DC Jokate awataka wafanyabiashara wanaoficha mafuta kuacha mara moja

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
DC JOKATE AWATAKA WAFANYABIASHARA WANAOFICHA MAFUTA KUACHA MARA MOJA - KOROGWE

Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga, Jokate Mwegelo amewataka Wafanyabiashara wanaoficha mafuta Wilayani Korogwe wakisubiria mabadiliko ya bei ili wauze kwa bei kubwa kuacha mara moja kwakuwa wanahujumu uchumi na kuichafua Serikali.

DC Jokate amesema hayo leo July 31, 2023 baada ya kutembelea Kituo cha Mafuta Mombo High Way ambacho hakijafanya kazi kwa siku ya tatu leo kwa kisingizio kuwa pump imeharibika “Kuna maeneo tunajua kuna changamoto lakini hapa mafuta mnayo leo siku ya tatu Wananchi hawapti hudumu hii haikubaliki"

 
Back
Top Bottom