Deni la Taifa lapaa!

Mkuu nimekuelewa...!!!! Lakini seriously kuna siku nilikuwa ninaongea na Mfaransa mmoja..., na alisema in not so many words kwamba vitega uchumi ambavyo vipo kanda ya ziwa tu.., kama vingekuwepo kwenye nchi ya watu wanaotumia vichwa vyao na sio tamaa zao, ingewezesha kuendesha nchi nzima..., hivi kwanini hatuwezi kuwalisha east africa nzima..? kama Azam ameweza kutengeneza Juice, kupack unga na kusupply nchi jirani, hivi serikali inashindwa kusimamia vitu kama hivi na kuongeza ajira? tunakalia kusifia ajira za machinga na mabar maid zimeongezeka..., wakati tungeanzisha viwanda kama 50 nchini vingepunguza hao machinga na wakawa na uhakika wa mishahara kila mwisho wa mwezi...,
Na bado maisha yanavyokuwa magumu ndio wizi na ujambazi utaongezeka..., because people have got to eat.

VoR tulikuwa na National Agricultural Products Boards (NAPB), baada yake ikaja National Milling Corporation (NMC) kwenye 1973 hivi na sasa Azam huyo huyo anatumia karakana na maghala ya NMC tuliyoiua wenyewe. Tanzania ni kheri mara elfu tusingekuwa na hayo madini na gesi labda akili ingefanya kazi. Ardhi ya nyanda za juu Kusini inatosha kabisa kulilisha taifa (ingawa ukweli ni kwamba NSGRP imefurika hivi sasa) ila swali moja kubwa, kilimo chetu kinalipa?
Wizi huu wa juzi wa stakabadhi za pembejeo ulikuwepo toka enzi zile za NAPB na Tanzania Fertilizer Company.

Chanzo kikubwa cha ongezeko la madeni haya ni Multilateral debt relief initiative ambayo tulianza kufaidi ahueni hii kwenye 2004 hivi, tukaanza kutupatupa fedha hovyo tukiudanganya umma na wafadhili kwamba ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo. Maendeleo yenyewe yamekuwa ni kutunisha mifuko ya Toyota Motors Limited (T), Dowans, IPTL, ile stimulus uchwara, Kagoda na Meremeta, mabenki ya makaburu (revisit ufisadi wa iliyokuwa NBC na restructuring yake kabla ya kuuzwa) na washenzi wengine wasio na hata chembe ya huruma na nchi hii.

Nikiweka kofia yangu ya uchumi, deni hili si la kufanya watu waogope maana nchi inajitosheleza kwa mapato yake ya uuzaji wa bidhaa nje. Madeni ni kitu cha kawaida ila si mtaji huu wa CCM.

Unajua ingependeza kujua asilimia ngapi ya deni la serikali linatokana na mikopo toka kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii pamoja na mafao. Kuna mabomu huko yanayotungoja in the next five years at most.
 
Hivi wakati tunasamehewa 2001 hizo $ 3 billion deni lilikuwa ni kiasi gani?? Na je wakati JK anaingia magogoni na kudai amerithi uchumi bora na kwamba kazi yake itakuwa ni kujenga ukuta tu deni lilikuwa ni kiasi gani?? Naomba kuuliza!!
 
Sehemu kubwa ya deni hilo ni "interest rate" payable

Kuna haja ya kufikiri kukopa kutoka kwa taasisi ambazo hazitozi riba (interest) kwa faida ya nchi na wananchi wake.
 
Kuna mabomu huko yanayotungoja in the next five years at most.

Kweli Mkuu kuna Time Bomb...., na siku litakapolipuka sijui kama tutakuwa na uwezo wa kupick up the pieces na kuanza upya... maybe things will get better..., but am sure they will get worse before they get better...., kwakweli sometimes ninakuwa ashamed kuongea na wenzangu wa nji jirani, ninapotaja maliasili zetu lakini We have got nothing to show for it....., bora hata hawa wezi wangekuwa wanaiba na kujenga viwanda etc..., sasa hizi VX kweli na majumba South Afrika na England vinasaidiaje nchi? (hata wao watakufa wataviacha)....

I wish Wachina wangekuwa na kidonge cha (patriotism na uchungu wa nchi) kwa kweli ningekinunua na kuwapa hawa wananchi ambao sio wenzetu...
 
