Dar es Salaam imetumia mabilioni ya fedha kuziba mashimo barabarani, miezi miwili baadaye 80% ya mashimo yaliyozibwa yamerudi

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Kwa mtu ambae hana fani ya uhandisi angeona kwamba Dar es Salaam ya Chalamila ilifanya kazi nzuri sana miezi ya October na November 2023, kuziba mashimo mengi sana yaliyokuwa barabarani. Lakini baadhi ya mainjinia walituambia kilichokuwa kinafanyika ulikuwa ni utoto na kupiga fedha za serikali, kwa sababu mashimo yalikuwa yakizibwa kwa namna ya kutupia lami ndani ya shimo na kusawazisha juu. Walisema kuziba shimo kunafanyila kwa namna ya kuunganisha lami ya zamani na unayoweka, sio suala la kutupia tu lami ndani ya shimo, jambo ambalo lilifanyika bila hata kusafisha shimo kwanza na kulitengenezea mazingira ya kuunga lami ya kiraka na iliyopo. Matokeo ni kwamba lami za viraka zimebanduka baada ya miezi miwili tu.

Kuna mtu alisema baada ya wiki mbili tu, utaona mashimo yote yaliyozibwa yakirudi palepale. Alienda mbali kuwa huu ni namna fulani ya uzembe ambao unaweza kusema umechangiwa na Raisi Samia kutaka contract kama hizi wapewe wanawake na ma kontrakta wadogo, na hili likafanyika kisiasa. Watu wamepewa kazi kwa vi-note au kisiasa, na wahusika wanasema walishinikizwa kutoa hizo tenda kwa amri "toka juu". Kazi yote ikafanyika kimzaha sana.

Mabilioni ya fedha yalitumika, na watu wakawekewa pesa yao benki. Miezi miwili baadae viraka vyote vimebanduka. Tumerudi pale pale, na mashimo yakiwa chanzo kimojawapo kikubwa cha foleni za Dar es Salaam.

Hivi uongozi wa nchi hii kwa nini unafanya mambo ya hovyo namna hii? Upole wa Watanzania ndio unasababisha hili? Sasa hao mliowapa hizi tenda za kuziba mashimo, kwenye mkataba mliwapa muda kusema viraka vikibanduka ndani ya muda fulani watarudia hiyo kazi kwa gharama yao wenyewe? Ndio maana haishangazi ukiona nchi imepinduliwa baadhi ya viongozi wanapigwa risasi hadharani, au China inanyonga watu kama hao.

Chalamila yuko busy anafukuzana na changudoa mitaani, hili wala hataki kulisemea kwa waandishi wa habari kwa sababu ni la aibu kwa serikali? Au ndio tuseme anaona suala la changudoa ni la kipao mbele kuliko uozo huu uliofanyika kwa mabilioni ya fedha za walipa kodi? Au inawezekana pia ni kutokuwa na busara za uongozi akiona suluhisho kwa hili tatizo ni watu kuondoka Dar es Salaam kwenda mikoani ambako sijui hakuna magari?
 
Wanajenga miundombinu mibovu ili wajitengenezee hela kwenye marekebisho ya mara kwa mara.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Wanajenga miundombinu mibovu ili wajitengenezee hela kwenye marekebisho ya mara kwa mara.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
Sasa nimeanza kuelewa kwa nini viongozi wa Afrika wanapinga sana mapinduzi ya kijeshi yakifanywa katika nchi fulani. Wanahofia na kwao inaweza kutokea wanajeshi wakiona uozo umezidi na kuamua kuchukua hatua. Kuna nchi zilipinduliwa japo hazikuwa na uozo wa kiwango tulichofikia katika uongozi
 
Back
Top Bottom