Plea Bargain kwenye kesi ya utekaji...Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu Assad Abdulrasur (43) na wenzake watano kulipa faini ya Sh300,000 au kwenda jela miaka mitatu kila mmoja, baada ya kupatikana na hatia ya kumteka mwanamke na kisha kumshikilia kwa siku nne mfululizo.
Washtakiwa hao, walimteka Han Nooh Husein, tukio walilolitenda Oktoba 16, 2023 eneo la Msasani Beach, Wilaya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Pia, Mahakama hiyo imeamuru kila mshtakiwa kumlipa mlalamikaji (Han) fidia ya Sh500,000 kwa kumsababishia maumivu na mateso kutokana na kumshikilia kwa siku nne mfululizo katika nyumba ya Haidary Waziri iliyopo eneo la Msasani Beach.
Mbali na Abdulrasur, ambaye ni mkazi wa Msasani Village; washtakiwa wengine waliohukumiwa ku-tumikia adhabu hiyo ni Fahad Mussa (32) mkazi wa Dodoma Airport; Nathan Jothan (27) mkazi wa Sinza na Nicolas Nilahi (39) mkazi wa Wazo Hill.
Wengine ni Fredy Chahoza (49) mkazi wa Chamwino Dodoma; Ifan Saleh (41) mkazi wa Kisemvule.
Uamuzi huo umetolewa leo Machi 6, 2024 na Hakimu Mkazi Mkuu, Aaron Lyamuya, baada ya washtakiwa hao kufanya majadiliano na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DPP) ya kuimaliza kesi.
MWANANCHI
Aliingiliwa kimwili 1. Kawaida au 2. Kinyume?Alifanyiwa unyama na ukatili ambao kuusema hapa ni kumdhalilisha. Nilipoambiwa aliyofanyiwa kama mwanamke nililia machozi.
Ongeza na fidia ya 500,000 kila mtu ya kumlipa muhanga wa tukio.Imagine unaambiwa utoe 300,000 ama uende jela miaka mitatu 😆
Inawezekana ulichoambiwa kuna uongo ndani yake.Alifanyiwa unyama na ukatili ambao kuusema hapa ni kumdhalilisha. Nilipoambiwa aliyofanyiwa kama mwanamke nililia machozi.
800,000 tuOngeza na fidia ya 500,000 kila mtu ya kumlipa muhanga wa tukio.
Hakuna pesa yoyote inaweza kufidia uhalifu aliofanyiwa hata kifungo hakitoshi huu ndiyo ukweli wa hali halisi.800,000 tu
Yani unafikiri mimi ni mjinga wa kulia machozi kwa habari isiyo na uhakika?Inawezekana ulichoambiwa kuna uongo ndani yake.
Huyo bibie angefungua shitaka la madai, DPP asingeweza kuingilia kama alivyofanya kwenye hili la jinai. Tz unafanya uhalifu, halafu unanunua Uhuru wako kiurahisi tu, sijui DPP na hakimu wanapata kiasi gani, ilhali muathirika unaugumia madhila yaliyokusibu. Katiba mpya muhimu!Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu Assad Abdulrasur (43) na wenzake watano kulipa faini ya Sh300,000 au kwenda jela miaka mitatu kila mmoja, baada ya kupatikana na hatia ya kumteka mwanamke na kisha kumshikilia kwa siku nne mfululizo.