Dar: Mihadhara ya kidini yapigwa marufuku!

hiyo radio ya uchochezi ikajifunze kwa radio zilizofanikiwa za dini nyingine kama wapo radio nk sio kufundisha chuki kwa wengine huwezi kuta iyo radio inalaani shughuli za uchawi uganga wa kienyezi wao ni kulaani ukristo mara mfumo kristo wakati ndugu zao ndo wanaongoza nchi.utazani wametumwa kuchochea uvunjifu wa amani
 
WASIO DHAIFU NI KAMA KENYA CHEKI WALIVYO KIUME HAWAMUMUNYI MANENO;
"The Mombasa Republican Council's (MRC) campaign for the secession of Kenya's Indian Ocean coastal strip, a tourist hotspot and trade hub, is just one of many concerns ahead of the March election, the first since the 2007 vote after which some 1,200 people were killed and thousands were displaced."I am asking all MRC officials and members who are still out there to surrender voluntarily and also surrender their weapons this weekend," Coast province commissioner Samuel Kielele said at a gathering for national day celebrations in Mombasa.
"We know them and we will go for them if they don't heed this call. We will go for them and arrest them," he said.
President Mwai Kibaki also said his government would take decisive action against those who "issued threats of secession or those who threaten our security".

Source Kenya tells separatist group: surrender or face arrest | Reuters
 
wakikosa vijiwe vya mihadhara ndo watakumbuka na kwenda shule walau hata english course tu...kuna shule zingine secondary unasoma miaka miwili tu siku hizi, waende huko ili ukoko utoke kichwani wakirudi watakuwa kwenye 21century na kufanya ugaidi wa kuchoma makanisa kutaisha.
 
Mihadhara wakafanyie kwenye nyumba zao za dini na kinachofuata ni kuondoa ile Mikengere juu ya makanisa na Maspika juu ya misikiti me huwa nakeraka sana nikiyasikia.... Mkuu wa mkoa nakupa heko hat ule mtaa wa Agrey msikiti wa qibratain na pale near msimbazi msikiti wa Idrisa ni kero sana Mitaa inafungwa fungwa kwa shughuri zisizo na maana itakuwa ndio mwisho wake sasa.. wamama ntilie wamejazana jioni hadi njia kupitika inakuwa kero na wakati wa Ramadhani ndio huugeuza wao wanafturu barabarani kana kwamba hawana makwao....

Pale karibu na Mtaa wa Mchikichi ndio wameweka maduka ya vitabu vya dini na kuuteka mtaa magari hayapiti tena hivi nyinyi vipi?
 
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadick amepiga marufuku mihadhara yote ya kidini inayokashifu na kukebehi imani za watu wengine, hadi hapo hali itakapokuwa shwari.

Ameonya pia dhidi ya waandishi na vyombo vya habari vinavyochochea udini kuacha mara moja kabla hatua husika hazijachukuliwa.Alipoulizwa hali itakapokuwa shwari waendelee alisema , katiba inaruhusu uhuru wa maoni ambao hauhatarishi amani ya nchi.

Muda wote alikuwa wapi? Maji yameishamwagika tayari!

mihadhara wakafanyie kwenye nyumba zao za dini na kinachofuata ni kuondoa ile mikengere juu ya makanisa na maspika juu ya misikiti me huwa nakeraka sana nikiyasikia.... Mkuu wa mkoa nakupa heko hat ule mtaa wa agrey msikiti wa qibratain na pale near msimbazi msikiti wa idrisa ni kero sana mitaa inafungwa fungwa kwa shughuri zisizo na maana itakuwa ndio mwisho wake sasa.. Wamama ntilie wamejazana jioni hadi njia kupitika inakuwa kero na wakati wa ramadhani ndio huugeuza wao wanafturu barabarani kana kwamba hawana makwao....

Pale karibu na mtaa wa mchikichi ndio wameweka maduka ya vitabu vya dini na kuuteka mtaa magari hayapiti tena hivi nyinyi vipi?
wewe nyau mdini kweli mbona hujatoa mifano hiyo mikengele ilipo? Umetoa mifano kwa waislam tu
 
nafikiri mkuu hujafiri vya kutosha basi radio imani haitakiwi kabisa kuzungumzia na kukashifu dini nyingine kama inavyo fanya sasa itoe mafundisho kwa waamini wako inavyohitajika,na hilo gazeti la alnuura liache uchochezi haijawahi tokea na haita tokea kusikia radio au magazeti ya kikristo yana wasema waislam kama unaushahidi anika hapa jukwaani si kutukanatukana hapa.
wapo radio walisema aliyekojolea msahafu ni muislam, unataka ushahidi gani mwingine?
 
Radio na magazeti, machapisho ya vijarida pamoja na vipeperushi vina athari kubwa sana katika suala zima la uchochezi na ukiukwaji wa amri aliyoitoa huyu Mkuu wa Mkoa. Lakini pia bado ni kweli kuwa mihadhara ni haki ya kikatiba kwa hiyo kuzuia shughuli hiyo ni kunyonga uhuru wa wahusika. Mahubiri ya dini lazima yahusishe mihadhara, hivyo mihadhaara siyo mibaya bali maudhui katika mihadhara hiyo.

