Deodatus Balile kama Mzee Mwanakijiji

Nimemsikiliza Deodatus Balile leo StarTv tuzungumze magazeti, mhhhhhhhhh! ameniacha hoi! Haoni tatizo lolote na awamu ya Tano! Kila kitu ni shwari na salama. ANASIFIA KILA KITU, Amebadilika, kweli woga umetamalaki kila kona!
Odero and Pasco are more analytical and critical thinkers than Balile, Balile ameangukia kwenye kundi la kusifia kama CCM!
Amebadilika? Au ulikuwa humfuatilii vizuri Balile?!Sijawahi kuona Balile akiwa mfuasi wa issue zaidi ya mtu!

The guy is good katika kujenga hoja... usipokuwa makini unaweza kudhani ni mtu wa issue lakini kimsingi chambuzi zake mara zote zinalenga kubeba watu na sio hoja. Wakati ambao ulikuwa unamuona ni kama positive thinker ni kv zamani ilikuwa ukimgusa Lowassa, Balile anaweza kukuillia mbele ya kamera!

Sasa baada ya Uswahiba wa JK na Lowassa kwenda halijojo, ndipo hapo akawa ni kama positive thinker, but it's all about Lowassa! Endapo JK na EL wangeendelea kuwa dugu moja, hayo uliyoyaona leo kwa Balile ingekuwa ushayazoea kitambo!! Kama unabisha, soma tahariri yake kwenye gazeti la Rai, April 24, 2008! Balile huyu hapa:
Katika kipindi cha takribani miezi minne hivi,hapa nchini yametoke mambo ya kusikitisha.

Tumeshuhudia baadhi ya viongozi wetu wa serikali wakijiuzulu nyadhifa zao kutokana na tuhuma za ufujaji wa fedha za umma. Sababu kuu zinazoelezwa za kujiuzulu kwa viongozi hao,ni matumizi mabaya ya nyadhifa zao. Hali hiyo imesababisha baadhi ya yao kujikuta wakidaiwa kutumbukia katika mitego ya rushwa hali inayosababishwa na tamaa ya kujilimbikizia mali.

kutokana na misingi ya utawala bora,iliyoimarishwa zaidi katika serikali ya awamu ya nne,viongozi wote waliohusishwa na kashifa za ubadhirifu wa fedha za umma ,bila kujali iwapo wamehusika au la,wamewajibika kisiasa. Hilo ni jambo jema kwa taifa letu.

Ingawa viongozi hao wamejiuzulu kwa ridhaa yao kama hatua ya kutimiza misingi ya demokrasia na utawala bora,tungependa kuona hatua moja mbele zaidi. Hatua hii ni kuwachunguza na kubaini nani anahusika vipi.Tunapenda sheria ichukue mkondo wake,ambapo wote watakaobainika kuhusika watatiwa hatiani na kutumikia adhabu zao kwa mujibu wa sheria.

Hatuwezi kuhukumu,ila tunayo maswali ya kuuliza. Tunajiuliza iwapo waliojiuzulu kweli walihusika na hayo waliyotuhumiwa nayo,je, taifa hili lina viongozi wa aina gani? viongozi wetu wanajenga picha gani kwa Rais Jakaya Kikwete aliyewateua?

Pia kuna jambo la kusikitisha. Kwa sasa katika mfumo wea siasa za vingi ni rahisi kukinyooshea kidole chama tawala,CCM.Ni rahisi zaidi kuinyooshea serikali iliyopo madarakani . Ni rahisi mno kusema kwamba serikali haitekelezi wajibu wake ipasavyo.

Hili si jambo la kheri. Ni hatari kwani hali inavyoelekea taifa hili linakaribia kutumbukia katika mtego. Kwamba tumeacha mkondo wa kuzungumzia maendeleo, tumejikita katika ufisadi.


Ingawa wahenga walisema kuwa samaki mmoja akioza wote wameoza, si lazima usemi huu uwe sahihi kwa hili la mafisadi. Ukweli unabaki kuwa wapo viongozi wengine wanaotambua wajibu wao na wenye uchungu na nchi yao. Tusiwachafue hawa kwa uozo wa wenzao. Tusiwachafue kwa tope la ufisadi.

