Dar es Salaam Operation ni biashara kubwa wajawazito

Jodari

Senior Member
Mar 2, 2013
120
16
Nimeshuhudia Madr. Wengi sasa elimu yao wanaiweka upande na kuingia kwenye bishara hii ya kufanyia uperation wajawazito, operation huwa inafanyika kwa malipo makubwa kiasi cha laki6 kila mgonjwa. Ivi tuseme hawa maDr wameshindwa kabisa kutoa tiba na sasa wameamua kufanya biashara? Niliwahi kumpeleka mke wangu alikua mjamzito pale mikumi na nikaambiwa mtoto ameelekeza miguu chini kwaiyo akiwa tayari kujifungua afanyiwe operation ikaishia hapo hakuna tiba yoyote aliyopatiwa. Nilisafiri nikaenda dubai nikafika duka la dawa la kawaida nilipatiwa dawa zinaitwa folic acid na niliambiwa hizo zitamuweka sawa kila kitu mama na mtoto wake. Hii nchi ni ya ajabu sana ivi watu hawa wanaoitwa madr kukosa uzalendo na kazi zao inakuwaje? Akatumia hizi dawa kwa miezi 3 afya yake ikaimarika na akajifungua mtoto ana kilo4.3 kwa nji ya kawaida bila ya matatizo tunamshukuru mungu. Serikali tunaiyomba iwe inazianglia biashara hizi haramu pia.
 
wewe kweli zuzu hizo folic acid zinatolewa kila clinic ya hakina mama wajawazito kwa ajili kuongeza damu na pia kusaidia kutopata malformation, wewe ukaenda dubai kwa ajili ya folic acid, u should be ashamed of your ignorance
 
Hizo mnazopewa hapa mzee wangu na uzuzu wangu munatiwa changa la macho kabisa tena ni aibu yenu hazifai hata kumpa paka wangu nyumbani akiwa mjamzito.
 
wewe kweli zuzu hizo folic acid zinatolewa kila clinic ya hakina mama wajawazito kwa ajili kuongeza damu na pia kusaidia kutopata malformation, wewe ukaenda dubai kwa ajili ya folic acid, u should be ashamed of your ignorance

Ni bora usiongee ivi vitu usivovijua na nimeshawachukulia kama wadad 3 wamejifungua vizuri tuu, hakuna kifafa cha mimba, hakuna kuvimba miguu, wala hakuna hata kutapika
 
Hii nayo ni ishu, ila nimepata kusikia wasichana wengi wanataka operation kukwepa uchungu,pia sababu za kitabibu..ila ma Dr. wenyewe watufafanulie, japo kila sekta sasa inakabiliwa na mmomonyoko wa maadili wapo wanaofanya operation kama chanzo cha mapato ila aibu sana.
 
Jodari,

1.Sijatambua kuwa kuna ubaya gani kufanya operation kama unaweza ujuzi!
2.Unaposema ni gharama kubwa kiasi una maana ipi?..Ni kiwango gani cha gharama si kikubwa? Ni vifaa gani vitumikavyo katika mjamzito kujifungua, watu wangapi huusika?
3. Kwa maelezo yako unadhani dawa za Folic Acid hazipo nchini hadi Uarabuni?
5.Kwa misingi ipi Folic acid zitabadilisha ukaaji wa mtoto ..yaani kutanguliza miguu kubadilike kwa kutumia dawa hizo?
 
Last edited by a moderator:
Nimeshuhudia Madr. Wengi sasa elimu yao wanaiweka upande na kuingia kwenye bishara hii ya kufanyia uperation wajawazito, operation huwa inafanyika kwa malipo makubwa kiasi cha laki6 kila mgonjwa. Ivi tuseme hawa maDr wameshindwa kabisa kutoa tiba na sasa wameamua kufanya biashara? Niliwahi kumpeleka mke wangu alikua mjamzito pale mikumi na nikaambiwa mtoto ameelekeza miguu chini kwaiyo akiwa tayari kujifungua afanyiwe operation ikaishia hapo hakuna tiba yoyote aliyopatiwa. Nilisafiri nikaenda dubai nikafika duka la dawa la kawaida nilipatiwa dawa zinaitwa folic acid na niliambiwa hizo zitamuweka sawa kila kitu mama na mtoto wake. Hii nchi ni ya ajabu sana ivi watu hawa wanaoitwa madr kukosa uzalendo na kazi zao inakuwaje? Akatumia hizi dawa kwa miezi 3 afya yake ikaimarika na akajifungua mtoto ana kilo4.3 kwa nji ya kawaida bila ya matatizo tunamshukuru mungu. Serikali tunaiyomba iwe inazianglia biashara hizi haramu pia.

