Dar: Vicky Kamata atoa Msaada kwa Shule ya Sekondari Mbwenitete, iliyopo Jimbo la Kawe, Wadau Waombwa kuendelea kusaidia

pantheraleo

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
691
878
Salaam Wakuu,

Alfonce Peter Swai, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Serikali ya Mbwenitete iliyopo Mbweni, Kawe Wilaya ya Kinondoni Mkoani Dar Es Salaam, ameomba Wadau wa Elimu kusaidia Shule kwani ina Ufaulu Mzuri pamoja na Changamoto zilizopo.
IMG_20220513_131717_999.jpg

Amesema Komputa ni Somo lipo kwenye Mtaala wa Elimu, Shule ina Madarasa lakini haina Komputa hata moja. Ameyasema hayo leo Tarehe leo tarehe 13 Mei 2022 wakati akipokea Misaada Mbalimbali kutoka kwa Mkurugenzi wa Victoria Foundation Vicky Kamata.

Mwalimu Mkuu Swai wakati anaelezea changamoto zinazoikabiri Shule ya Mbwenitete, amesema maji yapo lakini hayajasambazwa Vyooni, Shule haina Uzio. Pia ameishukuru Serikali kwa kuwajengea Madarasa 7 ya mradi wa UVIKO.
IMG_20220513_130622_901.jpg

Naye Madam Victoria ambaye ni Makamu wa Shule hiyo, Amempongeza Vicky Kamata kwa Msada wa TV, Taulo za Kike na Vitabu. Amesema Shule bado ina Upungufu wa Vitabu vya Sanaa kwani wana Vitabu Vili kwa wanafunzi 80. "Shule yetu ya Sekondari ina Wanafunzi 1400, lakini Vitabu vya sanaa vilivyopo ni 2 kwa Watoto 87. Vitabu vya Sayansi vipo. Tunayo Maktaba lakini haina Samani kama Meza, Makabati na Viti, Wadau Wazidi kujitolea kutusaidia". amesema Madam Victoria.

Pamoja na Changamoto hizo, Shule imeweza kufaulisha Wanafunzi wote wa Kidato cha Sita 2021 kwenda Chuo Kikuu, Pia kidato cha nne walipata Sifuri ni 4 tu kati ya wanafunzi 90. Na hizo Sifuri zilisababishwa na sababu mbalimbali.

Naye Vicky Kamata ambaye pia ni Msanii wa Wimbo maarufu wa Wanawake na Maendeleo, ameiomba Jamii na Taasisi mbalimbali kuisaidia Shule ya Mbwenitete ili Wanafunzi wapate Msingi Mzuri wa Elimu.

Akitoa nasaha kwa Watoto waliohitimu Kidato cha Sita amesems "Maisha ndo mnayaanza, safari ndio mnaianza. Unaweza shangaa yule anayesoma kwa shida akafanya Vizuri Mtaani na mwingine aliyepewa kila kitu Shule na alikuwa anafanya Vizuri akashindwa Uraiani Sababu haumizi akili yake kufanya kazi. Vijana wa kike na kiume Maisha ni wewe, Usitegemee wazazi, tafuta vya kwako. Tegeneza vya kwako. Sawa Mzazi wako anaweza akawa na Cheo au mtu Maalufu, kumbuka Cheo ni cha wazazi, akifa hatakurithi na Utataabika sana" Amesema Vicky Kamata.

Amewataka Watoto wa Kike Wasijione Wanyonge kwani Wanaweza.
IMG_20220513_125503_226.jpg
IMG_20220513_125632_881.jpg
IMG_20220513_125703_884.jpg
IMG_20220513_124935_622.jpg
IMG_20220513_121617_451.jpg
IMG_20220513_125207_199.jpg

 
Back
Top Bottom