Ogende ogaruke na Shuntama

Superman

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
5,695
1,696
Nimewahi kusikia miaka ya nyuma kuwa kuna dawa za mapenzi za kihaya moja inaitwa UGENDE UGARUKE nyingine SHUNTAMA ambazo akina dada huwa wanatumia kuwapumbaza Wanaume kimapenzi ili wawapende sana.

Kwa wale walio na uelewa wowote wa mambo haya, je kuna ukweli wowote au ushuhuda? Au ni hadithi za hekaya za Abunuasi?

Nawakilisha.
 
Nimwahi kusikia miaka ya nyuma kuwa kuna dawa za mapenzi za kihaya moja inaitwa UGENDE UGARUKE nyingine SHUNTAMA ambazo akina dada huwa wanatumia kuwapumbaza Wanaume kimapenzi ili wawapende sana.

Kwa wale walio na uelewa wowote wa mambo haya, je kuna ukweli wowote au ushuhuda? Au ni hadithi za hekaya za Abunuasi?

Nawakilisha.

UGENDE-UGARUKE...Yaani utaenda...na utarudi mwenyewe, bila kulazimishwa!...ha..ha..haaa!
Nadhani dawa hiyo ni mbaya sana, kwa mwanandoa simshauri akae jirani nayo...lol!
 
UGENDE-UGARUKE...Yaani utaenda...na utarudi mwenyewe, bila kulazimishwa!...ha..ha..haaa!

Nadhani dawa hiyo ni mbaya sana, kwa mwanandoa simshauri akae jirani hayo...lol!

Du! Mkuu ndo unanifungua macho sasa.

Ina maana ukipewa hiyo wewe lazima utakuwa unarudi tu kwa huyo Dada aliyekupa. Ama?
 
Asa kuna faida gani kuwa na mtu ambaye unajua kabisa penzi lake kwako limepigwa jeki na hayo madudu?

Is it part of mapenzi au? kaazi kweri kweri
 
Kiboko ya zote inaitwa "tanaka",ukilambishwa hiyo ndugu zako wote unawaona kama kituo cha Polisi!
 
MJ1 ukishakuwa mhanga wa hayo 'madudu' huwezi kujua maana sasa si utakuwa unapelekeshwa tu kama mkweche unaovutwa na brekidauni?
 
Du! Mkuu ndo unanifungua macho sasa.

Ina maana ukipewa hiyo wewe lazima utakuwa unarudi tu kwa huyo Dada aliyekupa. Ama?

Huwezi mkwepa kaka!...Utajizungusha siku mbili tatu, lakini wapi, utaona yeye ndo nambari wani! Yeye hata ukimtukana wala hachukii, anajua huna option zaidi ya kumrudia!

Ni soo hizo dawa babaake! Ama kweli Mungu aliumba mimea ya ajabu sana, maana hii ni mimiea pyua, haichanganywi na kitu wala ndumba yoyote...lol!
 
Mambo mengine kujitafutia matatizo, inakuwaje wewe ukimchoka na yeye kawa king'ang'anizi kwa ajili ya hayo madude si utatamani ufukiwe ardhini.
 
Nami ndo kwanza leo kusikia hayo ya miti huku kwetu tuna kinyama kidogo cha ngombe au chochote kinavumbikwa ktk uchi wa mwanamke na kulishwa kazi yake ndo km hiyo kinaitwa limbwata.
 
Ya nini kuishi na mtu aliye pumbaa akili?? kama hawezekaniki bora kuachana nae.

Kuna binti mmoja alikwenda kwa wataalamu wa hayo mambo akaulizwa anachotaka akasema anataka mumewe asitoke nje, jamaa akawa hatoki nje kabisa literally yaani hata kazini kagoma kwenda, we...ilikuwa shughuli kwelikweli!
 
MWE! nAKUMBUKA KUNA JAMAA KAWEKEWA DAWA KWENYE MAJI YA KUOGA NA MKEWE kwenye ndoo, jamaa alizoea kuoga ikitumia kikombe kujimwagia maji mwilini, yaani ile anajimwagia tu! mkewe alimshuhudia nyoka akitoka bafuni huku kichwa ni cha mmewe, lakini kiwiliwili cha nyoka! ilibidi apigwe risasi maana hakikuwa kiumbe cha kawaida tena! Mungu atunusuru na hawa viumbe wa kike!
 
Huwezi mkwepa kaka!...Utajizungusha siku mbili tatu, lakini wapi, utaona yeye ndo nambari wani! Yeye hata ukimtukana wala hachukii, anajua huna option zaidi ya kumrudia!

Ni soo hizo dawa babaake! Ama kweli Mungu aliumba mimea ya ajabu sana, maana hii ni mimiea pyua, haichanganywi na kitu wala ndumba yoyote...lol!

Kaka huo mmea unapatikana vipi na unaitwaje?

Ni uchawi au ni sayansi ya tiba?
 
Hakuna dawa ya mapenzi duniani, utamwua mwenzi wako bure! Dawa ya mapenzi ni hii: Usiwe mchoyo, mwizi, mzinzi, mlevi, mfitini,

Ukiwa mchoyo hutataka mwenzi wako ajue kipato na matumizi yako, unamdhurumu, utafanya maisha yawe ya mashaka mashaka.

Ulevi kupita kiasi unakupelekea uzinzi. Ukiwa ulevini lazima utanunua uzinzi, na kwa kuwa mkeo hajui pato na matumizi yako, hivyo lazima shetani atakusaidia badala ya mkeo.

Hapo ndipo ndoa inakuwa ndoana.
 
Hizi sio hadithi za hekaya ni mambo ambayo yapo kabisa in reality na yana mifano hai. kama unaamini kuwa kuna limbwata basi ndio shuntama yenyewe
 
nami ndo kwanza leo kusikia hayo ya miti huku kwetu tuna kinyama kidogo cha ngombe au chochote kinavumbikwa ktk uchi wa mwanamke na kulishwa kazi yake ndo km hiyo kinaitwa limbwata.
Du, Mkuu Yussuf kumbe neno 'limbwata' maana yake ni jina la mnyama? mmmhhh wanaume tunakula mengi!
 
Nimwahi kusikia miaka ya nyuma kuwa kuna dawa za mapenzi za kihaya moja inaitwa UGENDE UGARUKE nyingine SHUNTAMA ambazo akina dada huwa wanatumia kuwapumbaza Wanaume kimapenzi ili wawapende sana.

Kwa wale walio na uelewa wowote wa mambo haya, je kuna ukweli wowote au ushuhuda? Au ni hadithi za hekaya za Abunuasi?

Nawakilisha.

Duu hayo majina yamenikumbusha mbali kidogo..Nadhani hiyo lugha ni ya nchi jirani!!
 
Back
Top Bottom