DAR: Masogange ahukumiwa miaka 3 Jela au faini Mil 1.5 kwa kosa la Dawa za kulevya! Aachiwa huru baada ya kulipa faini

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
2,036
3,931
masogange.jpg

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemtia hatiani msanii Agnes Gerald, maarufu Masogange kwa kosa la kutuma dawa za kulevya aina ya Heroin (DiacetyImophine).

Hukumu bado haijasomwa.

======

UPDATES;

=>
Agnes Gerald ahukumiwa Miaka mitatu jela au Faini ya Milioni moja na nusu kwa makosa mawili ya Madawa ya kulevya. Kosa la kwanza ni kutumia dawa za kulevya aina ya heroine, na la pili kutumia dawa za kulevya aina ya Oxazepam. Ameachiwa huru mara baada ya kulipa faini ya Sh milioni 1.5.

=> Masogange alikamatwa na Polisi baadae, Jeshi la polisi lilikabidhi sampuli kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kwa ajili ya kuthibitisha kama mlimbwende huyo anatumia dawa za kulevya au la.

=> Mahakama Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru msanii Agnes Gerald(Masogange) baada ya kulipa faini ya Tsh. Milioni 1.5

======

Mfululizo wa kukamatwa, kesi, hukumu na kuachiwa huru kwa Agnes Masogange kwenye kesi ya Madawa ya kulevya
Masogange ajisalimisha mwenyewe Mahakama a Kisutu
Kupandishwa kizimbani na kusomewa shitaka
Yaliyojili wakati wa kesi ya Masogange
Masogange kupelekwa kwa Mkemia Mkuu
Kesi kusikilizwa
Tetesi za kuachiwa huru
Hukumu

Visa vya watu maarufu wengine waliowahi kutuhumiwa au kukamatwa na madawa ya kulevya
 
Huyu siashiriki kupeleka mafurushi ya unga SA

Wazee hususani bosi wa mkoa akamtoa eti ulikuwa unga wa mihogo. Leo....!
 
Siungi mkono watumiaji dawa za kulevya ila kitu ambacho sijaelewa mpaka leo kipindi anatuhumiwa huyu masogange alikuwa anatuhumiwa pamoja na akina TID, romy jones na wengine.

Japokuwa akina TID na romy jones walikubari kuwa watumiaji wa dawa ni kesi ya masogange tu iliyopelekwa mahakamani na wemasepetu ambao ndiyo wao tu walikataa tuhuma hizo.

Sijui walitumia kanuni gani kuwasemehe akina TID na wenzake bila kuwafikisha mahakamani lakini hawa wawili ndiyo wakapelekwa mahakamani.

Kesi ya wema nadhani kila mtu amekwishajua kuwa ishaharibiwa huenda masogange kuna kitu alikataa kumpa mtu aliyekuwa anamtuhumu...
 
Chid Benz amekamatwa juzi na madawa ya kulevya ila baadae anaonekana mitaani akila good time.

Nchi masikini zina changamoto kubwa ya maendeleo. Ni nchi zinazoendeshwa kwa upendeleo na visasi, hakuna ufuataji wa sheria, sheria zake zina macho.

Ni matatizo matupu.
 
Siungi mkono watumiaji dawa za kulevya ila kitu ambacho sijaelewa mpaka leo kipindi anatuhumiwa huyu masogange alikuwa anatuhumiwa pamoja na akina TID, romy jones na wengine.
Japokuwa akina TID na romy jones walikubari kuwa watumiaji wa dawa ni kesi ya masogange tu iliyopelekwa mahakamani na wemasepetu ambao ndiyo wao tu walikataa tuhuma hizo.
Sijui walitumia kanuni gani kuwasemehe akina TID na wenzake bila kuwafikisha mahakamani lakini hawa wawili ndiyo wakapelekwa mahakamani.
Kesi ya wema nadhani kila mtu amekwishajua kuwa ishaharibiwa huenda masogange kuna kitu alikataa kumpa mtu aliyekuwa anamtuhumu...
Style ilitumika kumfikisha mahakani ni ile ya kutoa ushirikiano hasa hasa kutoa taarifaza wauzaji wakubwa. Kumbuka huyu ashawahi kukamatwa south afrika na mzigo wa maana tu. Na kwa experience yangu, mara nyingi wasafirisha wa haya madawa na hata hao baadhi ya wakubwa ni mateja kwa kiasi fulani so kuwa huyu dada anatumia sio geni kabisa. Tid na huyo mwingine nahisi walionyesha ushirikiano kwa namna moja ama nyingine. Kimashitaka hiyo inakubalika kabisa hasa wapelelezi wanapotaka kufika katika mzizi wenyewe kabisa.
 
