka kulipita wakati unarudi kwenye njia yako.

4)WAKATI HUWEZI KUONA MBELE KWA WAZI: Ikiwa huwezi kuona sehemu ya mbele vizuri kwa sababu yoyote ile tafadhali usithubutu kulipita gari la mbele yako.

5) MVUA INAPONYESHA: Mvua ikinyesha sana usipilipite gari la mbele yako kwa sababu barabara inaweza kuwa na utelezi na uwezo wa kuona mbali pia unapungua aidha kwa sababu ya mawingu, ukungu na hata matone yenyewe yanapo kithiri.

6) UNAPOFUATILIA MSAFARA WA MAGARI YANAYOENDA HARAKA: Epuka kuyapita magari yaendayo haraka kwenye msafara itakuwa hatari kufanya hivyo hasa kwa Madereva wapya ndio usijaribu kabisa kwani wote mtakua kwenye hali ya mwendo kasi na itakua rahisi kusababisha ajali.

7) BARABARA NYEMBAMBA: baadhi ya barabara ni nyembamba sana kuweza kuchukua magari mawili kwa wakati mmoja, epuka kulipita gari la mbele yako katika aina hizi za barabara.

8) BARABARA INAPOTELEZA: Mvua, maji, mafuta, maeneo yenye maji machafu yanajulikana kuwa na utelezi, kuwa mwangalifu kuhusu ku overtake maeneo ya aina hii.

9) MADEREVA WACHOKOZI: Epuka kuwapita madereva wenye fujo. Hawa ni madereva ambao huongeza mwendo kasi kila unapojaribu kuwapita ili kukuepusha na kuovertake. Madereva wa aina hii wanaona barabara kama njia ya mbio, ni madereva hatari na wanaweza kusababisha ajali kwa urahisi.

Kwa usalama wako na wengine, epuka kuwapita madereva wa aina hii, huna haja ya kuthibitisha kuwa wewe ni mwepesi au bora kuliko yeye, tafadhali usikimbilie kwenda kaburini.

10)WAKATI HUWEZI KWA UWAZI KUONA GARI LINALOTOKEA UELEKEO WA NJIA NYINGINE : Usidhani gari liko mbali, Mfano wale wazee wa tailage
A.K.A Wazee wa kubusu kalio au wazee wa kula mkia, watu wengi walifika kaburini kabla ya kutambua makosa yao. Tafakari kwanza wakati una overtake je umeshajiridhisha kua mbele ni salama na umeona kweli ni salama barabarani sio sehemu ya throne Bet hapahitajiki kubeti wazee.

11) WAKATI WA KUENDESHA USIKU: Kuendesha gari usiku kunahusisha tahadhari na uangalifu mkubwa, kama huoni vizuri tafadhali usi overtake, kama huna macho yenye ubora wa kuona usiku vizuri usiendeshe gari usiku kabisa, ikiwa ni lazima. fanya hivyo, endesha gari kwa uangalifu wote.

12)Usi overtake kwenye junction sehemu ambapo barabara zinakutana au njia ndogo inaingia njia kubwa mana unaeza kuta kuna gari inaingia bada ya kukadiria spidi ya gari unayotaka kuipita...

13) USI OVERTAKE kwenye barabara inayo toa vumbi jingi kiasi ambacho mbele huwezi kuona vizuri.

Index: neno kulipita gari jengine la mbele yako ni sawasawa na neno overtaking hivyo ukilikuta moja au yote basi maana ni moja.

NB: maeneo yenye alama na michoro isiyo ruhusu ku overtake hupaswi ku overtake hata kama unahisi kufanya hivyo ni salama.
Thanks.
AKSANTE SANA SANA KUKUMBUSHANA !!!! SEMA POMBE, DEMU MKALI KUSHOTO, SIMU,BANGI NA KIBURI CHA MADEREVA ESPECIALY WA SERIKALI TAHADHARI HAZIZINGATIWI KABISA KABISA!!!!!!!! Aksante tena
 
Vyema, wenye leseni za kuletewa waendelee kuelimika, waking we tujikumbushe
Barabara ina mambo mengi ukongwe na na umahiri wa uendeshaji haukuponyi na ajali. Kuna wakati wazembe wanakusababishia ajali kwa uzembe wao.

Mfano we unafika darajani halafu mpuuzi anachomoka kutoka upande wake kuelekea upande wako kwa kumuovateki mwenzake. Hamadi, mnakutana uso kwa uso na jambo baya linatokea.

Mfano 2. Tairi la mwezako linachomoka kwa spidi na kuja upande wako wakati na wewe uko spidi, ama tairi lako linachomoka ghafla.

Mf no 3. Mwenzako anaacha njia gari analileta upande wako

Ajali haina bingwa.

Sali sana, mlilie sana Mungu kupatie ulinzi kabla ya kuingiza chombo barabarani.

Kuna mazingira ya kutia hofu sana barabarani.
 
Kuna maeneo ambayo hauruhusiwi kulipita gari la mbele kama gari la mbele linakwenda taratibu na mbele unona vizuri hakuna gari linalokuja na kama unataka kulipita ilo gari ni vizuri kuwasha indiketa ya kuomba kupita na ukiona hajakujibu basi jaribu kumpigia oni.

Malori mengi kwenye highway uwa wanatoa ushirikiano haswa kwenye hayo maemeo atakuruhusu umpite na hata kama itatokea gari kwa mbele linakuja atapunguza mwendo ili upite salama..

Hata mimi binafsi kama kuna gari linataka kunipita kwenye maeneo yanayokatza nitamruhusu lakini napunguza mwendo ili aweze kupita salama.
 
Basi la newforce liliniingiza kweny matuta ya viazi mbatata nikiwa na baiskeli yangu kwa sababu ya michezo hii ya kuovertake, niliinuka pale nikiwa sina tofauti na viazi, vumbi mpaka puani. Yule dereva mpaka leo namtafuta mshenz yule.
 
Barabara ina mambo mengi ukongwe na na umahiri wa uendeshaji haukuponyi na ajali. Kuna wakati wazembe wanakusababishia ajali kwa uzembe wao.

Mfano we unafika darajani halafu mpuuzi anachomoka kutoka upande wake kuelekea upande wako kwa kumuovateki mwenzake. Hamadi, mnakutana uso kwa uso na jambo baya linatokea.

Mfano 2. Tairi la mwezako linachomoka kwa spidi na kuja upande wako wakati na wewe uko spidi, ama tairi lako linachomoka ghafla.

Mf no 3. Mwenzako anaacha njia gari analileta upande wako

Ajali haina bingwa.

Sali sana, mlilie sana Mungu kupatie ulinzi kabla ya kuingiza chombo barabarani.

Kuna mazingira ya kutia hofu sana barabarani.
Kweli ndugu, Mungu ni kila kitu ..... 90% za ajali ni uzembe wa madereva
 
Hakuna madereva wa ovyo km wa mabasi.yaani analazmisha kuovetaki na ukimuona ametanua inabidi utoe tairi zako nje maana huwa hawarudi.kiukwelii naona madreva wa ovyo wengi ni mabasi
ni kweli kabisa. bahati mbaya jamii tumekaririshwa kuwa madereva wa malori ndiyo wabaya
 
Barabara ina mambo mengi ukongwe na na umahiri wa uendeshaji haukuponyi na ajali. Kuna wakati wazembe wanakusababishia ajali kwa uzembe wao.

Mfano we unafika darajani halafu mpuuzi anachomoka kutoka upande wake kuelekea upande wako kwa kumuovateki mwenzake. Hamadi, mnakutana uso kwa uso na jambo baya linatokea.

Mfano 2. Tairi la mwezako linachomoka kwa spidi na kuja upande wako wakati na wewe uko spidi, ama tairi lako linachomoka ghafla.

Mf no 3. Mwenzako anaacha njia gari analileta upande wako

Ajali haina bingwa.

Sali sana, mlilie sana Mungu kupatie ulinzi kabla ya kuingiza chombo barabarani.

Kuna mazingira ya kutia hofu sana barabarani.
Mpumbavu wewe

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom