DART Special Thread: Tunaomba Maoni Ushauri, Malalamiko, Pongezi na Mapendekezo kuhusu Mabasi ya Mwendokasi

Why from Kibaha to Gerezani I use 750/- and I can't do the same from Gerezani to Kibaha?
wewe bongo yoyo yaan utoke kibaha mpaka gerezani kwa 750 iyo mwendokasi ya wapi au ya china, nauli ya kibaha mpaka kimara ni 700 utoke kimara mpaka gerezan ni 750 jumla 1450
 
Mimi napenda kujua usanifu mnaotumia katika upanuzi WA hizi barabara, Mfano chang'ombe veta kwenda chang'ombe Kilwa road, hapa mixes traffic, barabara ya Magari mchanganyikomeweka njia Moja hii Sio sawa, Najua mnaangalia sana miundo mbinu yenu ila kwenye mixed traffic inabidi pia mfanye maboresho na muweke njia mbili kila upande!!
Hili tatizo nimeliangalia Kwenye michoro ila litasumbua sana Bora mlifanyie kazi mapema!! Barabara ya Tabata kwenda kinyerezi phase 5, shida ni hiyo hiyo, barabara ya Mikocheni kwenda kawe kutoka Morocco tatizo ni hilo Hilo Single lane mixed traffic hii haikubaliki!! Lifanyieni kazi ni shida kubwa mtasababisha mbeleni
Hakuna mixed traffic, nenda huko chang'ombe - veta utaona mabasi yana njia yake hayatochanganyika na gari za kawaida
 
Hakuna mixed traffic, nenda huko chang'ombe - veta utaona mabasi yana njia yake hayatochanganyika na gari za kawaida
Usikimbilie kujibu kama hujaelewa, wenyewe wameelewa, mixed traffic ni wanaopita na Magari binafsi, na ujenzi ulivyo haya Magari Yana lane Moja tu, maana hakuna overtaking, Lori likiharibika utakesha unasubiri lipone!! Kwa nini wasiondoe tatizo kubwa linalokuja mbeleni Kwa kuweka barabara yenye kukidhi mahitaji ya watumiaji wote wa barabara!? Iliyokuwepo overtaking haikuwa shida pindi Lori likiharibika, Sasa nimegundua mpango huu upo kipande Cha Morocco to Kawe, Kigogo round about hadi kinyerezi kupitia Tabata dampo na Tabata, na kwingineko, ila Kwa Veta chang'ombe hadi Kilwa road, huu ujenzi Mbovu umeshatekelezwa na umeshaanza kero nyingi Kabla ya uzinduzi!! (Ambao hawakunielewa mixed traffic ni Magari mengine nje ya njia ya mwendokasi)
 
Huyu Dart kapewa za chembe, katelekeza uzi!
Kaanzisha uzi tarehe 17, kaja kuchungulia mara ya mwisho tarehe 18 kayoyoma!

Bila shaka atakuwa na Parody anaitumia kuchungulia huu uzi!!!
 
View attachment 2625074
DART Tumeanzisha ukurasa huu rasmi wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kwa lengo la kupata maoni, ushauri , mrejesho na hata malalamiko yanayohusu huduma zetu. Aidha tunawahakikishia watumiaji wa huduma zetu kuwa maoni, ushauri, malalamiko, Pamoja na hoja zenu juu ya huduma zetu yatafanyiwa kazi kwa uharaka na hatua stahiki zitachukuliwa ili kuboresha huduma.

Kwa kupata msaada wa haraka kuhusu huduma zetu unaweza kutupigia simu 0800110147 ni bure. Kuanzia saa 11 alfajiri hadi saa tano na nusu usiku

Pia unaweza kutufuatilia katika tovuti ya www.dart.go.tz na mitandao yetu ya kijamii ya Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka ya FACEBOOK, INSTAGRAM, TWITTER, LINKEDIN, YOUTUBE.

