Power G
JF-Expert Member
- Apr 20, 2011
- 3,886
- 1,194
Nina uhakika wengi wetu (kama siyo wote) katika maisha, tulishapenda, kupendwa, kuacha na kuachwa vile vile. Kwa hiyo katika mahusiano tunajua wazi kwamba penzi huzaliwa, hustawi na wakati ukifika hujifia. Lakini kabla ya penzi kufa ni viashiria vipi au dalili gani ambazo zikionekana, mhusika ataziona kwa mwenzake kuashiria kwamba penzi lake sasa liko ICU? Nadhani uzoefu wenu katika mahusiano utasaidia kujibu hili swali ili mhusika ajue mapema dalili aweze kutafuta dawa ya kuzuia penzi lake kufa.