DC amkwida diwani katika chakula

OSOKONI

JF-Expert Member
Oct 20, 2011
10,965
5,336
Shija Felician, Kahama
MKUU wa Wilaya ya Kahama, Benson Mpesya, juzi alimkwida na kumuondoa katika mstari wa viongozi kwenda kupata chakula, Diwani wa Kata ya Nyihogo (Chadema), Amos Sipemba.

Chakula hicho kilikuwa maalum kwa msafara wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Katika tukio hilo lililotokea wakati wa chakula cha mchana katika viwanja vya nyumba ya mapumziko alipokuwa amefikia waziri mkuu, Mpesya alianza kuwakaribisha wageni wa kimkoa kutangulia kupata chakula, huku akiwataka baadhi ya viongozi wa wawakilishi wa wananchi ,kuungana na msafara huo.

Mkuu huyo wa wilaya ambaye alionekana kuwa makini zaidi na ugeni huo, akiwa mara yake ya kwanza kupokea ugeni wa kitaifa tangu aipoteuliwa miezi minne iliyopita, alisimamia ugawaji wa chakula kwa wageni na wenyeji waliokuwa katika msafara huo.

Baada ya kumaliza kutangaza wageni wa kimkoa, aliwachagua Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Kahama, Machibya Jidulamabambasi na makamu wake, Lucas Makulumo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya wa Kahama, Alfred Mahanganya na makamu wake Mibako Mabubu.

Hali kadhalika Diwani wa Kahama Mjini ili waungane na msafara huo katika upata chakula.


Diwani Sipemba akiwa na mwenzake wa Kata ya Mwendakulima (TLP), Ntabo Majabi nao walijipachika kwenye mstari wakiwa nyuma ya Diwani wa Kata ya Kahama Mjini, Abasi Omari, ambaye Mpesya alimtaka ajumuike na ugeni kutoka mkoani.

Lakini alipoona Sipemba yuko mstarini, mkuu huyo wa wilaya alikwenda na kumtaka asiingie kwenye mstari lakini diwani huyo alikaidi amri.

Kitendo hicho kilimfanya Mpesya ampige jeki kwa nyuma kwa kutumia mkanda wa suruali aliyokuwa amevaa (diwani) na kumnyanyua mithili ya mhalifu.

Hatua hiyo ilimwezesha kiongozi huyo kufanikiwa kumuondoa diwani huyo kwenye mstari wa wageni na kumrejesha nyuma ambako alidakwa na askari polisi waliokuwa wakilinda usalama katika eneo hilo.

Hata hivyo baadhiya madiwani walilalamikia kitendo hicho walichokielezea kuwa ni cha udhalilishwa kwa mwenzao hasa baada ya kubaini kuwa diwani mwenzie wa TLP aliyeingia naye kwenye mstari, aliachwa mstarini.

Baada ya malalamiko hayo, mkuu wa wilaya alikwenda tena kwenye mstari wa wageni wa kimkoa na kumtaka diwani aliyekuwa amebaki kwenye mstari, atoke na alifanya hivyo.

Alisikika akisema mara nyingi madiwani wamekuwa wakivuruga itifaki katika misafara ya wageni wa kitaifa na kwamba sasa lazima waheshimu na kufuata taratibu.

Hata hivyo wakati ugawaji chakula ukiendelea mkuu huyo, alimfuata diwani huyo na kumnasua kutoka kwenye mikono ya polisi waliokuwa wamemshikilia.

Alimpeleka ndani ya ukumbi na kumuinganisha na wageni katika kupata chakula, jambo ambalo watu walilitafsiri kuwa ni kujisafisha baada ya kumdhalilisha diwani.
 
Siungi mkono viongozi wa chadema hata kama ni madiwani na wabunge kula vyakula kwenye hafla yoyote inayohusiana na viongozi wa serikali ya ccm. Watakupata wapi kama siyo kwenye chakula? Kwa siku moja tu hutokufa njaa.
 
hivi chakula huko Kahama ni adimu sana ??

Nashauri hii tabia ya kupanga foleni ife hasa kwa upande wa kupata chakula na Mpesya tafadhari sana usituaibishe watu wa Mbeya hasira za kubwagwa na Sugu usizihamishie Kahama
 
Elimu haisaidii. Mpesya ni kama hana elimu ya kujua vitu. Wanatumia sana muda huu kudhalilisha wanachama na viongozi wa CDM.

Shida ni vyeo vya kupeana.
 
Licha ya kudhalilishwa vibaya, hata yeye amejidhalilisha sana!
 
Siungi mkono viongozi wa chadema hata kama ni madiwani na wabunge kula vyakula kwenye hafla yoyote inayohusiana na viongozi wa serikali ya ccm. Watakupata wapi kama siyo kwenye chakula? Kwa siku moja tu hutokufa njaa.
huu ni mwanzo wa kupewa hata sumu

kama walivyo isusia TBC wasusie vivyo hivyo chakula na hawa watu. Ni lazima kufika mahali kubaini ni yupi adui na yupi rafiki wako
 
Diwani alivunja utaratibu. Kuna itifaki alikuwa akiifanya mkuu wa wilaya hivyo diwani angesubiri wakati wake ufike. Inakuwa kama waligombea chakula!
 
huyu diwani nae sijui njaa yani baada ya kudhalilishwa na kukwidwa kama mhalifu na kukabidhiwa kwa polisi anarudishwa ndani kula nae anaenda? kuonyesha ujasiri alitakiwa aende nyumbani moja kwa moja!!

Vyakula vyakula vyakula! Mtu unakwidwa lakini bado tu upo utadhani ndio chakula chako cha mwisho kabla hujanyongwa. Khaaa.
 
Diwani alivunja utaratibu. Kuna itifaki alikuwa akiifanya mkuu wa wilaya hivyo diwani angesubiri wakati wake ufike. Inakuwa kama waligombea chakula!

Nakubaliana nawe mkuu. Hakuna cha kunyanyaswa kwa CDM hapa. Diwani alivunja ITFAKI kwa "KUCHOMEKEA"
 
Vyakula vyakula vyakula! Mtu unakwidwa lakini bado tu upo utadhani ndio chakula chako cha mwisho kabla hujanyongwa. Khaaa.

Vyakua vya kwenye mkusanyiko vinaturusha sana akili sisi waswahili! Hii ndiyo mfano hai wa kwanini hadi leo Tanzania chakula kinatumika kama moja wapo ya rushwa katika chaguzi zetu!

Juzi juzi nilisikia mmoja wa wabunge wetu washika Bastola aliwapatia wananchi vitumbua katika kutafuta kura zao...,Tunaendekeza saana njaa; na tunaadhirika kwa sababu hiyo!
 
Back
Top Bottom