Dar: Mihadhara ya kidini yapigwa marufuku!

Skillionare

JF-Expert Member
Nov 6, 2011
1,190
523
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadick amepiga marufuku mihadhara yote ya kidini inayokashifu na kukebehi imani za watu wengine, hadi hapo hali itakapokuwa shwari.

Ameonya pia dhidi ya waandishi na vyombo vya habari vinavyochochea udini kuacha mara moja kabla hatua husika hazijachukuliwa.Alipoulizwa hali itakapokuwa shwari waendelee alisema , katiba inaruhusu uhuru wa maoni ambao hauhatarishi amani ya nchi.
 
Ingekuwa vyema MKuu wa mkoa aweke wazi ana maana gani "mihadhara ya kidini"

Na vyombo gani wanalenga kuhusiana na uchochezi? Bila kuwa specific tamko hii haina nguvu kabisa!
 
Bado hapo hajawa specific mihadhara ya dini gani na radio gani ni Radio free au Radio imaan,? Gazeti la Ijumaa au gazeti la Al-nuur?

Pia tamko hilo lifaa litolewe na mkuu wa nchi au waziri husika.
 
Mkwara wa kizamani!!Redio iman ifungiwe kwanza kama onyo, statement ilitakiwa kusomeka hivi-tunaifungia hadi hapo itakapojirekebisha,hii ya kumtishia kumkimbiza mtu uliyesimama naye ni dalili ya uoga.
 
Serikali inafanya makosa makubwa kuacha hii Redio WAPO ndio chanzo ni kashfa na matusi makubwa kwa viongozi wa kiislam.
 
Hii haina uzito wowote ni kama unashtuka kujifunika wakati ndio kunakucha....
Wakati wote watu wamepiga kelele kuhusu hiyo mihadhara lakini walijifanya kuziba masikio. Leo hii ndio wanashtuka wakati akili za watu zimeshaharibiwa kwa zaidi ya 80%.
 
Waislamu sasa hivi wanatumia misikitu kumwaga sumu, wanatumiana SMS pia. Kupiga marufuku mihadhara haisaidii.
 
Ni sawa na kutibu kansa ambayo tayari imeshasambaa mwilini.

Viongozi wa nchii ni kama wako likizo.Wako makini kudhibiti chadema na sio mihazara ya kidini.

It is already too late.
 
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam amepiga marufuku mihadhara yote ya kidini, hadi hapo hali itakapokuwa shwari.

Ameonya pia dhidi ya vyombo vya habari vinavyochochea udini kuacha mara moja kabla hatua husika hazijachukuliwa

Hata hali ikiwa swari hatutaki kuona mashehe wakishika Biblia kwenye mihadhara yao na kuistafsiri wanavyotaka wao. Kila mtu ahubiri cha dini yake.
 
Back
Top Bottom