Dar: Waliomteka Mwanamke kwa siku 4 waachiwa baada ya kulipa Tsh. 300,000

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu Assad Abdulrasur (43) na wenzake watano kulipa faini ya Sh300,000 au kwenda jela miaka mitatu kila mmoja, baada ya kupatikana na hatia ya kumteka mwanamke na kisha kumshikilia kwa siku nne mfululizo.

Washtakiwa hao, walimteka Han Nooh Husein, tukio walilolitenda Oktoba 16, 2023 eneo la Msasani Beach, Wilaya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Pia, Mahakama hiyo imeamuru kila mshtakiwa kumlipa mlalamikaji (Han) fidia ya Sh500,000 kwa kumsababishia maumivu na mateso kutokana na kumshikilia kwa siku nne mfululizo katika nyumba ya Haidary Waziri iliyopo eneo la Msasani Beach.

Mbali na Abdulrasur, ambaye ni mkazi wa Msasani Village; washtakiwa wengine waliohukumiwa ku-tumikia adhabu hiyo ni Fahad Mussa (32) mkazi wa Dodoma Airport; Nathan Jothan (27) mkazi wa Sinza na Nicolas Nilahi (39) mkazi wa Wazo Hill.

Wengine ni Fredy Chahoza (49) mkazi wa Chamwino Dodoma; Ifan Saleh (41) mkazi wa Kisemvule.

Uamuzi huo umetolewa leo Machi 6, 2024 na Hakimu Mkazi Mkuu, Aaron Lyamuya, baada ya washtakiwa hao kufanya majadiliano na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DPP) ya kuimaliza kesi.

MWANANCHI
Plea Bargain kwenye kesi ya utekaji...

Nchi hii imejaa mizaha haswaa
 
Inawezekana ulichoambiwa kuna uongo ndani yake.
Yani unafikiri mimi ni mjinga wa kulia machozi kwa habari isiyo na uhakika?
Fahamu tu, ni ukweli na uhakika.

Na ukitaka kujiridhisha na hilo ndio maana sisemi, ukiona mtu anakimbilia kusema jambo jua ni uongo. Ukweli ni nadra sana kusambazwa.
 
FB_IMG_1709906660913.jpg
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu Assad Abdulrasur (43) na wenzake watano kulipa faini ya Sh300,000 au kwenda jela miaka mitatu kila mmoja, baada ya kupatikana na hatia ya kumteka mwanamke na kisha kumshikilia kwa siku nne mfululizo.

Washtakiwa hao, walimteka Han Nooh Husein, tukio walilolitenda Oktoba 16, 2023 eneo la Msasani Beach, Wilaya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Pia, Mahakama hiyo imeamuru kila mshtakiwa kumlipa mlalamikaji (Han) fidia ya Sh500,000 kwa kumsababishia maumivu na mateso kutokana na kumshikilia kwa siku nne mfululizo katika nyumba ya Haidary Waziri iliyopo eneo la Msasani Beach.

Mbali na Abdulrasur, ambaye ni mkazi wa Msasani Village; washtakiwa wengine waliohukumiwa ku-tumikia adhabu hiyo ni Fahad Mussa (32) mkazi wa Dodoma Airport; Nathan Jothan (27) mkazi wa Sinza na Nicolas Nilahi (39) mkazi wa Wazo Hill.

Wengine ni Fredy Chahoza (49) mkazi wa Chamwino Dodoma; Ifan Saleh (41) mkazi wa Kisemvule.

Uamuzi huo umetolewa leo Machi 6, 2024 na Hakimu Mkazi Mkuu, Aaron Lyamuya, baada ya washtakiwa hao kufanya majadiliano na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DPP) ya kuimaliza kesi.

MWANANCHI
Huyo bibie angefungua shitaka la madai, DPP asingeweza kuingilia kama alivyofanya kwenye hili la jinai. Tz unafanya uhalifu, halafu unanunua Uhuru wako kiurahisi tu, sijui DPP na hakimu wanapata kiasi gani, ilhali muathirika unaugumia madhila yaliyokusibu. Katiba mpya muhimu!
 
Back
Top Bottom