DC-Hai Acha kuingilia taaluma ya ualimu

Kimetah

JF-Expert Member
May 8, 2013
1,049
188
Baada ya dc-hai ndugu Byakanwa kunukuliwa katika mahojiano na clouds FM wakati akijitetea kuhusu swala la kumweka ndani mwalimu,japo hakusema SABABU za kumweka mwalimu ndani,alisikika akisema ametunga mitihani kwaajili ya kidato cha nne.

Katika kufatilia kauli hiyo mambo yafuatayo yamebainika.
1.Katika kikao chake na ofisi ya afisa elimu wilaya,walimu wa taaluma na wakuu wa shule uliofanyika mwezi wa nne mwaka huu(april 2017) katika shule ya sekondari Hai,aliwaeleza kwamba watafute mitihani ya necta ya miaka iliyopita kuanzaia mwaka 2010 mpaka 2016 na kisha atachagua mitihani kati ya hiyo na ndio itakiwa kipimo cha kuwaandaa wanafinzi.
Alisisitiza kuwa mitihani hiyo itafanyika kama ulivyotungwa na necta bila kubadili hata nukta.


2.Mwezi wa sita 2017(june 2017) ratiba ilikuja na kuonyesha kila mwisho wa mwezi wa 7,8 na 9 itafanyika mitihani aliyoagiza iwepo.Na kika shule ifanye yafuatayo.
A.kuwa na mitihani hiyo.
B.kupiga copy ya mtihani utakaoagizwa na ofisi ya elimu wilaya kwa idadi ya wanafunzi alionao shuleni.
C.kuagiza wanafunzi waje na daftari dogo kwaajili ya kujibia mitihani hiyo.
Yaani kila mtihani ujibiwe kwenye daftari moja,hivyo wazazi wanajukumu la kununua madaftari ya kila mtihani wa mwezi husika.
D.Walimu wanajukumu la kusimamia mtihani huo kama moja ya majukumu yao.
E.Mtihani ukimalizika ukusanywe kwny kasiki/chumba madhubuti ili kusubiri utaratibu wa kusahihisha.

Baada ya kuanza kufanyika kwa mtihani hiyo,mwezi wa7 ukamalizika,mtihami wa pili wa mwez wa8 kabla ya kuanza wanafunzi walihoji.
WANATAKA MATOKEO YA MTIHANI WA KWANZA WA MWEZI WA SABA.
PIA
BAADHI YAO WALILALAMIKA KUTOWEZA KUPATA DAFTARI DOGO LA KUANDIKIA MTIHANI WA PILI WA MWEZ8 KWAN WAZAZI WAMEKATAA KUWAPA HELA YA KUNUNUA MADAFTARI TENA..

Upande wa waalimu walihoji.
Iweje mtihani mmoja umeisha alafu mtoto anapewa mtihani mwingine pasipo kupewa matokeo ya mtihani wa kwanza?
Taaluma ya ualimu inamtaka mwalimu atoe matokeo ya mtihani kabla ya mtihani mwingine kuanza ili mtoto ajue alipokosea kwa mwalimu kufanya masahihisho.

Baada ya maswali mengi kutoka kwa waalim na wanafunzi,ushawishi ilitumika na hatimaye mtihan wa pili wa mwez wa8 ulifanyika na kimalizika.

Mpaka shule zinafungwa tar.30/08/2017 hakuna utaratibu wowote wa kusahihisha mitihani hiyo uliotolewa.

Wadau wa elimu wanahoji.
1.Je mitihani hiyo inayofanyika bila wanafunzi kupewa majibu na masahihisho kufanywa na waalim,Inafaida gani kwa wanafunzi?

2.Huu utaratibu wa kukaririsha wanafunzi maswali,kwa kuwapa maswal ya miaka iliyopita kama yalivyo,unajenga wataalamu wa namna gani?

3.Je waalim wa Hai wanashindwa kutunga mtihani wa wilaya mpaka uamuzi wa kuchagua mitihan ya necta utumike na kupiga copy kama ulivyo kulingana na idadi ya wanafunzi?

4.Shule inato wapi gharama za kutoa copy ya mitihani yote,ilihali gharama hizo hazipo kwny fungu lolote linaloletwa na serikal katika shule?

5.Walimu watatoa jibu gani kwa wanafunzi watakapo hitaji matokeo ya mtihani wa kwanza na wa pili kabla ya mtihani wa 3 mwezi wa9?.


DC-Hai acha kuingilia taaluma ya ualimu


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom