David Kafulila: Tume inataka kunihujumu Kigoma Kusini

Aisatu

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
775
321
DAVID KAFULILA

TUME INATAKA KUNIHUJUMU KIGOMA KUSINI.

Kwanza Mkuu wa Mkoa Kigoma Kanali Issa Machibya na Mkuu wa Wilaya Mrisho Gambo walifanya kampeni kubwa na vitisho kwa wananchi wakitumia polisi.

Pamoja na hujuma zote hizo bado majumuisho kwa fomu za mawakala nimeongoza kwa kura 2435.

Kwa kujua hilo jana mgombea wa ccm Hasna Mwilima amekuja kukataa matokeo ya baadhi ya kata na kutaka zihesabiwe upya. Nikakataa kwa nguvu zote na nikamuonya msimamizi ache kupokea maelekezo ya Mkuu wa Mkoa.

Msimamizi akamua kusitisha zoezi la majumuisho na kwamba anamwandikia barua Mkurugenzi wa uchaguzi taifa kwa mwongozo.

Msingi wa kukataa kuhesabu upya matokeo ni ukweli kwamba fomu za mawakala tunazo na hazina kasoro.ccm hawana fomu za mawakala wao.

Lakini sababu ya pili sina imani na masanduku kwamba hayajachakachuliwa kwani tangu baada ya kupiga kura yalikuwa chini ya polisi na tume wenyewe bila wakala. Na hili linakuwa na uzito kwasababu ya taarifa za magari ya kura feki yaloingizwa chini ya usimamizi wa mkuu wa mkoa na wilaya

Msimamo wangu ni kwamba sipo tayar kufungua masanduku na kuhesabu upya ni bora msimamizi akili ameshindwa kusimamia zoezi na uchaguzi ufutwe kuliko kuhesabu masanduku ambayo sina hakika nayo.

Naomba umma ujue haya kwa ufafanuzi wa kinachoendelea kwani mpaka sasa wamejaza polisi eneo hili kiasi cha kutisha.

Tulianza na Mungu na Hakika tunamaliza na Mungu.

David Kafulila
 
Yaani ccm akili zenu sijui ziko wapi ,KAFULILA ANGEGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KONGWA KWA NDUGAI ,BADO KAFULILA ANGESHINDA SEMBUSE JIMBONI KWAKE KIGOMA ....HUYO MWAMBA ALIANGUSHA BAADHI YA MAWAZIRI NA MWANASHERIA MKUU NDIO IJE KUA HUYO MGOMBEA MWENZAKE NA HAO SIJUI WAKUU WA WILAYA
 
CCM wanaiba na kuchakachua kura, kwa kuingiza mabox mengine ktk vituo...ENDAPO UTAKUBALI TU KURA KURUDIWA KUHESABIWA KWA KUPITIA MASANDUKU... utaanguka, sbb wanabaki na yale masanduku Mkuu wa Mkoa na bwana halmashauri, kisha wanaingiza kura mpya... so UKIKUBALI TU KURUDIA KUHESABU KURA KWA KUPITIA MABOX utaanguka vibaya kama WENJE... kubali kurudia mahesabu KUFUATA FOMU ZA MATOKEO ambazo tayari zina matokeo halali... sio kurudia mabox...!!! WENJE ALIANGUKA KWA NJIA HIYO...!!!! PIA KIWIA wa Ilemela alianguka kwa njia hiyo ya kuhesabu mabox kwa mara ya pili...!!!!

So, kama unarudia kuhesabu, TUMIENI MATOKEO YA FOMU KURUDIA MAHESABU...!!!!

CCM ndio njia kuu hii wanatumia kuiba kura...!!!
 
DAVID KAFULILA

TUME INATAKA KUNIHUJUMU KIGOMA KUSINI.

Kwanza Mkuu wa Mkoa Kigoma Kanali Issa Machibya na Mkuu wa Wilaya Mrisho Gambo walifanya kampeni kubwa na vitisho kwa wananchi wakitumia polisi.

Pamoja na hujuma zote hizo bado majumuisho kwa fomu za mawakala nimeongoza kwa kura 2435.

Kwa kujua hilo jana mgombea wa ccm Hasna Mwilima amekuja kukataa matokeo ya baadhi ya kata na kutaka zihesabiwe upya. Nikakataa kwa nguvu zote na nikamuonya msimamizi ache kupokea maelekezo ya Mkuu wa Mkoa.

Msimamizi akamua kusitisha zoezi la majumuisho na kwamba anamwandikia barua Mkurugenzi wa uchaguzi taifa kwa mwongozo.

Msingi wa kukataa kuhesabu upya matokeo ni ukweli kwamba fomu za mawakala tunazo na hazina kasoro.ccm hawana fomu za mawakala wao.

Lakini sababu ya pili sina imani na masanduku kwamba hayajachakachuliwa kwani tangu baada ya kupiga kura yalikuwa chini ya polisi na tume wenyewe bila wakala. Na hili linakuwa na uzito kwasababu ya taarifa za magari ya kura feki yaloingizwa chini ya usimamizi wa mkuu wa mkoa na wilaya

Msimamo wangu ni kwamba sipo tayar kufungua masanduku na kuhesabu upya ni bora msimamizi akili ameshindwa kusimamia zoezi na uchaguzi ufutwe kuliko kuhesabu masanduku ambayo sina hakika nayo.

Naomba umma ujue haya kwa ufafanuzi wa kinachoendelea kwani mpaka sasa wamejaza polisi eneo hili kiasi cha kutisha.

Tulianza na Mungu na Hakika tunamaliza na Mungu.

David Kafulila

Aache kulialia aachie tu jimbo ndivyo mambo yalivyo.

Lazima Zitto aheshimiwe.
 
david kafulila nakukumbuka kwenye kashfa ile iliyotingisha sana ulisimamia kile ulichoamini tumia uzoefu ule ule kujinasua hapo ulipokwama nakutakia kila la heri katika mapambano ,haya yaliyopo mbele yetu .
 
Kubali matokeo Kafulila afadhali ya nusu shari kuliko shari kamili,Filikunjombe yuko wapi leo?
 
ukipambana na pigwa ili umshinde, mgonge knock out!!! kura elfu 2 tofauti ni ndogo sana......
 
Kamanda komaa sana tuu!! usije kuthubutu kukubali kurudiwa juhesabu kura......kama wanataka warudie uchaguzi mzima!
 
Back
Top Bottom