Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,318
- 33,125
WATU wengi wamekuwa wakisumbuliwa na ugonjwa wa Amoeba lakini hupuuzia pale dalili zinapoanza, ni ugonjwa mbaya ambao ukikaa sana tumboni husababisha madhara makubwa , kama kuhara damu kupindukia, kutapika, kusikia kizunguzungu, kukosa hamu ya kula na kupata homa kali.
Ugonjwa huu mara nyingi husababishwa na maji na vyakula jamii ya mbogamboga kama hutakuwa umesafisha vizuri.
Dalili za ugonjwa ni pamoja na tumbo kujaa na kukata kwa vipindi fulani, mtu akienda kujisaidia mara nyingi huishia kujikamua sana na akipata choo huwa hajisikii kumaliza.
Hizo ni baadhi ya dalili ila zipo nyingi lakini usitumie dawa mpaka utakapogundua kwa kupima kwani dawa nzuri inanywewa pale mtu anapogundua ana tatizo gani.
Tiba asilia ya Amoeba
Majani ya mpera
Tiba asilia inayotumika kumaliza kabisa tatizo hili ni pamoja na majani ya mpera, unayachukua na kuyakamua kwenye maji masafi ya kunywa ukiwa umeshayaosha vizuri kisha unakunywa nusu kikombe kwa siku mara tatu kwa siku tatu mfululizo.
Kitunguu swaumu
Chukua kitunguu swaumu punje tano menya kisha viweke ndani ya nusu lita ya maji safi na salama, changanya na maji ya limao moja chemsha mpaka maji yapungue, usisahau kuweka chumvi kidogo kwa ajili ya kupata ladha.
Ukishatengeneza kinywaji hicho unaweza kunywa kila siku glasi moja.
Ni tiba nzuri isiyo na madhara kwa mgonjwa.