Boran Jakutay
Senior Member
- Apr 8, 2023
- 110
- 255
Kama ulidhani kutokukamilika kwa mradi wa mwendokasi awamu ya pili kutoka Gerezani hadi Mbagala Rangi Tatu kunawakera wakazi wanaohangaika na usafiri kila linapokucha au kukuchwa unajidanganya. Ipo adha nyingine ya vituo vyake kugeuzwa madanguro, walalamikiwa wakubwa wakiwa baadhi ya askari polisi wanaodaiwa ‘kutengeneza fedha’ kupitia biashara hiyo ya ngono.
Japokuwa polisi na viongozi wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (Dart) wanasema hawana taarifa ya kinachoendelea katika vituo vya mabasi hayo, Mwananchi Digital imefanya utafiti na kujiridhisha kwamba biashara hiyo imeshamiri na inafahamika miongoni mwa wakazi wa maeneo husika wakiwamo viongozi wa serikali za mitaa.
Sio Kamanda Muliro tu, Ofisa Habari wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (Dart) inayosimamia miundombinu hiyo, William Gatambi alisema hana taarifa kuhusu kinachoendelea katika vituo hivyo.
Wakati Polisi na Dart wakitoa maelezo hayo, katika kituo cha mabasi hayo Mbagala Rangi Tatu biashara hiyo inaelezwa kushamiri na wanaoifanya wanasema wanalazimika kutoa fedha takribani Sh 10,000 kwa waliopewa dhamana ya kulinda raia na mali zao.
Inaelezwa kwamba, magari ya doria yanayopita kuanzia saa nne usiku hadi saa tano usiku hayakamati watu, lakini yanayopita kuanzia saa sita hadi saa saba usiku ndiyo yanakamata watu. Wakishakamatwa, wanapandishwa katika gari kisha wanachukuliwa fedha na kuachiwa waendelee na biashara yao.
CHANZO: MWANANCHI