Sehemu kubwa ya deni hilo ni "interest rate" payable

Kuna haja ya kufikiri kukopa kutoka kwa taasisi ambazo hazitozi riba (interest) kwa faida ya nchi na wananchi wake.

Nothing comes without strings attached...., Kwa maliasili tulizonazo we dont need kukopa... period.
 
Hivi wakati wa Mkapa akiwa madarakani si tulifutiwa madeni yote? au percentage kubwa ya madeni yalifutwa na tukabaki na deni dogo sana. Sasa hili deni la $10 billioni limetoka wapi na kipi kimefanyika na deni hili kubwa katika kuboresha hali za maisha ya Watanzania walio wengi?

Kuna haja sasa katika kusoma bajeti ya Taifa kwenye Bunge details za deni la Taifa ziwe zinawekwa wazi kabisa, ili tujue tulianza na deni la kiasi gani katika mwaka unaokwisha, tumelipa kiasi gani na limeongezeka kwa kiasi gani na pia hiyo nyongeza ya deni imetumika vipi katika kuboresha maisha ya Watanzania.

Huku kwenye deni la Taifa kwa maoni yangu nako kumejaa ufisadi wa hali ya juu. Si ajabu madudu yote yanyofanywa hazina kwa mfano kukomba pesa zote mwaka jana ili kufanyia kampeni za CCM katika uchaguzi wa 2010 inawezekana kabisa kuwa pesa hizo zinaingizwa katika deni la Taifa.
 
VoR tulikuwa na National Agricultural Products Boards (NAPB), baada yake ikaja National Milling Corporation (NMC) kwenye 1973 hivi na sasa Azam huyo huyo anatumia karakana na maghala ya NMC tuliyoiua wenyewe. Tanzania ni kheri mara elfu tusingekuwa na hayo madini na gesi labda akili ingefanya kazi. Ardhi ya nyanda za juu Kusini inatosha kabisa kulilisha taifa (ingawa ukweli ni kwamba NSGRP imefurika hivi sasa) ila swali moja kubwa, kilimo chetu kinalipa?
Wizi huu wa juzi wa stakabadhi za pembejeo ulikuwepo toka enzi zile za NAPB na Tanzania Fertilizer Company.

Chanzo kikubwa cha ongezeko la madeni haya ni Multilateral debt relief initiative ambayo tulianza kufaidi ahueni hii kwenye 2004 hivi, tukaanza kutupatupa fedha hovyo tukiudanganya umma na wafadhili kwamba ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo. Maendeleo yenyewe yamekuwa ni kutunisha mifuko ya Toyota Motors Limited (T), Dowans, IPTL, ile stimulus uchwara, Kagoda na Meremeta, mabenki ya makaburu (revisit ufisadi wa iliyokuwa NBC na restructuring yake kabla ya kuuzwa) na washenzi wengine wasio na hata chembe ya huruma na nchi hii.

Nikiweka kofia yangu ya uchumi, deni hili si la kufanya watu waogope maana nchi inajitosheleza kwa mapato yake ya uuzaji wa bidhaa nje. Madeni ni kitu cha kawaida ila si mtaji huu wa CCM.

Unajua ingependeza kujua asilimia ngapi ya deni la serikali linatokana na mikopo toka kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii pamoja na mafao. Kuna mabomu huko yanayotungoja in the next five years at most.

Mimi siyo mchumi, hapo kwenye red uko serious?? Maana deni kubwa kuliko hata bajeti yetu halafu tustuke?? Worse enough ongezeko la zaidi ya 30 % in 4 years time it's alarming???

Mimi nafikiri opposition inabidi wawasilishe mada binafsi kuulizia hili deni linavyoballon kila siku. Haaingii akilini kwamba between June 2010 na October 2010 (four months) deni limeongezeka by 0.6 billion. Au hizo ndizo JK alizitumia kununulia T-shirts za kampeni??
 
i didnt expect anything from JK... he hasn't done anything, hajali chochote kinachompa responsibility... he is more attracted to fame and fortune

JK government is the worst nightmare to any patriot
 
Na bado!!! There are more yet to come!!!.. Mpaka tutakapo pata akili ya kuingia mtaani na kupinga ujahili huu kama wenzetu wa Tunisia.
 
Terminal benefits za wanasiasa nazo zinachangia kuongezeka deni.

