meddie
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 434
- 125
Hii ndio capital city yetu lakini inashagaza na kutuangusha sana;
Kwa kuzingatia umuhimu wa Dar es Salaam kama Capital city, kunahaja kubwa ya wana dar kubadilika na kuhamasika kwa ajili ya kuleta mabadiliko nchini. Najua CHADEMA wanayo support kutoka Dar es Salaam, lakini kama ingekuwa katika kiwango kikubwa kama inayotoka mikoani speed ya mabadiliko ingekuwa kubwa zaidi!
DAR ES SALAAM PLEASE COME UP AND COME FOR CHANGE WE NEED!
- Uchafu
- Foleni; (mwendo wa kilomita 1 unakwenda masaa3). Watu tuliiii kisa amani!!
- Barabara mbovu na chafu ...tena ktk maeneo wanakoishi so called civilized community
- Watu wanalipuliwa na kufa kwa mabomu -hakuna maelezo wala uwajibikaji. Watu tuliiii kisa amani!!
- Mgao wa umeme masaa 24!! Watu tuliiii kisa amani!!
- Vingora kila wakati!! Mnasimama masaa eti kiongozi anapita (hujui anatoka wapi na kwa lipi hasa!)
- Ukiwa Dar utaona msafara wa magari asubuhi yakienda taratibu kuelekea mjini, jioni msafala unatoka mjini kuelekea Bunju, Mbezi, ruvu, mbagala kuu . . Mjini wahindi na waarabu kibao lakini kwenye msululu wa magari jioni na asubuhi huwaoni! Hayo ni magari acha wanaofuata reli!! Haya ndiyo maisha siku neda siku rudi.
- Ikija wakati wa uchaguzi utaona magari yamepambwa kijani, watu wamevaa t-shirt, kofia, kanga wanafuraha kama hawana akili mzuri!! Wanasikiliza mtu akiwaeleza upuuzi kana kwamba ukweli wa maisha yanayowakabili wameyasau/ama hawayaoni. Mkoa huu ndo CCM inajizolea kura kemkem!!!
- Usiku utaona kila kona mabaa yamefurika hakuna pa kukaa, (utafikiri kuna sherehe furani)! Night activity ni watu kwenda baa tu hakuna jambo jingine!! Utasikia kuna baa mpya imefunguliwa twende lakini ukifika bia ni ile ile!! Kwenye baa watu wanakaa kwa kustarehe utafikiri hawana hadha yeyote wala haja ya mabadiliko!!
- Ni mji umesheheni elite wa nchi hii lakini unakosa mchango na msimamo wa dhati inapokuja swala la kuchukua hatua za kuleta mabadiliko ya kweli kisiasa/kiuongozi hapa nchini! Ebu linganisha Dar es Salaam na mikoa kama Arusha, Mbeya, mikoa ya kanda ya Ziwa. Wasomi wengi Dar wanakaa kwanza wanamsikiliza JK anasema nini na wao wanaanza kusupport aakweli uvunjifu wa amani aaa udini!!!!
Kwa kuzingatia umuhimu wa Dar es Salaam kama Capital city, kunahaja kubwa ya wana dar kubadilika na kuhamasika kwa ajili ya kuleta mabadiliko nchini. Najua CHADEMA wanayo support kutoka Dar es Salaam, lakini kama ingekuwa katika kiwango kikubwa kama inayotoka mikoani speed ya mabadiliko ingekuwa kubwa zaidi!
DAR ES SALAAM PLEASE COME UP AND COME FOR CHANGE WE NEED!