DEO FILIKUNJOMBE AMEOMBA MWONGOZO KWA SPIKA ; kuhusu fedha za rushwa rada

mbunge wa Ludewa ni MWANAUME WA UKWELI ametaka kujua hatima ya waizi na madalali walio tuhujum kwenye rada na ametaka kujua maelezo rasimi kuhusu fedha zilizo rudishwa; na hatua kwa wahujum ametolea mfano uingereza walivyowashughulikia kisawasawa waizi wa fedha zetu za rada kwan upande wa tanzania serikali yetu inaonekana imezubaa kuwashughelikia wezi na madalali wale,,, lakini kwa kuwa makinda ndo mama mwenye nyumba amefunika chini ya kapeti sakata hilo!! nini maoni yako kama mtanzania uliye hujumiwa na kupigwa chenga ya mwili ?kwa sababu kimsingi watanzania hatujatendewa haki ,,
 
Natamani sana mimi ningezaliwa LUDEWA na mbunge wangu kuwa Deo Filikunjombe. Mimi mbunge wangu ni wa Magamba na katika ile orodha ya wabunge ambao hawajawahi kuongea/kuchangia bungeni tangu 2010 na yeye yumo.

Hongera sana Deo tuko nyuma yako. Tunataka kufahamu RUSHWA ya chenji ya rada waliohusika ni akina nani? na wamechukuliwa hatua gani? Komaa kama ulivyomkomalia Boss wa TBS hadi akang'oka, utaingia kwenye historia ya ukombozi wa pili wa nchi hii.
 
ametaka maneno ya kwenye hotuba ya hawa ghasia wazir tamisemi yabadilishwe na yaandikwe hela za wizi na rushwa ya rada na sio chenji za rada kama yalivyo andikwa ,, ametaka historia ya tukio hilo iwekwe bayana 2jue iwasadie na kizaz kijacho ili uhuni huo usittokee tena na iwe mwanzo na mwisho na liwe somo
 
Deo sio mnafiki .. Abarikiwe anafanyika baraka kwa ccm na wana ludewa they proud of him for sure!!
 
Deo yuko sahihi hakukuwa na chenji katika ununuzi wa Rada hata kidogo,ila kulikuwa na fedha ya rushwa na wizi ndani yake. Hivi chenji inaweza kukaliwa vikao vya muda mrefu Dodoma na London?
Hata hivyo CCM badala ya kujinadi kuwa ina mbunge makini, wao watamkalia vikao kuwa ni ADUI na mpinzani wao. Hii maana yake ni nini? ni kuwa Rushwa na wizi huo una baraka za chama.
 
Tunahitaji Wabunge kama hawa 10 tu ndani ya CCM, maana wengine watakuwa wamelala so uwiano wa uwezekano wa mabadiliko ni rahisi kwani walio active lakini wanafiki ukijumlihsa na walio active lakini si wanafiki, wanaweza wasizidi 30.
 
mbunge wa Ludewa ni MWANAUME WA UKWELI ametaka kujua hatima ya waizi na madalali walio tuhujum kwenye rada na ametaka kujua maelezo rasimi kuhusu fedha zilizo rudishwa; na hatua kwa wahujum ametolea mfano uingereza walivyowashughulikia kisawasawa waizi wa fedha zetu za rada kwan upande wa tanzania serikali yetu inaonekana imezubaa kuwashughelikia wezi na madalali wale,,, lakini kwa kuwa makinda ndo mama mwenye nyumba amefunika chini ya kapeti sakata hilo!! nini maoni yako kama mtanzania uliye hujumiwa na kupigwa chenga ya mwili ?kwa sababu kimsingi watanzania hatujatendewa haki ,,
hana cha ukweli wala nini,kama angekuwa mwanaume kweli angepiga kura ya hapana tumsikie,akawaonesha wananchi kuwa yeye haoongozwi na matakwa ya chama.ku kaa kimya kumemprove falier.
 
CCM "watam-Kolimba" huyu bwana anayejifanya haujui mwelekeo ulio wazi wa chama chetu wa "mwalimu usinibaini, wajinga ndiyo waliwao: nikipata mbili moja yangu, moja yako".,
 
Ikiwa rushwa iligeuzwa for convenience's sake ikaitwa takrima na hamkulalamika basi hata nguruwe ikiambiwa imebatizwa na sasa inaitwa samaki, tumieni msilalamike. Au what's food for the goose is poison for the gander?.
 
hongera Deo.
2015 jiondoe CCM na jiunge na kina Godbless Lema ambao ni majasiri kama wewe.
No no no! Deo abakie hukohuko CCM na tunamwombea 2015 ashinde ili CCM itakapo kuwa chama cha upinzani iwe na wabunge makini wa kuikosoa Chadema inapokwenda kombo.
Huwezi kuwa na chama cha upinzani chenye wabunge kama Komba na Lusinde ukategemea kuwa na serikali bora maana hawatakuja na hoja mbadala.
Tumejionea udhaifu wa CCM ukiainishwa na wabunge mahiri wa Chadema atleast sasa serikali inajitambua. Vinginevyo kama haridhiki na hiyo CCM aende NCCR ili aendelee kuisaidia Chadema kwa kupinga yale yatakayo kuwa hayaendi sawasawa.
Nina hakika kwa vile Chadema sio chama cha kipuuzi, hoja zake kama mpinzani HATAZOMEWA (kama ilivyo sasa) ila zitachukuliwa kwa umakini mkubwa na kufanyiwa kazi kwa manufaa ya nchi.
 
Deo ni mwanamume wa shoka.Mimi nadhani hili swala ni nyeti na wabunge wapewe majibu ya kueleweka vinginevyo bajeti ya Waziri mkuu Tamisemi isipitishwe hadi kieleweke na wahusika wachukuliwe hatua za kisheria hasa Andwew Chenge.Hapa ndipo tutaona wabunge wa ccm kama watashikamana tena kuwatetea wezi wa fedha za umma.
 
Back
Top Bottom