Nasikia kila mkuu wa mkoa atavuta 40 million X 25 = 1 billion
Wakuu wa wilaya nao 40 million X 25 X 5 = 5 billion
Wabunge sijui zilikuwa ngapi say 40 million X 256 = 10.2 billion
Mawaziri siju....
 
Nothing comes without strings attached...., Kwa maliasili tulizonazo we dont need kukopa... period.

Si rahisi kutokukopa kabisa kama nchi, (almost imposible)

Issue ni kutafuta mkopo nafuu ambao hauna (compounded interest kama wa IFM, WB)
 
Si rahisi kutokukopa kabisa kama nchi, (almost imposible)

Issue ni kutafuta mkopo nafuu ambao hauna (compounded interest kama wa IFM, WB)

Mkuu hapa issue ni kutumia pesa vizuri na sio kufuja..., kwa mtaji huu hata World Bank wakitupa hazina yao yote tutakuwa tumeimaliza in 10 years..., Hata tukipewa pesa bure kwa mtaji wa huu ufujaji haitasaidia kitu..., Angalia Rwanda na Kagame... Je yeye sio champion wa kukataa mikopo...., tunakuwa omba omba wakati tuna maliasili kuliko hao tunaowaomba..., anyway Bob Marley alisema
"In Abundance of Water A Fool Is Thirsty"
 
this is too dangerous, kama hali ndio hii tuna kazi kubwa sana, hata rais anaekuja atakuwa na utawala wa shida mno kutokana mfumo mzima wa kiuchumi ambao serikali imeharibu. corruption, abuse of power, misusing and mis-management of resources. too much to carry! watu inabidi wajue wapi tulipo, nani kasababisha, na maamuzi magumu tunayopaswa kufanya.
 
huyu jamaa akishughulikia tatizo la umeme litamsaidia kuongeza uzalishaji...
eti mnasema ni economist...... du udsm kazi ipo

Hapo Penya Blue ndo umenikera...UKILAZA wa mtu mmoja unahukumu Jumuia nzima????? Hata Lipumba alisoma pale.....nami pia na wengineo wengi tu humu Jamvini tumesoma pale lakini sio Vilaza....Muhukumu yeye kama yeye...UDSM imetoa vichwa vingi tu sema hawana urafiki au ufamily friend na JK thus y hawajapata chance kundini...
 
Si rahisi kutokukopa kabisa kama nchi, (almost imposible)

Issue ni kutafuta mkopo nafuu ambao hauna (compounded interest kama wa IFM, WB)

I totally agree with you. This strategy can be part of the solution. Now who should implement it? JK & Co! They are failing us big time.
 
Si rahisi kutokukopa kabisa kama nchi, (almost imposible)

Issue ni kutafuta mkopo nafuu ambao hauna (compounded interest kama wa IFM, WB)

Kwa nini usiwaelekeze ccm wakakope huko unakosema?
 
Mikopo kwa ajili ya matumizi tena ya kawaida na ambayo hayana tija kwa taifa ndo lizigo lenyewe tunalobebeshwa. PM anazira VX V8, anafikiri inamsaidia mkulima wa kijijini kwake! CCM imetumia 50 bln kuturudishia huyu mt Magogoni, sina hakika kama pesa yote imetokana na mapato ya chama.

Mkuu wa nchi na safari lukuki nje ya nchi na wapambe wa kutosha sijui ni nini kama taifa tumevuna ktk hilo.

Anyway hata mbuyu ulianza kama mchicha, hasira ya watu kuna siku itafika huko, ndipo tutajua ni nini maamuzi yao
 
hapa kuna tatizo tena kubwa sana, yanaani serikali inatumia zaidi ya inachoingiza...this is a big mess.Hii nchi sijui inakoelekea ni wapi, sioni kinachofanyika ninini? hivi JK anajua anachokifanya kweli kweli?

Jamani kuna uwezekano tukawa tuna mlaumu bure kumbe jamaa ni mgonjwa au ana matatizo mengine tu ya kutoelewa hali halisi ya maisha ya wananchi wake.

Haiiingii akilini kila kitu kimepanda maradufu huku mishahar ikiwa hapo hapo, matumizi bado makubwa sana, mishahar minono ya vigogo huku watu wakifa na njaa..duh hapa ni maombi tu hakuna la ziada
 
Back
Top Bottom