Dereva aliyesababisha ajali ya Wangwe aachiliwa huru; kesi haikufunguliwa mahakama sahihi!

tamthilia ya Malya kwanza huyu jamaa Kaishi hotel mpaka siku ya kutoka,Na watumishi waliokuwa wana mhudumia hapo hotelini ni jiran...gerezan kakaa muda mchache.

kheee kumbe we mfanyakazi wa hoteli ? hongera kwa kumhudumia kijana mallya
 
Siasa ni mchezo mchafu hasa kwa nchi zetu za ulimwengu wa tatu ambazo sheria inakuwa applicable kwa walalahaoi tu!!Vyama vya siasa vimejaa UMAFIA vikitanguliza maslahi binafsi mbele!!Nimekukumbuka sana Jembe langu Wangwe (R.I.P)!Siasa za Tz bado zina safari ndefu kufikia demokrasia ya kweli!!
 
kikubwa nikumpongeza yeye kwa kushinda kesi na mahakama kwa kutenda haki ushabiki wa siasa za LIPUMBA ,MREMA na MBATIA hauna nafasi ktk mambo ya sheria.
 
Monday, 05 March 2012 22:55
digg

By The Citizen Correspondent
Dodoma. The Court of Appeal in Dodoma yesterday set free the 27-year-old Deus Mallya ......... said one of the reasons for quashing the judgement was that the case was supposed to have been filed at Kongwa District Court and not at Dodoma Resident Magistrate's Court.

Kuna wakati nadhani nafahamu maana ya sheria...ila kuna wakati naelewa sielewi maana ya sheria kabisa!
Yaani hapa halizungumzwi kosa lenyewe, ila mwendendo wa mashtaka!
 
Kama kuna identical behavior hapa bongo basi ni SHERIA na METHALI.

METHALI za Kiswahili:
1. Chelewa chelewa utamkuta mwana si wako (haraka haraka haina baraka)
2. Ngoja ngoja inaumiza matumbo (kawia ufike)
Ndio zetu hizo, inatumika inayovutia upande wetu mara tuwambapo.

SHERIA za Tanzania:
1. Deus Mallya kaendesha gari kizembe, kasababisha kifo cha mtu mmoja; Jela miaka mi3
2. Andrew Chenge kaendesha gari kizembe kasababisha vifo vya watu wawili; Faini laki 7
3. Deus Mallya kaendesha gari bila leseni (sio leseni inayoendesha gari kwa ustadi); kavunja sheria na adhabu kali ikachukuliwa
4. Andrew Chenge kaendesha gari bila BIMA (bima ndio ingewafidia ndugu wa marehemu); alivunja sheria, lkn adhabu ndio ile

Hapa utaona kuwa mshtakiwa wa kesi ya pili ana makosa mengine zaidi;
1. Akiwa kama mwanasheria, anafahamu fika kuwa kughushi ni kosa: Alighushi bima na kuibandika kwenye gari lake
2. Akiwa kama mwanasheria anajua wazi kuwa kuidanganya mahakama ni kosa; yet still alipanua mdomo kusisistiza kuwa bima ile ni ya ukweli

Hapa ndio nawashangaa ndugu zangu mnaopinga maandamano na kutushauri tufuate taratibu; kwa sheria hizi zenye double standards au kwa zile za Mungu?

Sheria inafuatwa kwa walalahoi tu hao mafisadi huwa haiwahusu ule msemo kuwa sheria ni msumeno inakata kotekote kwa walalahoi ni tofauti kwao ni kisu kinakata upande mmoja tu!!!
 
Pamoja na kuwa keshaserve ndan muda ila ni furaha sasa kuwa huru zaidi.. Nadhan kuna mambo ya kisheria yalikuwa hayajakamilika. Now its over.

