Demu anahisi kuwa Mama yamgu Hampendi

Freddy81

Member
Feb 3, 2009
99
3
Jaman mi mwenzenu demu anahisi kuwa hapendwi na mama mkwe, so nataka nimwondolee hiyo fikra katika akili zake, ni njia gani ambayo mnaweza kunishauri waungwana? Nahitaji sana maoni yenu
 
Ni kumuhakikishia tu kwamba Mama Mkwe hana matatizo naye, na labda kumwambia Mama aonyeshe upendo na furaha kwa shemeji yetu.
 
Jaman mi mwenzenu demu anahisi kuwa hapendwi na mama mkwe, so nataka nimwondolee hiyo fikra katika akili zake, ni njia gani ambayo mnaweza kunishauri waungwana? Nahitaji sana maoni yenu

...Kwanza nikuulize, huyo demu yeye mwenyewe anampenda mama mkwe?

Ni kumuhakikishia tu kwamba Mama Mkwe hana matatizo naye, na labda kumwambia Mama aonyeshe upendo na furaha kwa shemeji yetu.

...wrong bro, wrong! huwezi kumlazimisha mtu ampende/kumwonyesha furaha binadamu mwingine. These things comes natural...

Mama zetu hawakurupuki tu "kuwa-doubt" hawa wenzetu.
 
Jaman mi mwenzenu demu anahisi kuwa hapendwi na mama mkwe, so nataka nimwondolee hiyo fikra katika akili zake, ni njia gani ambayo mnaweza kunishauri waungwana? Nahitaji sana maoni yenu

Mkuu usilogwe kabisaaa!! wacha nature i-take njia yake.

Huyo dada kwanza atakuwa na matatizo, utaanzaje kusema eti mama mkwe hakupendi, kwani yeye anataka aolewe na mama mkwe?? Yeye msichana anafanya juhudi gani kuhakikisha mama mkwe anampenda?

Hao ndio vishetani vinavyoingia kwenye familia na kuanza kuvuruga na kuvunja undugu/mahusiano. Anataka wewe ugombane na mama yako?

Kaka yangu zinduka, mchunguze vizuri huyo dada, wewe umeishi na mama yako na unamfahamu vizuri sana. Unaweza ukaisoma dhamira ya mama yako. Kama ni kweli mama yako hampendi demu wako basi jua kunako issue kwa huyo mpenzi wako. Usichukulie mambo juu juu. Kaa na mama akupe mtazamo wake, unaweza ukaushukua ushauri wake au ukauacha lakini utakuwa umeelewa kinachoendelea, na itakusaidia jinsi ya kuishi na demu wako.

Vinginevyo kama umezimika sana basi we endelea na mpenzi wako na umwambie asiangalie mama mkwe anampenda au lah, ila hiyo haifai. Lazima mpate baraka toka kwa wazazi.

Mama kutompenda mkwewe mara nyingi inatokea kama wewe kaka upo karibu sana na mama yako. Mvutano utakuwepo. Kinachotakiwa huyo binti ajue jinsi ya kum-treat mama mkwe. Hao wamama wanachohitaji ni heshima kidogo tu, umjali kama amekuzalia chema, BASII, na urafiki utakuwepo.
 
Back
Top Bottom