DART kuchukua hatua dhidi ya Dereva na Wasimamizi wa Mwendokasi waliowapeleka Abiria Morocco badala ya Kimara

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
MWENDOKASI.jpg
Muda mfupi baada ya Member wa JamiiForums.com kusimulia tukio la Dereva wa Basi la Mwendokasi aliyetakiwa kuwapeleka Abiria Kimara kutoka Kivukoni, badala yake akawapeleka Kituo cha Morocco kisha kuwaacha hapo, jana Machi 26, 2024, mamlaka husika inatarajiwa kuchukua hatua.

Mtendaji Mkuu wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), Dkt. Athuman Kihamia amesema:

“Nilipata taarifa ya tukio hilo kutoka kwa kiongozi wa juu ambaye alipewa taarifa kutoka kwa Abiria aliyekuwa kwenye gari, nikafika eneo la tukio lakini kwa kuchelewa kidogo na hivyo kukuta wameshamaliza changamoto iliyotokea.

“Nimepata ripoti ya kilichotokea na imebainika Derev ana Wasimamizi hawakutumia busara katika kufanya maamuzi na kuhudumia Abiria, mwisho wake wakaanza kujibizana nao na kuwatelekeza kituoni hapo badala ya kuwapeleka Kimara.

“Kuna tukio lingine linalofanana na hilo pia limetokea Kimara, tunatarajia kuchukua hatua kali dhidi ya wahusika wote wanaofanya vitendo kama hivyo.

“Unapokabidhiwa huduma hiyo unatakiwa kuwa na nidhamu kwa sababu hiyo miundombinu ni ya Wananchi wao ndio wameiweka Serikali madarakani na wanahitaji huduma nzuri na wao ndio Wapiga kura.

“Tunatrajia kuchukua hatua kali ndani ya siku mbili hizi na tutatoa tamko dhidi ya Dereva aliyehusika pamoja na Wasimamizi ambao walikuwepo wakati wa tukio ili iwe fundisho kwa wengine wenye utovu wa nidhamu kazini.

“Kuna malalamiko mengi ambayo tumeyapata kuhusu huduma zetu, tunayafanyia kazi taratibu.”

Dkt. Athuman Kihamia aliteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika nafasi hiyo akichuku nafasi ya Dkt. Edwin P. Mhede ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Hoja ya Mdau hii hapa - Abiria wa Mwendokasi tuliotakiwa kutoka Kivukoni kwenda Kimara, Dereva katupeleka Morocco kisha akaturudisha Kivukoni
 
Hili suala linajirudia mara ya pili,ukiangalia kwa jicho zuri utagundua shida. Wananchi wana hasira na UDART lakini hasira zao wanazimalizia kwa madereva na watendaji wa chini wanaokutana nao. Ni sawa na mtu upige simu Vodacom huduma kwa wateja alafu umtukane mhudumu kuwa nyie Vodacom ni wezi. Nadhan kama raia wana hasira na Udart hasira zao wazipeleke sehemu husika. Ni mtazamo tu binafsi.
 
Tusiendeshe Nchi kwa mihemko na maagizo ya Wanasiasa. Basi linakwenda MOROCCO wahuni wachache wanapanda kwa Nguvu wanamwambia dereva peleka gari kimara! Halafu tnasema tunamwadhibu dereva? Tuache kufanya vitu kiholela, hao abiria ni wahuni tu ilipaswa wote wawe polisi kwa kusabbisha usumbufu. Kwa wapenda ustaarabu this is NO THANKS, Tukemee huu ujinga na upumbavu wa abiria wachache wanaotaka kujichukulia sheria mkononi.
 
Umewahi kupanda mwendokasi?
Basi lilisimama mahali ambapo ya Kimara yanaenda. Abiria hawakuwa wapumbavu hadi wapande hilo basi.
 
Hili suala linajirudia mara ya pili,ukiangalia kwa jicho zuri utagundua shida. Wananchi wana hasira na UDART lakini hasira zao wanazimalizia kwa madereva na watendaji wa chini wanaokutana nao. Ni sawa na mtu upige simu Vodacom huduma kwa wateja alafu umtukane mhudumu kuwa nyie Vodacom ni wezi. Nadhan kama raia wana hasira na Udart hasira zao wazipeleke sehemu husika. Ni mtazamo tu binafsi.
Naona wewe siyo mteja wa mwendokasi!
 
Wewe!
Ukitaka kuutikisa huo mnyororo wa uwajibikaji utagonga hadi jumba jeupe.
Ni vema tukamalizana na hao makanjanja tulio na uwezo nao hata wa kuwakaripia tu.
 
Tusiendeshe Nchi kwa mihemko na maagizo ya Wanasiasa. Basi linakwenda MOROCCO wahuni wachache wanapanda kwa Nguvu wanamwambia dereva peleka gari kimara! Halafu tnasema tunamwadhibu dereva? Tuache kufanya vitu kiholela, hao abiria ni wahuni tu ilipaswa wote wawe polisi kwa kusabbisha usumbufu. Kwa wapenda ustaarabu this is NO THANKS, Tukemee huu ujinga na upumbavu wa abiria wachache wanaotaka kujichukulia sheria mkononi.
Unatetea kibarua cha mumeo (dereva wa mwendokasi).? Kazi hana sasa atarudi nyumbani msaidiane kuvisha pampers watoto
 
Tusiendeshe Nchi kwa mihemko na maagizo ya Wanasiasa. Basi linakwenda MOROCCO wahuni wachache wanapanda kwa Nguvu wanamwambia dereva peleka gari kimara! Halafu tnasema tunamwadhibu dereva? Tuache kufanya vitu kiholela, hao abiria ni wahuni tu ilipaswa wote wawe polisi kwa kusabbisha usumbufu. Kwa wapenda ustaarabu this is NO THANKS, Tukemee huu ujinga na upumbavu wa abiria wachache wanaotaka kujichukulia sheria mkononi.
Duu
 
Back
Top Bottom