Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 39,996
Niliandika juu ya DECI kwa kirefu tarehe 14 January mara baada ya kupata taarifa ya uwepo wa shirika hilo na nikaonesha kwa kirefu jinsi gani litaporomoka. Nikatoa mapendekezo ya kutosha ya hatua gani zichukuliwe nikiamini kabisa kwa kuingilia kati mara moja jambo hilo lingeweza kuepusha hatari iliyo mbele yetu.
Jambo hili lilipoibuliwa tena na vyombo vya habari wiki hizi chache zilizopita sisi "Cheche" tuliandika kwa kirefu juu ya DECI na kuelezea ni kwanini mchezo huu ni hatari. Tulionesha (kama walivyofanya wengine vile vile) kuwa DECI kimsingi ni mchezo wa ulaghai wa fedha (financial fraud). Licha ya ukweli wa DECI kujulikana kwa muda mrefu (haiwezekani isijulikane hadi watu karibu nusu milioni wanajiunga!) serikali imekuwa legelege na inayofanya mambo kama haina akili nzuri.
Ilipotoka makala yetu ya wiki iliyopita pamoja na makala zilizotoka kwenye Tanzania Daima na MwanaHalisi ambazo tumejitahidi kuzipush ili kuliamsha taifa bado jambo hili linaonekana bado linaleta ukungu mbele yetu. Ninavyoandika leo moyo wangu ni mzito kwa sababu leo asubuhi nimepata email moja ambayo naiweka hapa jinsi ilivyo ya mmoja watu ambao watakuwa wameathirika na uamuzi wa kuifungia DECI.
Sakata hili la DECI linaendelea kuthibitisha mambo ambayo nimeyavalia njuga kwa muda:
a. Usalama wa Taifa (namaanisha uongozi wake) una matatizo makubwa mno kiasi cha kuruhusu wizi huu kutokea mbele ya macho yao. Taasisi yao ya Intelligensia pamojana taasisi ya Inteligensia ya mambo ya fedha (FIS) wanaendelea kuthibitisha kuwa hawana uwezo wa kusimamia fedha zetu. Baada ya yaliyotokea Benki Kuu nilitarajia labda wataamka lakini bado wamelala kama pono!
b. Jeshi la Polisi bado halina uwezo (kiuongozi na kimkakati) kuzuia uhalifu kama huu wa kifedha. Inapofikia Jeshi la Polisi linatoa ulinzi wakati mwizi anaiba basi jeshi hilo linapoteza sifa ya kuwa msimamizi wa usalama wa "raia na mali zao". Inachekesha (kwa kuudhi) kuwa Jeshi la Polisi limekuwa washirika wa wizi huu halafu wao wenyewe ndiyo wanatakiwa kusimamia kuchunguza. Hii inanikumbusha tukio la vifo vya watoto Tabora ambapo Jeshi hilo likijua ubovu wa jengo lile na matukio ambayo yalitokea pale kabla likaitwa kushiriki uchunguzi wa jambo ambalo wao wenyewe walitakiwa wachunguzwe! Kila kitu tunafanya kinyume nyume.
c. Endapo vurugu zitatokea nchini (kama email hii inavyoashiria) kama ilivyotokea kule Albania 1996 basi kuna viongozi ambao barua zao za kujiuzulul zinatakiwa kuwa mezani mara moja kwani ni ushahidi wa kushindwa kwao kuongoza. Viongozi hao kwa haraka ni Waziri wa Mambo ya Ndani (ambaye sielewi kwanini bado ni Waziri!), Mkuu wa Jeshi la Polisi na Mkuu wa Usalama wa Taifa ambaye kwa kila kipimo ameshindwa kulinda usalama wa Taifa au kukusanya taarifa za kijasusi ambazo zingeweza kuzuia upuuzi huu unaoendelea nchini.
d. Waziri Mkuu ambaye ana matatizo ya kufuata utawala wa sheria ajiandae yeye mwenyewe kuwajibika endapo damu itamwagika nchini kutokana uzembe na usimamizi mbaya wa serikali. Kauli yake kuhusu DECI inaendelea kuthibitisha ni jinsi gani bado Tanzania hatuelewi kitu kinachoitwa "the tyranny of the law" au wakati mwingine kinajulikana kama "the dictatorship of the law". Bado tunafanya mambo kana kwamba sheria is optional!
Well email yenyewe:
Ninachosema ni kuwa, mapendekezo yetu yaliyoko kwenye "Cheche" toleo la wiki hii ndiyo njia pekee ya kunusuru machafuko nchini. Vinginevyo, kutokana na uzembe wa watu wachache, tujiandae kulipa gharama kubwa, gharama ambayo CCM isiithubutishe.

Mwanakijiji, mimi sikufahamu, lakini nimelazimika kukuandikia ujumbe huu mfupi, maelezo uliyoyaeleza kwenye barua kwenye gazeti la mwana halisi, ulichoeleza ni muhimu watu wajue kuwa ukoloni mambo leo umepitwa na wakati, vitisho vimepitwa na wakati, wakoloni walichokiacha ndicho kinachoendelea mpaka leo.
Maana yake mtanzania hatakuwa huru mpaka pale atakapofunguliwa macho aone, wakati huyu mheshimiwa aitwae kipenzi cha watanzania, kikwete, alisema maisha bora kwa kila mtanzania, lakini hatufichi hakuna kilichofanyika, watanzania wana hali mbaya kuliko kawaida, wamenyanga'nywa mali zao nyumba zao, baada ya kukopeshwa na taasisi za fedha, pride, finca, na zingine za aina hiyo.
Ikainuka Deci, iliyotusaidia sana walala hoi, na sasa unasikia ilivyoendelea kuambiwa ni upatu, sasa mwisho wa mambo haya hatujajua nini kitatokea, ila waambie wazi c.c.m. Mwisho wake ndio huo, imetudanganya inatosha, sasa wananchi wanasema liwalo na liwe, hatuwezi kukubali
kupoteza fedha zetu kijinga, wakati serkali yetu ilitoa leseni, sawa hawakufanya ilivyotakiwa, walikuwa wapi?
Tukisema kuwa serkali ya c.c.m. Imetuibia ni sawa. Nalosema mwakani haiwezi kurudi madarakani. Tumeamua, wanachana lak 7. Na wale walionyuma yetu jumla ni m.3. Kama c.c.m. Inataka mioyo yetu irejee watupe hela zetu, kinyume chake. C.c.m. Kwa heri, haitarudi madarakani tena.
Jambo jipya laja. Waambie, waandikie, wameshindwa kuwabana mafisadi walioiba mabilioni, leo wananyang'anya walala hoi vimtaji vyao walivyowekeza Deci. Ok. Inzi kufia kwenye kidonda ni halali yake, jambo laja, hatutanyamaza, nasema jambo laja. Laja. Laja. Asante, sipendi jina langu litajwe, ila mambo ndio hayo. Damu yamwagika nchini. Oh.