"TWENDE PAMOJA NA TANZANIA ITAKUWA IMARA"
 
wewe nyau mdini kweli mbona hujatoa mifano hiyo mikengele ilipo? Umetoa mifano kwa waislam tu
Punguza Jazba nyie mbona mkipewa Ukweli mnahamaki sana.... Mikengere naichukia sana haswa pale Luther House Kuna Kanisa pale kuna kipindi niliishi New Africa Hotel then NBC house pale ilikuwa ni kero sana pale... Kuna Mtaa wa Narung'ombe kuna kanisa pale hufunga mtaa na huwa linapiga kengere mornie ila sikuhizi wameweka kikengere kidogo so hata hakikeri raia.... Ila ile mispika nomaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa! time nyingi sana ni kero Katiba mpya yaondolewe haya kwani ni nani haswa ayasikie? kama ni imani ipo moyoni mwa mtu na sio kulazimisha mtu asikie maneno yasiyo eleweka...

Ningekuwa na mabawa ningekuwa nayapitia nayang'oa na kwenda kuyatupa baharini....

Kharid Ponera Punguza Jazba
 
Last edited by a moderator:
Huu ni upuuzi. Kwanini kuipigia mihadhara marufuku hadi hali itakapokuwa shwari wakati wameishakiri kuwa inakashfu dini za wengine? Kinachokera ni kwamba hawa wanaojifanya wahubiri hawana elimu si ya ukristo wala uislam bali njaa na kutafuta sifa. Kuna haja ya kufanya mihadhara kuwa kosa la jinai hasa wahusika wanaposhambulia dini nyingine au kutokuwa na elimu juu ya kile wanachohubiri.
 
KIchapo cha Jana na baada ya jamaa kuona WAJEDA kibao mtaani, Leo ukiwa KAriakoo ukimsalimia mtu "ASALAAM ALEYKUM" jibu lililo kuwa linapatikana ni MILELE AMINA. Kichapo noma.
 
kwa wakristo utaikuta BIBLIA na YESU wake,kwa waislamu nako BIBLIA na YESU!kumbe wote Wagalatia mmepishana staili ya kutoka tu!
 
[h=3][/h]

Hivi karibuni mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Saidi Meck Sadiki alikaririwa akisema kuwa serikali imepiga marufuku mihadhara ya kidini inayokashfu dini nyingine hadi hali itakapotulia. Mihadhara hii imekuwa ikiendeshwa na kushabikiwa na waislam hasa wa kada ya chini hasa wasio na elimu ukiachia mbali kudhaminiwa na wafanya biashara wengi wenye asili ya kiarabu. Huu ni upuuzi. Kwanini kuipigia mihadhara marufuku hadi hali itakapokuwa shwari wakati wameishakiri kuwa inakashfu dini za wengine? Kinachokera ni kwamba hawa wanaojifanya wahubiri hawana elimu si ya Ukristo wala Uislam bali njaa na kutafuta sifa. Kuna haja ya kufanya mihadhara kuwa kosa la jinai hasa wahusika wanaposhambulia dini nyingine au kutokuwa na elimu juu ya kile wanachohubiri.
Hii imekuwa staili ya serikali yetu ya nguvu ya soda katika kupambana na matatizo. Leo tunaambiwa hata Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) nayo imepiga marufuku mihadhara ya wana Uamsho. Too late. Mwanzoni chini ya kihoro cha kutaka muungano SMZ iliridhia na hata kushirikiana na Uamsho kuhubiri chuki na dhihaka dhidi ya muungano ikidhani ingeweza kuwatumia kufikia ajenda zake bila kujua kuwa nao walikuwa na ajenda zao fichi. Maalim Seif Shariff Hamad alipigia upatu hili . Kwani hii imekuwa ajenda yake tangu akiwa CCM hata baada ya kufukuzwa CCM na kurejea kwa mlango wa nyuma chini ya kisingizio cha serikali ya Umoja wa Kitaifa (GNU) ambayo hata hivyo inamhusu yeye na si chama chake. Leo wamegundua janja ya kutumiana wanaamka na kuanza kupiga mihadhara marufuku. Yote hii ni matokeo ya kuwa na watawala wasioona mbali.
Hakuna anayehitaji mihadhara katika maisha. Mbona mihadhara imeanza juzi juzi miaka ya 90? Mbona kabla ya hapo tulikuwa tunaheshimiana na kupendana. Kesho wataibuka wahubiri wa mihadhara wa Kikristo waanze kuonyesha udhaifu wa Uislamu na waislamu wataanza kuja juu na kuchoma makanisa kutokana na kutokuwa na subira. Je namna hii tutafika? Maana kila dini ina udhaifu wake. Ndiyo maana dini zote hupenda kuwaaminisha watu badala ya kuwaelimisha. Hivi kwa mfano mtu leo akija anaongelea maisha ya Khadija mke wa kwanza wa Mtume aliyemwamuru Mtume amuoe si watu mtakatana shingo bure?
Wengi wa waendesha mihadhara ni watu wasio na kazi ambao kimsingi ni wanyonyaji. Hata Uislam kama utatafsiriwa vizuri unazuia ujinga huu. Sayydina Omar ibn Al- Khatab Khalifa wa pili alipiga marufuku watu kumaliza salat na kuendelea kupiga mdomo wakiswali taraweh badala ya kwenda kufanya kazi.
Ila baada ya Tanzania kuruhusu utapeli wa kutumia majoho ya dini, tumeshuhudia kuibuka utitiri wa mihadhara na madhehebu ya kikristo mengi yakiendeshwa na matapeli wanaotaka utajiri wa haraka.
Je serikali inamdanganya nani zaidi ya kujidanganya na kulea huu uhuni usio na faida kwa watanzania?
 
Nakpupa LIKE, kwa kuniibia mawazo yangu na kuyaandika hapa. wewe si mimi bali unafikiri kama ninavyofikiri,BIG UP.

[/QUOTE]
 
Back
Top Bottom