DAR: Zitto Kabwe ameachiwa kwa dhamana, ametuhumiwa kuvunja sheria ya makosa ya mtandao na kutoa takwimu za uongo

Awamu ya 5 inakusanya kodi kwa bidii lakini ndiyo Awamu ambayo inaongoza kwa matumizi mabaya ya pesa za Umma kuliko awamu zote.

Pesa inayotumika kwenye kukandamiza Demokrasia, kuwakomoa kuwabambikia kesi kuwadhalilisha, kuwadhoofisha Wapinzani ni pesa nyingi sana ni pesa ambazo zingeweza kujenga Daraja toka Dsm mpaka Zanzibar, kujenga viwanda Hosptal vyuo zaidi na barabara kila wilaya, lakini Madalali wa Siasa wakiongozwa na Lipumba na Bashite.

Maliyamungu mshauri mkuu wa Mtukufu wanavuna mabilioni kupitia mladi wao huo ambao hauna mkaguzi mkuu wa serikali kwani pesa zao huchukua Hazina Moja kwa moja kwa Amri ya Mtukufu malaika wa chato.
 
Sawa tu akamatwe .

Mambo mengine ni ya kujitakia maana kasikia kabisa mtu asitumie statistics za serikali bila kibali cha ofisi husika kumpa ruhusa yeye anaokoteza na kukimbia kimbia nazo mara London mara kijichi.

Tumeona takwimu zake zikitofautiana kabisa na zile serikali ilizozitoa.

Zzk, yeye anatumia slogan ya "pindua pindua ya mtandao wa simu" ngoja apewe adabu.

Mchuma janga hula na wa kwao.
 
Amekamatwa ili kuhojiwa na polisi. Na kabla ya hapo amedanganya umma kwa takwimu za uongo mara nyingi. Na tunajua hili ni kosa la jinai kwa mujibu wa Sheria za nchi.
Kwa hiyo nini cha ajabu akikamatwa?
Mbona serikali hudanganya takwimu mara nyingi sana ni nani atawashitaki serikali?
 
Ndio alichokua anakitaka sasa naye akaonje mahabusu kama mwenzie TL, anaropoka mno.
Anaropoka nini? Huko mahabusu ndipo kuna viwanda? Hakuna Udikteta usiokuwa na mwisho fanyeni unyama lakini ipo siku utafika mwisho walikuwepo akina Chiluba, idd Amin, Abacha, Bokasa, Sadam Husein, Gadafi wanyama kuliko Mtukufu leo hii wapo wapi?
 
Walishaonywa na Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi kuwa Safari Hii Kampeni ijikite kwny kutatua kero za level ya Udiwani si vinginevyo!

Yeye kaanza kuongelea ya Takwimu za BOT zinawahusu nini Madiwani!

Arudishwe kwao Misitu ya Congo
 
kama ni muongo na takwimu za serikali zapo sahihi na wanajiamini wa nini kushughulika nae?


Kwa nini apotoshe umma?

Wewe ukiwa Mwl, mwanafunzi akiandika majibu yasiyo sahihi na ulivyomfundisha utampatia alama za vyema kuwa amefanya vizuri!?

Nchi haiwezi ikavumilia wapotoshaji ili kupitia huo uongo wawadanganye watu na kujipatia sifa za kisiasa na vyeo kwa njia ya kudanganya.

Ngoja afundishwe adabu.
 
tunashukuru hawakumpiga risasi..
maana wasio hoja hukimbilia silaha..
ndio maana wengine wilihoji hizi PeheChidii..
bahati mbaya wakatoweka..
aendelee kushusha hoja kama alivyomshushia Ndubwai hadi leo ni bubu..
 
Salamu Wakuu..

Nimeona habari ya kukamatwa kwa Mh Zitto Kabwe kupitia kurasa fulani mtandaoni. Kwa haraka unaweza kujua ni kutokana na nini labda kutokana na press aliyofanya kuhusu masuala ya takwimu za ukuaji wa mapato, na uchumi kwa ujumla.

Kwa wale wahusika ni vyema kwasasa kuangalia hali hiyo na kukumbuka methali ya "Usishindane na kari;Kari ni mja wa Mungu".

Kizazi kisije wasomaji kwa mabaya na uongo wao...
 
Serikali ya kidikiteta kazi kukamata kamata tu hawana hoja kw nn wanatumia jeshi la polisi kujilinda?
 
Back
Top Bottom