Denti auwawa kwa wizi wa Pera

hata mimi nimeiba maembe kwa jirani yangu ni kiwa mtoto, nimeiba makungu shule ya tambaza , nimeiba zambarau, nimeiba mapera....
tumeshakamatwa na mlinzi wa tambaza, akatupa hela na akatutuma tukamnunulie sigara na akawa rafiki yetu akatuambia tukitaka kungu tukamwambie.
tumekamatwa tukiiba embe tukatishiwa halafu baadae yule mzee aktuambia tupande juu ya muembe tukaangua maembe nusu akachukua yeye na nusu sisi, kila tukitaka maembe tunacheza karibu anatuita.

hamna hata mmoja aliyetupiga wala kutupeleka polisi kwa wizi wa matunda
wacheni unafiki watu humu hata polisi kwa wizi wa mapera haitakiwi.....
kama umelelewa maisha ya kawaida asilimia 90% ya wana JF wachangiaji watakua washaenda kuangua matunda bila kibali na mpaka leo mpo hai

huyo anaweza akawa mtoto wako au ndugu yako, kuwaweka kwenye gari tu na kutaka kuwapeleka polisi ni ushenzi.....
 
Back
Top Bottom