Dar: Mtumishi wa Wizara ya Ardhi akutwa na hatia ya Matumizi mabaya ya Madaraka na Kughushi Nyaraka

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
Mahakama ya Wilaya ya Ilala imemkuta na hatia ya Matumizi Mabaya ya Madaraka pamoja na Kughushi Nyaraka, mtumishi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliyetambulishwa kwa majina ya Melchiory Rutayuga Mukandala.

Keshi hiyo iliyowasiliswa na Jamhuri kupitia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKURU) imetaja makosa ya mtuhumiwa kuwa ni kinyume na Kanuni ya Adhabu na Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329.

Mahakama imemhukumu Mtumishi huyo adhabu ya kulipa faini ya Tsh. Milioni 1 kwa kila kosa au kutumikia kifungo cha miaka miwili gerezani kwa kila kosa na adhabu zote zinaenda kwa pamoja.
 
Hawa ndio wanaleta vurugu na migogoro ya viwanja ....Kwa waliotapeliwa wanajua balaa lake.
 
Kwa Hali hii akirejea kazini ni tatizo... Ana takiwa afukuzwe kazi baada ya kukutwa na hatia, isiwe kulipa na kurudishwa kazini
 
Kwa makosa hayo mawili fine ni million mbili! 😂😂😂😂😂
Msije mkatoa lawama kwa hakimu maana yeye anatimiza matakwa ya kisheria … Hivyo wakupewa lawama ni watunga sheria ambao ni wabunge
 
Alighushi nyaraka kujipatia nini au kujipatia shilingi ngapi, hamjasema

Ukute alighushi nyaraka na kujipatia kiwanja masaki kisha analipa faini milioni 2
 
Huyu m
Mahakama ya Wilaya ya Ilala imemkuta na hatia ya Matumizi Mabaya ya Madaraka pamoja na Kughushi Nyaraka, mtumishi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliyetambulishwa kwa majina ya Melchiory Rutayuga Mukandala.

Keshi hiyo iliyowasiliswa na Jamhuri kupitia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKURU) imetaja makosa ya mtuhumiwa kuwa ni kinyume na Kanuni ya Adhabu na Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329.

Mahakama imemhukumu Mtumishi huyo adhabu ya kulipa faini ya Tsh. Milioni 1 kwa kila kosa au kutumikia kifungo cha miaka miwili gerezani kwa kila kosa na adhabu zote zinaenda kwa pamoja.
mbona wamemuonea. Makosa ya kifisadi adhabu yake Ni faini isiyozidi elfu kumi au kifungo Cha nje wiki moja.
Sasa wewe kutwa na nyama ya ngiri uone Moto wake.
 
Kwa makosa hayo mawili fine ni million mbili! 😂😂😂😂😂
Msije mkatoa lawama kwa hakimu maana yeye anatimiza matakwa ya kisheria … Hivyo wakupewa lawama ni watunga sheria ambao ni wabunge
Wabunge Ndiyo Tatizo
 
Back
Top Bottom