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

Anuani
S.L.P 724, 16103
Ubungo Maji, Morogoro Road
Dar es Salaam, Tanzania

Barua pepe: info@dart.go.tz.

#usafiri wa umma nadhifu

#mwendokasi app
mtu anakaa kituoni hadi masaa mawili, bus likija lipo nyomi abiria wanakimbilia kupanda kama nyumbu wa serengrti wakivuka mto mara. Tuige hata matatu za kenya kwenye ustaarabu wa kupanda bus, wekeni mabasi mengi mabasi yakiwa yanapita kwa muda mfupi mfupi hamna abiria atakayegombania bus! watanzania tunafeli mambo madogo sana shame on us!
 
Hongereni sana kwa kujiunga JF,

Maoni yangu/Malalamiko:-

Kuna tabia ambazo madereva wenu wanakera sana mpaka wanapoteza maana ya mwendokasi ,navyojua serikali haifanyi biashara zaidi ya kutoa huduma ,sasa kuna baadhi ya madereva wakishafika kwenye vituo vikuu(eg gerezani/morrocco/Ubungo) basi wanapaki magari wanaenda kukaa kupiga story wakati kuna abiria kibao wanasubiri magari.....Sijajua why wanafanya hivyo au utakuta wanaondoka tupu bila kubeba abiria.
Tunashukuru kwa kutupa kongole, wakati mwingine ukikutana na changamoto yoyote tupigie kwenye namba yetu ya bure ya 0800110147 ili waweze kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria , uwe na namba ya gari kituo ulichopo na muda ambao jambo hilo limetendeka.
 
Huyu Dart kapewa za chembe, katelekeza uzi!
Kaanzisha uzi tarehe 17, kaja kuchungulia mara ya mwisho tarehe 18 kayoyoma!

Bila shaka atakuwa na Parody anaitumia kuchungulia huu uzi!!!
Hakuna mtu aliyekimbia tupo humu kwa saa 24 , ndiomaana tumeanzisha huu uzi kwa ajili ya kupata feedback ya namna mambo yetu yanavyokwenda.
 
Jamani wazuieni haawa wanawake wanaopanda udart wakiwa wamevaa vicondom vyao wanatutamanisha kuwabambia tukiwa kwenye basi.
Suala la mavazi ni la kila mmoja na namna anavyoona linafaa na namna alivyolelewa hatuna mamlaka ya kuamuru abiria avae namna gani , sisi jukumu letu ni kuboresha usafiri wa umma katika mji wa Dar es Salaam na baadaye katika majiji mengine makubwa.
 
Sasa unaboreshaje usafiri wa umma kama ndani ya basi lako watu tunakuwa tumedimdisha? Usichukulie poa haya mambo au unataka mpaka siku nipigwe na mrembo kisa nimemchafualia nguo yake kwa kumbambia.
Mbona mna majibu mepesi kwenye mambo ya msingi nyie watu?
 
Kwanini ikifika saa tatu madereva wenu pale kivukoni wanapaki mabasi yanayoelekea kimara/mbezi na kupelekea msongamano mkubwa wa watu? Kwa kigezo cha kuwa wanaenda kunywa chai?
 
Pia ongezeni idadi ya mabasi wakati wa rush hours mida ya saa 12 jioni -2 usiku pale gerezani, yaani abiria wanakaa zaidi ya saa nzima kwenye foleni kusubiri usafiri. Kwakweli inachosha, inaboa na inapoteza muda.

Pia idadi ya mabasi kutoka kimara kuelekea gerezani/kivukoni/morocco haitoshi wakati wa asubuhi kuanzia saa 12 asubuhi mpaka saa 3 asubuhi ...msongamano wa watu ni mkubwa na magari ni machache
 
View attachment 2625074
DART Tumeanzisha ukurasa huu rasmi wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kwa lengo la kupata maoni, ushauri , mrejesho na hata malalamiko yanayohusu huduma zetu. Aidha tunawahakikishia watumiaji wa huduma zetu kuwa maoni, ushauri, malalamiko, Pamoja na hoja zenu juu ya huduma zetu yatafanyiwa kazi kwa uharaka na hatua stahiki zitachukuliwa ili kuboresha huduma.