Mbona akina majizo na tid na chid benz wanadunda kitaan alafu mumekomaa na dada wa watu kwahiyo mnataka mumufunge kisa kakataa kuingia ccm achen upuuz wenu

Selikal ya kishamba sana hii inayoongozwa na viongoz wapuuz washamba waliojaa visas

Maza faka
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu video queen Agnes Gerald 'Masogange' kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini ya sh milion 1.5 baada ya kupatikana na hatia ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin na Oxazepam
 
Mmmh....sasa hyo milion 1 ndo itamshinda? Hii nchi sheria yake bwana ingekua mtu ambae siyo maarufu angepigwa fain hata ya milion nying nying huko....
 
Selikar ya kipuuz sana hii kwanini majizo hajafungwa vp kuhusu tid na chid benz vp kuhusu mdogo wake na ester bulaya kwanini hao hawajafungwa mumehangaika na video queen

Masikin wa mungu mdada wa watu hadi namuonea huruma

Pole agnes
 
Huyu siashiriki kupeleka mafurushi ya unga SA

Wazee hususani bosi wa mkoa akamtoa eti ulikuwa unga wa mihogo. Leo....!
Mkuu,mnyonge mnyongeni haki yake mpeni,ni bora unapoandika uwe na data kamili au kama hujui ni bora uulize.
wakati masogange anakamatwa South Africa huyo bosi wa mkoa wala alikuwa hajulikani, sijui alikuwa bado yuko shule ?!
Kwa hiyo aliyemtoa masogange siyo bosi wa mkoa,watu waliyo mtuma masogange na ule mzigo wa(siyo unga halisi) raw materials ya kutengenezea unga walilipa faini,ilikuwa ni pesa nyingi kwa wakati ule nadhani haikuwa chini ya rand 2ml.
Wakati huo SA ilikuwa ukikamatwa na unga kwa kiasi kikubwa unafungwa bila fine ila kwa raw materials unapata kifungo au unalipa fine.
Ila sasa hivi ni kifungo tena kikubwa sana ,siyo chini ya 15yrs
 
Siungi mkono watumiaji dawa za kulevya ila kitu ambacho sijaelewa mpaka leo kipindi anatuhumiwa huyu masogange alikuwa anatuhumiwa pamoja na akina TID, romy jones na wengine.
Japokuwa akina TID na romy jones walikubari kuwa watumiaji wa dawa ni kesi ya masogange tu iliyopelekwa mahakamani na wemasepetu ambao ndiyo wao tu walikataa tuhuma hizo.
Sijui walitumia kanuni gani kuwasemehe akina TID na wenzake bila kuwafikisha mahakamani lakini hawa wawili ndiyo wakapelekwa mahakamani.
Kesi ya wema nadhani kila mtu amekwishajua kuwa ishaharibiwa huenda masogange kuna kitu alikataa kumpa mtu aliyekuwa anamtuhumu...
Ndo basi tena maamuzi ya mahakama
 
Hahaha angekuwa MTU wa chadema hapo kusingekuwa na option ya faini ,angeenda ndani mazima
 
Siungi mkono watumiaji dawa za kulevya ila kitu ambacho sijaelewa mpaka leo kipindi anatuhumiwa huyu masogange alikuwa anatuhumiwa pamoja na akina TID, romy jones na wengine.
Japokuwa akina TID na romy jones walikubari kuwa watumiaji wa dawa ni kesi ya masogange tu iliyopelekwa mahakamani na wemasepetu ambao ndiyo wao tu walikataa tuhuma hizo.
Sijui walitumia kanuni gani kuwasemehe akina TID na wenzake bila kuwafikisha mahakamani lakini hawa wawili ndiyo wakapelekwa mahakamani.
Kesi ya wema nadhani kila mtu amekwishajua kuwa ishaharibiwa huenda masogange kuna kitu alikataa kumpa mtu aliyekuwa anamtuhumu...
Nafikiri kuna kifungu cha sheria kinachompa uhuru jaji wa ku-lighten sentence kama mshitakiwa atakiri kosa bila ya kuisumbua mahakam,lakini ukikana na ushahidi ukathibiti basi mvua itakunyeshea tu
 
Wakima TID na akina vanessa hata mahakamani nadhani hawakufikishwa. Akina TID na Romy walipoachiwa tu wakaanza kutembea na makonda wakikiri utumiaji wao wa dawa
 
Back
Top Bottom