Deni la umeme Zanzibar: Magufuli, Shein na Muhongo wakutana Ikulu. Wawaondoa hofu Wazanzibar

Queen V

JF-Expert Member
Jan 19, 2012
776
1,330
C7ReqIpX4AAGKez.jpg


Rais Magufuli leo tarehe 19 Machi 2017 amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, Ikulu Dar es Salaam.

Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Mwijarubi Muhongo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Kahitwa Bishaija na Meneja Mwandamizi wa Fedha wa TANESCO Bw. Sadock Mugendi.

Wakati huo huo, Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo amewatoa hofu wananchi wa Zanzibar kuwa hawatakatiwa umeme baada ya Serikali ya Mapinduzi (SMZ) kuanza kulipa deni inalodaiwa na TANESCO.

Prof. Muhongo amesema tayari SMZ imeanza kulipa kiasi cha Shilingi Bilioni 10 na itaendelea kulipa deni hilo mpaka litakapomalizika.

Aidha, Prof. Muhongo ametoa wito kwa wadaiwa sugu wote wa TANESCO kulipa madeni yao katika kipindi cha siku 5 zilizobaki kwa kuwa wasipolipwa watakatiwa umeme.

Imetolewa na
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
19 Machi, 2017
 
Uongo Mtupu anajitetea SMZ hawana hela ya kulipa waliogopa muungano utavunjika faster ndio maana mzee wa Shilawadu kakimbilia kumuomba shein msamaha kwa yale aliyosema. Hana ubavu wa kukata umeme!!!! yeye ana ubavu wa kuua upinzani na kuwakamata wakina lissu na Lema tuu.
 
Uongo Mtupu anajitetea SMZ hawana hela ya kulipa waliogopa muungano utavunjika faster ndio maana mzee wa Shilewedu kakimbilia kumuomba shein msamaha kwa yale aliyosema. Hana ubavu wa kukata umeme!!!! yeye ana ubavu wa kuua upinzani na kuwakamata wakina lissu na Lema tuu.
Amuombe masmaha kwa kumuita Ikulu? Kwani nani asiyejua kuwa yumeme Zanzibar usingekatwa na si kwa ajili ya Muungano kwani Hata ingekuwa labda ni nchi jirani Je ingekuwq busara Kukata?!?!? Jamani hizi akili bado mmeshikiwa tu hebu wawaachie basi angalau mpaka 2019 ndio wawashikie tena!
 
Uongo Mtupu anajitetea SMZ hawana hela ya kulipa waliogopa muungano utavunjika faster ndio maana mzee wa Shilewedu kakimbilia kumuomba shein msamaha kwa yale aliyosema. Hana ubavu wa kukata umeme!!!! yeye ana ubavu wa kuua upinzani na kuwakamata wakina lissu na Lema tuu.


Unajua zaidi ya 1/2 ya Watalii wanaokuja TZ watakuja shauri ya Zanzibar? Na unajua mapato ya Utalii yanachangia kwa kiasi gani kwenye Uchumi wetu?
 
Nilisema zamani Magufuli na Serikali yake hana ubavu wa kukata umeme Zanzibar.
Ni mkurupujaji tuliemzoea tu.
 
A small gesture kuondoa utata. Deni la Mamia ya mabillioni kwa Billion 10 (ambazo si ajabu zimetoka bara) halafu tunaambiwa hawatakatiwa. Kateni tu ili walipe deni, maana sisi huku hatuna hata nafasi ya kukopa unit moja
 
Sionagi faida ya kuwakumbatia hawa wazanzibar naona wanatutia hasara tu...
 
Back
Top Bottom