Kwa kupata msaada wa haraka kuhusu huduma zetu unaweza kutupigia simu 0800110147 ni bure. Kuanzia saa 11 alfajiri hadi saa tano na nusu usiku

Pia unaweza kutufuatilia katika tovuti ya www.dart.go.tz na mitandao yetu ya kijamii ya Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka ya FACEBOOK, INSTAGRAM, TWITTER, LINKEDIN, YOUTUBE.

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

Anuani
S.L.P 724, 16103
Ubungo Maji, Morogoro Road
Dar es Salaam, Tanzania

Barua pepe: info@dart.go.tz.

#usafiri wa umma nadhifu

#mwendokasi app
USHAURI
1. Wakati tunafikiria kuondoa mabasi ya mikoani usiku kuna haja gani DART kuwa na ukomo wa muda wa kazi?
2. Kama 24hrs ni shida kwa nini msiwe na route ya saa tisa usiku from Kibaha - Gerezani?
3. Kwa nini nyakati za asubuhi na jioni msiongeze mabasi To & Fro Gerezani - Kimara - Kibaha?
 
Suala la kufanya kazi kaa saa 24 lina changamoto zake hasa za kiusalama, lakini suala lako tumelichukua na tutaliwasilisha kwa mamlaka zinazopanga masuala ya usafiri ili kuona kama linawezekana kutekelezwa. Kuhusu suala la kuongeza Mabasi ndio kipaumbele chetu kwa sasa, tutakapokamilisha kuongeza Mabasi yakutosha route ya Kibaha itapewa kipaumbele kwani ina abiria wengi hasa nyakati za asubuhi na jioni.
 
Sasa unaboreshaje usafiri wa umma kama ndani ya basi lako watu tunakuwa tumedimdisha? Usichukulie poa haya mambo au unataka mpaka siku nipigwe na mrembo kisa nimemchafualia nguo yake kwa kumbambia.
Mbona mna majibu mepesi kwenye mambo ya msingi nyie watu?
Hakuna majibu mepesi hapo hivyo ndivyo ilivyo kumchafua mtu ama kumgusa ama kumshika shika bila ridhaa yake ni kosa kisheria na kama wewe ni mmoja wa hao wenye tabia za kuwadhalilisha wakina mama katika mabasi na hata katika usafiri mwingine wa umma acha mara moja
 
Pia ongezeni idadi ya mabasi wakati wa rush hours mida ya saa 12 jioni -2 usiku pale gerezani, yaani abiria wanakaa zaidi ya saa nzima kwenye foleni kusubiri usafiri. Kwakweli inachosha, inaboa na inapoteza muda.

Pia idadi ya mabasi kutoka kimara kuelekea gerezani/kivukoni/morocco haitoshi wakati wa asubuhi kuanzia saa 12 asubuhi mpaka saa 3 asubuhi ...msongamano wa watu ni mkubwa na magari ni machache
Tumeendelea kusisitiza kuwa tuko katika hatua za kukamilisha uongezaji wa Mabasi tunatambua adha wanayopata wateja wetu tuendelee kuvuta subra tu, yajayo yanafurahisha na hutajutia kuendelea kutumia usafiri wa Mabasi ya mwendokasi.
 
Hakuna majibu mepesi hapo hivyo ndivyo ilivyo kumchafua mtu ama kumgusa ama kumshika shika bila ridhaa yake ni kosa kisheria na kama wewe ni mmoja wa hao wenye tabia za kuwadhalilisha wakina mama katika mabasi na hata katika usafiri mwingine wa umma acha mara moja
Wee niache wakati kubambia kutamu. 🤣🤣🤣🤣 Aya bana kama nyie hamtachukua hatua basi nggoja niwaite mataliban waje wawasaidieni kazi
 
Back
Top Bottom