Kama taifa tunahitaji tafsiri mpya ya neno ufisadi. Ufisadi umekuwa msamiati maarufu kweli katika taifa hili, na kila kona kuna msukumo(pressure) wa kuaminisha jamii kuwa kwa sasa kila mwanasiasa ni fisadi.

tumejiingiza katika mijadala isiyotoa majibu kwa matatizo yanayotukabili. Ni vyema sasa tuanze kubainisha njia nzuri za kukuza uchumi wa taifa hili. Serikali nayo ifike mahali ijue kuwa hakuna uhuru usio na mipaka. Kuwaachia watu wakaendelea na mjadala wa ufisadi huku wakipotosha ajenda ya maendeleo hakulisaidii taifa hili.

Kwamba serikali nayo sasa inaelekea kutumia muda wake mwingi kujadili ufisadi,badala ya kutueleza jinsi ya kujenga visima vya maji,barabara.zahanati,shule za sekondari na bila kusahau madawati katika shule za msingi,ni hatari pia.wakati umefika sasa tubadilike, au tutabadilishwa na upepo tusioujua si muda mrefu.

tunapaswa kutambua kuwa tumebakiza muda kidogo kabla ya serikali ya awamu ya nne kumaliza kipindi cha kwanza cha miaka mitano. Katika kipindi hiki tunapaswa kurejea katika ilani ya uchaguzi na kujiuliza serikali iliahidi nini na mpaka sasa imetekeleza nini. Huu utakuwa mjadala sahihi kwa ustawi wa taifa hili.

kutonakana na hali hiyo,watanzania tunapaswa kufumbua macho na kuangalia mbele kuhusu matatizo mengine ya kijamii. Ufisadi ni tatizo mojawapo ndiyo,tunasema usifumbiwe macho,ila usitupofushe katika matatizo mengine. Kama tupo kwenye mapambano ya kweli dhidi ya matatizo yanayolikabili taifa letu ni wazi mkakati wa sasa wa ufisadi hatufikishi tutakako. Mungu Ibariki Tanzania.
Now tell me, hivi Balile huyo hapo juu ndie yule wa serikali ya JK iliyomaliza muda wake? By April 24, 2008 tayari serikali ya CCM ilishakuwa kwenye kashfa mzito ya IPTL, EPA na Richmond let alone kashfa ya Meremeta, Kagoda, Deep Green n.k!

Lakini kv Lowassa bado alikuwa na nafasi CCM, Balile akawa anataka serikali izitie adabu media zinazojadili masuala ya ufisadi kv hakuna uhuru usio na mipaka. Kuwaachia watu wakaendelea na mjadala wa ufisadi huku wakipotosha ajenda ya maendeleo hakulisaidii taifa hili.

That's Balile bro!
 
Unaweza kujikuta uko peke yako kwa sababu hujiulizi kwa undani zaidi kwa nini wamebadilika?

Mtu mwenye hekima na busara achilia mbali komono sensi akiona baadhi ya watu aliokuwa anakubaliana nao wameanza kubadilika basi huanza kujiuliza maswali magumu ili apate majibu.

Siasa siyo ushabiki. Siasa ni muamuzi mkuu katika maisha.

Kwa kukusaidia zaidi, achana na huyu Pasco wa Jamiiforums, mtafute pia huyu Pascal Mayalla ili uwasikie wote kuhusu kauli zao kuhusiana na uongozi wa Rais Magufuli!

Uyu Paskal Mayalla ni kibaraka wa ccm, kila mtu anamjua.
 
Amebadilika? Au ulikuwa humfuatilii vizuri Balile?!Sijawahi kuona Balile akiwa mfuasi wa issue zaidi ya mtu! The guy is good katika kujenga hoja... usipokuwa makini unaweza kudhani ni mtu wa issue lakini kimsingi chambuzi zake mara zote zinalenga kubeba watu na sio hoja. Wakati ambao ulikuwa unamuona ni kama positive thinker ni kv zamani ilikuwa ukimgusa Lowassa, Balile anaweza kukulia mbele ya kamera! Sasa baada ya Uswahiba wa JK na Lowassa kwenda halijojo, ndipo hapo akawa ni kama positive thinker, but it's all about Lowassa! Endapo JK na EL wangeendelea kuwa dugu moja, hayo uliyoyaona leo kwa Balile ingekuwa ushayazoea kitambo!! Kama unabisha, soma tahariri yake kwenye gazeti la Rai, April 24, 2008! Balile huyu hapa: Now tell me, hivi Balile huyo hapo juu ndie yule wa serikali ya JK iliyomaliza muda wake? By April 24, 2008 tayari serikali ya CCM ilishakuwa kwenye kashfa mzito ya IPTL, EPA na Richmond let alone kashfa ya Meremeta, Kagoda, Deep Green n.k! Lakini kv Lowassa bado alikuwa na nafasi CCM, Balile akawa anataka serikali izitie adabu media zinazojadili masuala ya ufisadi kv hakuna uhuru usio na mipaka. Kuwaachia watu wakaendelea na mjadala wa ufisadi huku wakipotosha ajenda ya maendeleo hakulisaidii taifa hili. That's Balile bro!
Nimekuelewa! Sikuwahi kusoma makala hii ( siyo mfuatiliaji sana wa siasa), ila napenda kujua ukweli katika kitu chenye maslahi ya wengi- hasa democracy inapokuwa tempered with. Sentensi yake ya mwisho inanipa mashaka makubwa na uzalendo wake! Kuna mtu/watu "mwovu" alikuwa anamtetea/anawatetea kwa kuzima mijadala ya ufisadi isiendelee wakati kuna hizo catastrophe ulizozitaja IPTL etc!
 