Jodari,..kwa heshima na taadhima, haya uliyoandika hapa yanakufanya uonekane chizi...
1. Huduma ya upasuaji ama uzazi kwenye vituo vya serikali ni BURE. Wewe kutokana na kutaka 'better' service na utofauti, ulienda kituo binafsi (umesema mikumi). Yes huduma kwenye vituo binafsi ni ya kulipia. Ni huduma kama ilivyo huduma yoyote ile.
2. Laki sita pia ni hela ndogo sana kwa huduma ya upasuaji wa mke wako. Jaribu tu ku-google bei ya operation kama hiyo nje ya mipaka yetu, kisha urejee na kauli zako. Wangetakiwa wakuambia dola 3000-5000. Si unataka utofauti mzee wangu?
3. Kwamba mtoto ametanguliza miguu wakati wa uchungu??...kisha ukasafiri kwenda dubai, ukarudi ukamkuta hajajifungua wala kupata tatizo jingine ni aina nyingine ya uzandiki. Mwanamke hawezi kuwa kwenye uchungu kwa zaidi ya masaa 24 na mtoto akazaliwa salama,...talking from a proffessional point of view. Huyo mtoto na mama yake usingewakuta.
4. Kwamba maduka na hospitali za hapa kwetu hazina Folic acid???...ina maana kweli kwa kipindi choote cha ujauzito wa mkeo hakupewa FA??..maana hii ni dawa wanayokunywa kila siku tangu siku ya kwanza wakienda Antenatal clinic...sasa kama haipo Tanzania,..alitumia nini kipindi hicho chote??
5. Taarifa tu,..FA sio dawa,..ni Iron Supplement kumsaidia mama awe na kiwango cha kutosha cha damu,..pia inasaidia kupunguza risk ya congenita malformation. Haina kazi nyingine yoyote...waka HAIMGEUZI mtoto aliyekaa vibaya.
6. Kwamba umewanunulia akina dada wengi FA za uarabuni kwa kuwa za hapa kwenu ni unga,...tukuulize tu kuwa wewe ni mganga wa kienyeji??..ulijuaje kama ni hizo FA ndo zimewafanya wajifungue kawaida??..

Wakati mwingine, jaribu kusoma kwanza, una access ya internet,..jifunze, utaonekana mbumbumbu (no harm intended).
Kiukweli uliyoyaandika yanakutia aibu.

Kwa heri
 
Kwamba alitumia kwa miezi mitatu???....kwa maana nyingine huyu mama wakati unampeleka hospitali alikuwa na miezi sita ya ujauzito!!!....aliyekuambia kuwa mtoto anakaa hali ya kawaida (kutanguliza kichwa) kama anataka kuzaliwa akiwa na wiki 24 ni nani?....

ukipewa ushauri na mtaalamu na kama hujauamini,..tafuta elimu,..usijaribu kutaka kushindana na elimu/ujuzi,..utakuja kumuua mkeo siku nyingine

FA wanapewa kwa kipindi chote cha ujauzito....ulimkosesha mkeo FA kwa kutoamini dawa za hapa nyimbani,..matokeo yako unayajua mwenyewe,..ama kwa bahati nzuri wapo salama,..ila wangeweza kuwa na hali nzuri zaidi.

Kijijini kwetu katika zaanati hizi dawa zipo bro,..tena bure...si lazima Dubai
 
nafikiri wengi hajamuelewa mkuu kwa hiyo mada ni kweli kachanganya vitu viwili katika mada, kuanzia gharama za upasuaji, upatikanaji wa tiba na vile vile maadili ya madr kwa upande wangu naombanizungumzie kwa upande wa maadili wa madr ni ukweli usiopingika kuwa sasa hivi operation nyingi zimeongezeka kwa sababu kwenye vituo binafsi wanacharge pesa nyingi sana na mnaposema serikali ni bure sio bure kama mnavyofikiria lazima utoe pesa kuanzia nesi yule wa kukupangia ratiba kote huko lazima utoe pesa, sasa hivi madaktari wengi ukienda tu wengi wanakuambia utafanyiwa operation na hata wanawake wengi sasa wanataka operation kuwa wakifanyia upasuaji njia zao za utupu wa mbele wao unabaki vile vile so bado inakuwa kivutio kwa mumewe na vile vile tumbo linabaki vile vile bila michirizi michirizi hiyo ndio imani yao na vile vile hawataki kusikia uchungu, na hii inawapata wanawake wengi wenye kipato cha juu na cha kati, nina dada yangu ni muhanga wa haya makitu hana matatizo kabisa ila akifikia tu muda wa kujifungua ni kwenda kwa dr kalonzo pale mwanza sasa ni watoto wawili,
 
Wanawake wengine wanajitakia hizo operation ila kiukweli njia ya kawaida ni salama zaidi
 
Back
Top Bottom