Kwani wakati ana appeal alipewa bail pending appeal?
Mana kama ni la,mbona ameshaserve hiyo miaka yake si wamesema tangu 2008 ama sjaelewa fresh?
Hiyo judgement ni useful kwa precedent tu lakn kimsingi kashaserve muda mrefu ndani

Kisheria Malya hajawahi kufungwa!

Sijui sheria zetu za Tz, lakini Mallya anaweza kuomba fidia. Nakumbuka kesi moja huko Ulaya iliyotolewa kwenye 'nyepesi nyepesi' kuwa marehemu alishinda kesi iliyomhukumu kunyongwa na akiwa amekwishanyongwa. Kilichotokea ni kuwa wakili wake alikuja kuomba rufaa baadaye (kwa kibali maalumu) baada ya kugundua kulikuwa na ushahidi ambao ungemweka mshitakiwa (marehemu) huru. Baada ya kushinda kesi, walifungua madai ya fidia. Sasa sijui kwa Tanzania hasa ukizingatia mshitaki ni Jamhuri!
 
"Malya was convicted on March 18, 2008, of driving a car without a valid licence and driving recklessly. He was sentenced to three years in jail by the then Dodoma District resident magistrate Thomas Simba.

Following the judgement, Mallya appealed to the Court of Appeal. The accident that killed Mr Wangwe
occurred on July 28, 2008, at Panda Mbili in Kongwa District in Dodoma Region"

Hapo kwenye RED ndio huwa nakubaliana na mtazamo wa Rais Mkapa juu ya uvivu wa waandishi wa habari Tanzania.

Hizo ni typo errors -- lakini kiini cha habari ni sahihi. hata hivyo Mkapa naye ni mwandishi wa habari naye mvivu sana. aliwahi kusema huko nyuma akiwa bado Rais kwamba baada ya kustahafu angependelea kuandika. Kwa kuwa anaimudu vizuri lugha ya Kiingereza, tulitarajia kuona makala zake katika magazeti yetu ya kiingereza, lakini yuko kimya.....!

Sababu zenyewe ni kwamba amejitwisha zigo kubwa la ufisadi kwamba anaona haya kuandika.
 
Kwa hiyo hukumu imebatilishwa kwa sababu sio murder na filing yake ilifanyika kwenye mahakama sio sahihi? Hivi tofauti ya traffic case na murder au manslaughter baada ya dereva kugonga na kuua ni ipi?
Mkuu kwa sheria za Tanzania kosa la kugonga na kuua lipo chini ya Sheria ya makosa barabarani hivo ni 'traffic offence' na siyo kosa la mauaji ie murder and manslaughter yenyewe yapo chini ya Penal Code Cap 16. Makosa ya barabarani ikiwemo kugonga na kusababisha kifo yanapaswa kufunguliwa kwenye mahakama ya wilaya.
 
Binafsi naona kazi aliyotumwa amefanikisha kwa hiyo yuko huru......fikiria wale askari waliotumwa kumuua Gen. Imrani Kombe, nao waliachiwa majuzi.

Hii ni dunia ya tatu, tule vile tulivyonavyo na kisha tusubiri haki itokayo kwa Mungu, hapa duniani haki haipo. Lakini hata hao wanaminya haki za wengine mbona Mungu akichoka anawaadhibu?? Fikiria Muamar Gadafi, Shekh Yahya hussein, n.k.
 
Mmmhhhhh!

Sheria.

Ina uzuri wake.

Na ubaya wake.

Watu nao je?

Hamna kitu hapo bali usanii tu, Jamhuri na Polisi wanajua kwa hakika kuwa ajali ilitokea Kongwa kwa nini wapeleke Dom?
Kama kupeleka Dom badala ya Mahakama iliopo karibu na tukio ni kosa mbona WanaCDM wanaosemekana kumdhalilisha DC Kimario kule Igunga mwaka jana walipelekwa kushitakiwa Tabora Mjini? Mimi naona nchi yetu imejaa 'Wasanii' kwenye Mihimili yote-Bunge, Serikali na Mahakama.
 
Kisheria Malya hajawahi kufungwa!
Ila aliwahi kukaa jela kwa miaka kadhaa!! tehtehteh!..
Sheria hapa ndipo inaponichosha, inanikumbusha juzi kuna lori limegonga kimkweche changu trafiki walivyotaka kujipendekeza nikawaambia tumeshaelewana jamaa atanilipa, gari iko gereji na leo naichukuwa, lakini ningetaka hizi sheria zenu za kihuni sijui uje kuclaim insurance basi lazima utalijuwa jiji.
 
Kwa hiyo hukumu imebatilishwa kwa sababu sio murder na filing yake ilifanyika kwenye mahakama sio sahihi? Hivi tofauti ya traffic case na murder au manslaughter baada ya dereva kugonga na kuua ni ipi?

1. Traffic case:- without malice aforethought ............ accident in nature
2. Murder:- with malice aforethought .........................criminal in nature
3. Manslaughter:- without malice aforethought ............criminal in nature
 
Kwa nijuavyo mimi Deus Malya hakuwa gerezani na alikata rufaa ya hukumu ya awali kwani juzijuzi tu(Wiki tatu zilizopita) amefanya utapeli kwenye hotel moja dodoma kwa kula na kulala bila kulipa akisingizia eti alikuwa kwenye mkutano ukumbi wa Chimwaga chuo kikuu cha Dodoma
 
Sijui sheria zetu za Tz, lakini Mallya anaweza kuomba fidia. Nakumbuka kesi moja huko Ulaya iliyotolewa kwenye 'nyepesi nyepesi' kuwa marehemu alishinda kesi iliyomhukumu kunyongwa na akiwa amekwishanyongwa. Kilichotokea ni kuwa wakili wake alikuja kuomba rufaa baadaye (kwa kibali maalumu) baada ya kugundua kulikuwa na ushahidi ambao ungemweka mshitakiwa (marehemu) huru. Baada ya kushinda kesi, walifungua madai ya fidia. Sasa sijui kwa Tanzania hasa ukizingatia mshitaki ni Jamhuri!

Ukisoma vizuri hiyo habari haizungumzii kosa lenyewe kwa hiyo, hiyo ni judicial review na kwa uelewa wangu kilichofanyiwa review ni legal technicalities au principles kama vile jurisdiction ya kesi ambapo hiyo review itatumika kama precedent katika siku zijazo namna ambavyo mahakama za chini zitapaswa kufuata kwenye mazingira kama hayo na siyo innocence vs guiltiness of the accused person. Kwa hiyo Mallya hawezi kudai fidia kama habari itakuwa imeishia hapo labda kwa sababu hiyo ni one of the reasons for quashing the judgement tusubiri hizo sababu zingine
 
Following the judgement, Mallya appealed to the Court of Appeal. The accident that killed Mr Wangwe occurred on July 28, 2008, at Panda Mbili in Kongwa District in Dodoma Region.

Ni kwa nini hakukata rufaa High court au mwandishi alikosea uhakika?
 
Hapo umenena mkuu....kweli kabisa lakini kwa hapa Tz sheria ziko kwa wale wasio na kitu kwani wenye kitu wanaonekana kama wako juu ya sheria. Ukienda kwenye magereza zetu wengi wa wafungwa na washitakiwa wabembakiwa kesi. Sheria zetu ziko wazi kwamba ukishitakiwa kwa kosa la KUUA basi mdhamana haupo...lakini unakumbuka issue ya Marehemu Dito na yule Marehemu dereva wa Daladala..?? aliendesha kesi akiwa nje kwa mdhamana.
Iko siku watz hawa wote kwa ujumla wao watazitambua haki zao na kuanza kuzidai na hapo wale waliokuwa wananeemeka kwa mgongo wa kununua sheria watakapoaibika. IKO SIKU "HAKI ITATAWALA" hata Mungu amelisemea hili kwenye maandiko matakatifu.

Back
Top Bottom