Nimemsikiliza Deodatus Balile leo StarTv tuzungumze magazeti, Mmmh! ameniacha hoi! Haoni tatizo lolote na awamu ya tano! Kila kitu ni shwari na salama. ANASIFIA KILA KITU, Amebadilika, kweli woga umetamalaki kila kona!

Odero and Pasco are more analytical and critical thinkers than Balile, Balile ameangukia kwenye kundi la kusifia kama CCM!
Mkuu Chuakachara, hili bandiko ndio nimeona leo. Kama CCM inafanya mambo mazuri, jee kuna ubaya wowote mtu kuisifia na usionekane unajipekeza CCM?.

Kama rais Magufuli anafanya mambo mazuri, jee kuna ubaya kumsifia bila kuona unajipekeza kusaka uteuzi?.

P
 
Mkuu Chuakachara, hili bandiko ndio nimeona leo. Kama CCM inafanya mambo mazuri, jee kuna ubaya wowote mtu kuisifia na usionekane unajipekeza CCM?.

Kama rais Magufuli anafanya mambo mazuri, jee kuna ubaya kumsifia bila kuona unajipekeza kusaka uteuzi?.

P
Pascal nimesema mara nyingi na kuna mtu humu , namuunga mkono, kuwa AS LONG AS MAZURI YANAAMBATANA NA KUUA WATU, KUPOTEZA WATU, KUPIGWA RISASI 38, and the like, WHATEVER GOOD ONE MIGHT BE DOING , if at all are there, GO DOWN BY THE TRENCH! SIWEZI KUSIFIA MUUAJI ETI kwa vile KANILETEA SGR, NDEGE ETC.
 
Pascal nimesema mara nyingi na kuna mtu humu , namuunga mkono, kuwa AS LONG AS MAZURI YANAAMBATANA NA KUUA WATU, KUPOTEZA WATU, KUPIGWA RISASI 38, and the like, WHATEVER GOOD ONE MIGHT BE DOING , if at all are there, GO DOWN BY THE TRENCH! SIWEZI KUSIFIA MUUAJI ETI kwa vile KANILETEA SGR, NDEGE ETC.
So far, there is no proof ni nani amefanya hayo. Kunyoosheana vidole kwa vitu ambayo havina uhakika au uthibitisho ni ramli chonganishi, nimeisha wahi kushauri humu

Matukio hayo yamepangwa na kutekelezwa na watu wasiojulikana


Na wahusika wote wa matukio hayo, hata wasipojulikana, watahukumiwa na hukumu ya karma.
P
 
So far, there is no proof ni nani amefanya hayo. Kunyoosheana vidole kwa vitu ambayo havina uhakika au uthibitisho ni ramli chonganishi, nimeisha wahi kushauri humu

Matukio hayo yamepangwa na kutekelezwa na watu wasiojulikana

P

Sina hakika kama huwajui hawa wababe serial killers
 
Pascal nimesema mara nyingi na kuna mtu humu , namuunga mkono, kuwa AS LONG AS MAZURI YANAAMBATANA NA KUUA WATU, KUPOTEZA WATU, KUPIGWA RISASI 38, and the like, WHATEVER GOOD ONE MIGHT BE DOING , if at all are there, GO DOWN BY THE TRENCH! SIWEZI KUSIFIA MUUAJI ETI kwa vile KANILETEA SGR, NDEGE ETC.
Duh...!.
P
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom