Dereva jihadhari na kulipita gari la mbele yako (overtaking) katika maeneo haya

professional Driver

JF-Expert Member
Sep 23, 2022
2,959
3,492
Wakuu habari:
Baada ya kuona ajali nyingi katika bara la Afrika hasa Tanzania zinatokana na upungufu wa uelewa wa Madereva, miundombinu ya barabara na uzembe, zipopia zinazo sababishwa na chombo chenyewe.

Nimeona leo angalau nifungue uzi kuhusu kukumbashana juu ya hatari ya (overtaking)kulipita gari la mbele yako barabarani.
Kumbuka ukiwa kama Dereva mpya au mkongwe basi unapaswa kuzingatia usalama wako, abiria, watumiaji wengine wa barabara na chombo chako ukiwa barabarani.

Karibu.

Kitendo cha kulipita gari la mbele yako katika maeneo yasiyo sahihi na kwa mazoea kimesababisha vilema na hata vifo kwa baadhi ya watu katika jamii zetu.
Maeneo yafuatayo usithubutu kufanya manuva ya overtaking (kulipita gari la mbele yako) {bila ya uangalifu} yatakugharimu siku moja.

1) KWENYE DARAJA: Epuka kulipita gari la mbele yako kwenye madaraja hasa yasiyo na upana toshelevu, madaraja ni sehemu hatari kuvuka kwani huwezi kulikwepa gari litakalo kuja mbele yako wakati una overtake zaidi utalipeleka gari lako kuingia kwenye maji au kugongana uso kwa uso na gari la mbele yako litakalo jitokeza wakati una overtake.

2) KWENYE KONA: Wakati unapokutana na kona inayo kuzuia uwezo wako wa kuona mbali zaid tafadhali usijaribu kulipita gari la mbele yako kwani huwezi kua na uhakika wa aslimia kubwa kama mbele yako kuna gari linalo kuja au hakuna hivyo itakufanya
Kupungaza ufanisi wako wa kuchukua hatua kama litatokea lolote kwa ghafla.

3) JUU YA MLIMA: kama vile kwenye kona, milima, vilima ni mahali pabaya pa kupita huwezi kuona mbele vizuri na unaweza kukosa mwendo wa kutosha wa kulipita gari la mbele yako na kusababisha kugongana na gari ulililo taka kulipita wakati unarudi kwenye njia yako.


4)WAKATI HUWEZI KUONA MBELE KWA WAZI: Ikiwa huwezi kuona sehemu ya mbele vizuri kwa sababu yoyote ile tafadhali usithubutu kulipita gari la mbele yako.

5) MVUA INAPONYESHA: Mvua ikinyesha sana usipilipite gari la mbele yako kwa sababu barabara inaweza kuwa na utelezi na uwezo wa kuona mbali pia unapungua aidha kwa sababu ya mawingu, ukungu na hata matone yenyewe yanapo kithiri.

6) UNAPOFUATILIA MSAFARA WA MAGARI YANAYOENDA HARAKA: Epuka kuyapita magari yaendayo haraka kwenye msafara itakuwa hatari kufanya hivyo hasa kwa Madereva wapya ndio usijaribu kabisa kwani wote mtakua kwenye hali ya mwendo kasi na itakua rahisi kusababisha ajali.

7) BARABARA NYEMBAMBA: baadhi ya barabara ni nyembamba sana kuweza kuchukua magari mawili kwa wakati mmoja, epuka kulipita gari la mbele yako katika aina hizi za barabara.

8) BARABARA INAPOTELEZA: Mvua, maji, mafuta, maeneo yenye maji machafu yanajulikana kuwa na utelezi, kuwa mwangalifu kuhusu ku overtake maeneo ya aina hii.

9) MADEREVA WACHOKOZI: Epuka kuwapita madereva wenye fujo. Hawa ni madereva ambao huongeza mwendo kasi kila unapojaribu kuwapita ili kukuepusha na kuovertake. Madereva wa aina hii wanaona barabara kama njia ya mbio, ni madereva hatari na wanaweza kusababisha ajali kwa urahisi.

Kwa usalama wako na wengine, epuka kuwapita madereva wa aina hii, huna haja ya kuthibitisha kuwa wewe ni mwepesi au bora kuliko yeye, tafadhali usikimbilie kwenda kaburini.

10)WAKATI HUWEZI KWA UWAZI KUONA GARI LINALOTOKEA UELEKEO WA NJIA NYINGINE : Usidhani gari liko mbali, Mfano wale wazee wa tailage
A.K.A Wazee wa kubusu kalio au wazee wa kula mkia, watu wengi walifika kaburini kabla ya kutambua makosa yao. Tafakari kwanza wakati una overtake je umeshajiridhisha kua mbele ni salama na umeona kweli ni salama barabarani sio sehemu ya throne Bet hapahitajiki kubeti wazee.

11) WAKATI WA KUENDESHA USIKU: Kuendesha gari usiku kunahusisha tahadhari na uangalifu mkubwa, kama huoni vizuri tafadhali usi overtake, kama huna macho yenye ubora wa kuona usiku vizuri usiendeshe gari usiku kabisa, ikiwa ni lazima. fanya hivyo, endesha gari kwa uangalifu wote.

12)Usi overtake kwenye junction sehemu ambapo barabara zinakutana au njia ndogo inaingia njia kubwa mana unaeza kuta kuna gari inaingia bada ya kukadiria spidi ya gari unayotaka kuipita...

13) USI OVERTAKE kwenye barabara inayo toa vumbi jingi kiasi ambacho mbele huwezi kuona vizuri.

Index: neno kulipita gari jengine la mbele yako ni sawasawa na neno overtaking hivyo ukilikuta moja au yote basi maana ni moja.

NB: maeneo yenye alama na michoro isiyo ruhusu ku overtake hupaswi ku overtake hata kama unahisi kufanya hivyo ni salama.
Thanks.
 
Hyo namba 2 niyamoto sana.
Siku moja nipo mishemishe na kiboxa changu(pimped),natembea kiatu ile mbaya halafu barabara ya vumbi...

Ile kufika kwenye kona ile naovateki kumbe jamaa hajaniona,nkaongza moto nikamuacha mpinzani halafu npo pembezoni mwa barabara.....
Nikawa nachambua ili nirudi road,chuma ikanishinda na ile spidi nkajikuta nmevamia mahindi pembeni ya barabara...

Wenge linakuja kunitoka naskia "amepona huyo"
Nyomi la watu wamenizunguka
 
Hyo namba 2 niyamoto sana.
Siku moja nipo mishemishe na kiboxa changu(pimped),natembea kiatu ile mbaya halafu barabara ya vumbi...

Ile kufika kwenye kona ile naovateki kumbe jamaa hajaniona,nkaongza moto nikamuacha mpinzani halafu npo pembezoni mwa barabara.....
Nikawa nachambua ili nirudi road,chuma ikanishinda na ile spidi nkajikuta nmevamia mahindi pembeni ya barabara...

Wenge linakuja kunitoka naskia "amepona huyo"
Nyomi la watu wamenizunguka
Hahaha ila pole sana jamaa unasikia ile kapona huyo uamini kama kweli umepona dah
 
Back
Top Bottom